Mzalendo_Mwandamizi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2007
- 1,116
- 4,773
Mkuu asante sana. Bila shaka Chadema watafanyia kazi jambo hili maana bahati nzuri viongozi ni member hapa, na kwa kweli ninavyowajua ni wasikivu sana!Kama bloga,nisingependa ku-comment lolote kuhusu blogu ya bloga mwenzangu.Hata hivyo,kuna mapungufu makubwa katika namna Chadema inavyoshughulikia habari na kuzisambaza kwa vyombo vya habari hususan blogu.
Mara kadhaa nimelazimika kuchukua picha hapa Jamii Forums (na kuweka shukrani kwenye post husika) baada ya kukosa ushirikiano kutoka kwa jamaa wa Chadema.Ifahamike kuwa wengi wa mabloga wanafanya shughuli hiyo kwa mapenzi yao tu ya kupashana habari (ukiweka kando baadhi ya wenzetu ambao blogu zao zina wadhamini).Sasa kama taasisi haijihangaishi kushirikiana na mabloga kuwezesha matukio au habari inazozihusu kuwekwa hadharani,kuna nyakati inafikia hatua kwa bloga kuamua kuachana na habari hizo.
Tatizo hili lilikuwa sugu zaidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.Tovuti ya Chadema ina mapungufu lukuki kwenye kuweka habari mpya.Lakini tatizo kubwa zaidi ni kama nilivyosema hapo juu kuwa hawajihangaishi kusambaza habari zao.Gazeti linaweza kujihangaisha kusaka habari kwa vile lenyewe linafanya baishara lakini kwa bloga ni tofauti.Kinachotusukuma wengi wetu ni dhamira tu ya ku-share habari na wanajamii wenzetu.
Kwahiyo,nimalizie kwa kutoa wito kwa Chadema na taasisi nyinginezo kutambua nafasi muhimu ya blogu katika zama hizi za utandawazi zinazotegemea sana teknohama.Pengine badala ya kuwahukumu bloga waifanyie nini Chadema,kuna haja ya kuihoji Chadema ifanye nini kwa mabloga ili habari zake zisambae mtandaoni.Haigharimu chochote ku-upload picha na kusambaza kwa blogu mbalimbali badala ya kutarajia mabloga wajihangaishe kusaka picha husika huku na huko.
Na Chadema ina mengi ya kujifunza katika namna teknohama inavyoweza kuleta mabadiliko tarajiwa,mfano hai ukiwa namna Obama na timu yake ilivyoutumia vilivyo mtandao (wa intaneti) katika kampeni zake za Uchaguzi Mkuu uliopita nchini Marekani.
Ndio,Chadema wanaweza...WAKITAKA!
Wadau nimeperuzi tena Blogu ya Michuzi na kujiridhisha tena kuwa ana hila na CDM, mpaka sasa haja weka picha za mazishi ya Kiongozi wa CDM Shinyanga, Shilembi ila zingekuwa za CCM haraka zinge kuwa posted as BREAKING NEEWZ
Unajua Magamba Watu Wabaya Sana!! Wanaua Proffessionalism za Watu Bila Hata Kuwa Na Huruma, Sijajua Huyu Ndugu walimpa Shilingi Ngapi????? Any way Mchumia Tumbo always Unapomshibisha Husahau Hata Kutumia Akili, Poor Issa Michuzi, Ghafla umejiua Kiproffessional!!
Kama bloga,nisingependa ku-comment lolote kuhusu blogu ya bloga mwenzangu.Hata hivyo,kuna mapungufu makubwa katika namna Chadema inavyoshughulikia habari na kuzisambaza kwa vyombo vya habari hususan blogu.
Mara kadhaa nimelazimika kuchukua picha hapa Jamii Forums (na kuweka shukrani kwenye post husika) baada ya kukosa ushirikiano kutoka kwa jamaa wa Chadema.Ifahamike kuwa wengi wa mabloga wanafanya shughuli hiyo kwa mapenzi yao tu ya kupashana habari (ukiweka kando baadhi ya wenzetu ambao blogu zao zina wadhamini).Sasa kama taasisi haijihangaishi kushirikiana na mabloga kuwezesha matukio au habari inazozihusu kuwekwa hadharani,kuna nyakati inafikia hatua kwa bloga kuamua kuachana na habari hizo.
Tatizo hili lilikuwa sugu zaidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.Tovuti ya Chadema ina mapungufu lukuki kwenye kuweka habari mpya.Lakini tatizo kubwa zaidi ni kama nilivyosema hapo juu kuwa hawajihangaishi kusambaza habari zao.Gazeti linaweza kujihangaisha kusaka habari kwa vile lenyewe linafanya baishara lakini kwa bloga ni tofauti.Kinachotusukuma wengi wetu ni dhamira tu ya ku-share habari na wanajamii wenzetu.
Kwahiyo,nimalizie kwa kutoa wito kwa Chadema na taasisi nyinginezo kutambua nafasi muhimu ya blogu katika zama hizi za utandawazi zinazotegemea sana teknohama.Pengine badala ya kuwahukumu bloga waifanyie nini Chadema,kuna haja ya kuihoji Chadema ifanye nini kwa mabloga ili habari zake zisambae mtandaoni.Haigharimu chochote ku-upload picha na kusambaza kwa blogu mbalimbali badala ya kutarajia mabloga wajihangaishe kusaka picha husika huku na huko.
Na Chadema ina mengi ya kujifunza katika namna teknohama inavyoweza kuleta mabadiliko tarajiwa,mfano hai ukiwa namna Obama na timu yake ilivyoutumia vilivyo mtandao (wa intaneti) katika kampeni zake za Uchaguzi Mkuu uliopita nchini Marekani.
Ndio,Chadema wanaweza...WAKITAKA!
Wadau nimeperuzi tena Blogu ya Michuzi na kujiridhisha tena kuwa ana hila na CDM, mpaka sasa haja weka picha za mazishi ya Kiongozi wa CDM Shinyanga, Shilembi ila zingekuwa za CCM haraka zinge kuwa posted as BREAKING NEEWZ
Haya mawazo bado tunayo?...kuna mzungu mmoja alikuwa anaisifia jf mpaka raha..
Wanayo na sijaona habari ya msiba huu kwenye tovuti yao,duh! kazi ipo!Hivi chadema hawana website... au hata blog!?
Jibu swali,mbona website ya CDM haijatangaza?Michuzi ana benefit na serikali iliyopo madarakani. Huwezi kukata mkono unaokulisha hata siku moja!