rr4
JF-Expert Member
- Mar 19, 2015
- 3,962
- 5,886
- Thread starter
- #21
...najua hujanielewa lakini tunavyoenda utaelewa.
Mwekezaji ku 'comply' na taratibu za nchi husika ina maana mtu anayewekeza China masharti atakayopewa kuyafuata ni tofauti na Amerika, Egypt, Kenya, South Afrika au DRC. Na yeye kwa sababu keshaona opportunity katika anachokihitaji atayafuata tu, mfano DRC ukienda kuwekeza maeneo ambayo serikali ina nguvu wanadai eti ni kuihakikishia famili na washirika wa watawala share yao na utapata ulinzi masaa 24 wakati ukivuna usikopanda na ukienda eneo ambako waasi wana nguvu basi wewe unamuona kamanda wa waasi na anakupa ulinzi na njia zote za eneo husika. Hapo usije kushangaa Joseph Kony aliwezaje kukusanya pembe za ndovu na kuziuza vipi ...na pesa alilipwaje na nani alimlipa ili kuendelea kumiliki siraha na kuwasumbua wananchi wasio na hatia. The more risk you take the more chances of making it ...urahisi wa kutajirika!
Vivyo hivyo na hapa acacia huenda walitanguliza 'conman' wao na akawahakikishia kuwa 'wakuu wanaingilika'. Na kwa vile hayo ndio yalikuwa mazingira waka 'comply' nayo wakaanza kuvuna na biashara yao ikishamiri huku sisi tukiendelea kukosa dawa na hata madawati ya kukalia!!! Naamini wangelikuwa Kenya pia wangefuata masharti ya huko vivyo hivyo wangelikuwa Japan au India. Inaumiza lakini ndio ukweli!
AMEN...............MAY THE LORD OUR GOD BLESS YOUR DAY MKUU.