Kwa hao watanzania wenye miaka 120+, maana yake walizaliwa miaka ya 1800s. Sasa ikiwa tu wale waliozaliwa mwanzoni mwa 1900s hawajui exactly walizaliwa lini kutokana na kutojua hata Kalenda ni nini, je mnathibitisha vipi mpaka kusema mtu ana miaka 120. Hao wa 1900s ukiwauliza tarehe ya kuzaliwa, wapo wanaosema mimi nilizaliwa msimu wa nzige, mwingine anakwambia msimu ule wa radi nyingi, sasa hapo unajuaje umri kamili wa mtu?
Hata ukiangalia watanzania wengi waliozaliwa 1950 kwenda chini wengi wao hawana hata vyeti vya kuzaliwa.