BMW Gear (automatic) Zimegoma

BMW Gear (automatic) Zimegoma

RRONDO

Platinum Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
60,417
Reaction score
139,271
Wadau, leo mchana wakati naendesha gari yangu gear zilianza kuingia kwa shida [gari ni 320i automatic] na baadae gari ikagoma kabisa kubadili gear nafikiri ili gomea namba nne au tano maanake nilikuwa kwenye junction ikawa inaondoka kwa shida,kama manual uondokee namba tatu!!

Nilipaki pembeni ya barabara maanake ilikuwa inaenda slow kwa shida sana,baada ya dakika tano nikajaribu kuondoka ingawa kwa shida lakini ilifika angalau 50kph,kufika home getini ikagomea hapo nikailazimisha ikaingia ndani kwa shida sana,inaunguruma lakini haiendi. Nikajaribu kupaki ikagoma,nikazima gari na nakaiwasha hapo hapo gear zikakubali nikapaki.

Jioni kama saa 12 nikajaribu kuiwasha, gear zikaingia vizuri tu,nikatoka nayo nikaendesha bila tatizo hadi 80kph nikarudisha kupaki. Sasa hapa najiuliza tatizo ni nini??
1.ni gearbox imeshachoka
2.transmission fluid ishachoka[niliibadili hata km 2000 hazijafika]
3.electric problem yaani gear hazijitambui

Kama kuna mtu ashawahi kuppata hili tatizo anipe mwanga maanake mimi kabla ya kwenda kwa fundi huwa napenda niwe na idea nini inaweza kuwa tatizo kabla hawajaanza kubahatisha!

CC: OLESAIDIMU MANI CYBERTEQ Kaizer
 
Pole mkuu..hapo inawezekana kabisa yote matatu au mojawapo...ila.kwa trans fluid uwezekano ni mdogo nina wasi wasi na 1 na 3 ..nenda wafanye proper diagnostics..pole sana
 
Inaweza kuwa hiyo namba tatu kuna .
 
Pole mkuu..hapo inawezekana kabisa yote matatu au mojawapo...ila.kwa trans fluid uwezekano ni mdogo nina wasi wasi na 1 na 3 ..nenda wafanye proper diagnostics..pole sana

hapa najipa moyo labda ile trans fluid magumashi....sitaki kusikia gearbox imekufa!!!
 
Inawezekana ATF ndo tatizo kwani kwa maelezo yako inaonekana gari ikipoa ndo gia zinafanya kazi kitu kinachoonyesha kwamba kuna tatizo la ATF kuhiti.
 
yeah....hata akili yangu inaniambia hivyo....baada ya kupaki kwa muda mrefu jioni nilivyoendesha ikawa poa
 
hapa najipa moyo labda ile trans fluid magumashi....sitaki kusikia gearbox imekufa!!!

Kwa nini ulibadili transmission fluid....huwa haichoki!
Kuna chance uliwekewa feki au aina isiyo sahihi.
 
Kuna sign yoyote inayoonesha kwenye dashboard wkt inaanza hili tatizo?
 
Watu wenye mangarangara utawajua tu!
unajua mafundi wa rejeta, gear box, sijui fundi umeme! X6 saa ngapi itagoma gear?

kwi kwi kwi. Kongosho salamu zako
Pole mkuu..hapo inawezekana kabisa yote matatu au mojawapo...ila.kwa trans fluid uwezekano ni mdogo nina wasi wasi na 1 na 3 ..nenda wafanye proper diagnostics..pole sana
 
Last edited by a moderator:
yeah....hata akili yangu inaniambia hivyo....baada ya kupaki kwa muda mrefu jioni nilivyoendesha ikawa poa

Na ukizingatia siku hizi vilainishi vinatengenezwa mtaani kama batiki
 
Hivi gari automatic ukiizima ikiwa kwenye gear, inakubali kuwaka tena bila kuweka parking?
 
haiwaki...mpaka parking au neutral....yangu stick inasogea kwenye position zote lakini haiendi.
 
Kwa nini ulibadili transmission fluid....huwa haichoki!
Kuna chance uliwekewa feki au aina isiyo sahihi.

mkuu nalijua hilo...ila gari imekaa muda sasa kwahio nikabadili,ni kweli wanasema usibadili lakini hata ukipitia forums za magari wengi wanabadili baada ya muda fulani.
 
Watu wenye mangarangara utawajua tu!
unajua mafundi wa rejeta, gear box, sijui fundi umeme! X6 saa ngapi itagoma gear?

kwi kwi kwi. Kongosho salamu zako

mkuu hamna gari isio haribika....tena hizi za bei mbaya ndio balaa....hata zikihisi hewa ni chafu matatizo.
 
Ingekuwa kuna tatizo lolote basi lazima sensor ingepeleka info kwenye ecu then ingetokea sign kwenye dashboard. ..kuna gari nilituma bongo nissan primera. ..ilinisumbua sana kwa style kidogo kama yako lkn yenyewe haikuwa na tatizo la gear. .....kuna fundi mmoja yupo kariakoo aliniwekea mafuta gani sijui ya kusafisha mfumo wote wa engine. ...ilisaidia sana maana nilikuwa nishakubali kutoa laki nne za kununua sensor badala yake nikatoa elfu tano tu. ......ngoja nimtafute bimkubwa bongo anipe namba ya huyo fundi kisha nikupe umpigie
 
Sioni mantiki ya kuibadili hydraulic fluid......
Ikibidi kubadili ni muhimu kuhakikisha unapata aina sahihi na ubora halisi!

mkuu nalijua hilo...ila gari imekaa muda sasa kwahio nikabadili,ni kweli wanasema usibadili lakini hata ukipitia forums za magari wengi wanabadili baada ya muda fulani.
 
Ingekuwa kuna tatizo lolote basi lazima sensor ingepeleka info kwenye ecu then ingetokea sign kwenye dashboard. ..kuna gari nilituma bongo nissan primera. ..ilinisumbua sana kwa style kidogo kama yako lkn yenyewe haikuwa na tatizo la gear. .....kuna fundi mmoja yupo kariakoo aliniwekea mafuta gani sijui ya kusafisha mfumo wote wa engine. ...ilisaidia sana maana nilikuwa nishakubali kutoa laki nne za kununua sensor badala yake nikatoa elfu tano tu. ......ngoja nimtafute bimkubwa bongo anipe namba ya huyo fundi kisha nikupe umpigie

thanks.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom