Bloggers wa nyumbani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bloggers wa nyumbani!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Masikini_Jeuri, Mar 22, 2011.

 1. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  nashukuru kwa kuwa mstari wa mbele kutuhabarisha katika tasnia mbali mbali lakini niloliona leo ni mfululizo wa makosa kadhaa ambayo yakiendelea mtapoteza maana halisi ya kutuhabarisha na kuwa ni kutupotosha.

  Kuna suala la kuandika habari kishabiki........sijui kam ni sahihi niseme kuandika habari ili kuwa maarufu; sasa katika uandishi wa namna hii katika nyingi ya blog zetu unakutana na habari isiyokamilika au ambayo haiweki wazi chanzo na wakati mwingine ikiwa imepotoshwa mfano halisi kwa leo ni suala la huu msiba wa wasanii! Ukiipitia blog ya Machella MACHELLAH 0713 470 492 machellahm@yahoo.com: KUNDI LA BENDI YA FIVE STAR LAPATA AJALI NA 13 KATI YAO WAFARIKI DUNIA.

  Anaripoti kuwa amepokea habari toka mkoani Pwani na Majeruhi wamekimbizwa hospitali ya Tumbi! Wakati tukio limetokea mkoani Morogoro na majeruhi wako hospitali ya mkoa wa Morogoro!

  sasa waweza kadiria ni usumbufu kiasi gani jamii iliyokumbana na habari kama hii imeupata; kama mtu hakuwa na haja ya kucheck na other sources!

  Tujaribu kuwa makini bloggers! Umaarufu utakuja wenyewe na sio kwa kukurupuka namna hii!
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kuna haja ya sheria za kiuandishi kuwa aplied na katika blog pia, na si katika magazeti na redio peke yake.
   
 3. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  umenena kweli,tatizo huwezi kudhibiti blogs,mtu anaweza kuwa yuko korea lkn anaripoti matukio yaliyotokea tanzania wakati hana vyanzo vya uhakika.
   
 4. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,229
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Tuna miaka mingi kurekebika katika hili!..Ni jambo la kusikitisha pale habari isiyo na kichwa wala miguu inapotoka kwenye gazeti lenye msururu wa wahariri na hata baada ya kubainika ilikua ya kupotosha bado kusiwepo neno la kuomba radhi!
   
Loading...