Blog zinazoonyesha Picha za Marehemu wa Ajali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Blog zinazoonyesha Picha za Marehemu wa Ajali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by luck, May 25, 2012.

 1. luck

  luck JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Oct 3, 2009
  Messages: 769
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 80
  Suala hili limejadiliwa sana miezi michache iliyopita lakini nimeamua nililete hapa baada ya kuona baadhi ya blogs zikiendelea kutoa picha za kutisha za marehemu pindi ajali zinapotokea. Lately kuna ajali ilitokea mkoani Iringa (mtanisahihisha km nimekosea) na baadhi ya blog zilitoa picha za kutisha za ajali hii iliyohusiha gari dogo saloon na fuso na kusababisha vifo kadhaa ikiwamo dereva wa saloon.

  Blogger mtambue kwamba marehemu hawa ni wenzetu hivyo wanapaswa kuheshimiwa na kusitiriwa, marehemu hawa wana ndugu, jamaa na marafiki. Je ndugu, jamaa na marafiki hawa watajisikiaje pale watakapoona picha za ndugu zao waliofariki zikizunguka kwenye mitandao? Just imagine unaona ubongo wa baba au mama yako, mtoto wako e.t.c utajisikiaje.

  Bloggers acheni mchezo huo, vinginevyo tutalia hadi mpatiwe udhibiti kwa kushindwa kutumia busara!
   
 2. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mi sioni tatizo!kwani sheria imezungumzia?lakin binafs sion tatizo watu tungependa kuona taarifa za wazi na picha za wazi ili tujifunze kuepuka ajar zisizokua za lazima.ingekua ni picha za aliyebakwa hapo sawa ila za maiti SIONI TATIZO,labda nielimishe kidogo
   
 3. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  kala bas manki ww
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  jana ITV wameonyesha mwili wa marehemu mwanafunzi wa tumaini univasiti aliejinyonga...tena akiwa live live kaning'inia kwenye kamba....
   
 5. luck

  luck JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Oct 3, 2009
  Messages: 769
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 80
  Mkuu,
  Huoni tatizo? Fikiria baba/mama yako mzazi kapata ajali katapakaa barabara nzima afu watu wanampiga picha na kumweka mtandaoni! Kama utakuwa OK kwa hilo mimi nafikiri una tatizo kubwa zaidi kichwani
   
 6. Masulupwete

  Masulupwete JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 659
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Hii kitu iliwekwa kwenye blog ya mjengwa. Nafikiri kuna tatizo la moderation kwenye hiyo blog. Mjengwa anapaswa kuwa serious na hili.
   
 7. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sijakuelewa
   
 8. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anavyokufa mnyama ndivyo tunavyokufa sisi
   
 9. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hakuna ubaya,acha taarifa itolewe kwa upana wake,,watu wanajifunza zaidi kuepuka mambo ya uzembe barabarani, hata kama angekuwa nani kama ni kutokea/kufa tayari ishatokea
   
 10. A

  Activist p Member

  #10
  May 26, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haipendezi hata kidogo bwanaa!
   
 11. Deejay nasmile

  Deejay nasmile JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,916
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Ndio maana blog yangu ni ya entertainment zaidi
   
 12. U

  UmtwaAlumbwagwe Member

  #12
  May 26, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njoo ufanyiwe maombi.
   
 13. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mimi nimesema SIONI TATIZO, lakni pia nikaomba kuelimishwa kama kunatatizo na liko wap hasa,nilitegemea unielimisha labd tatizo lipo kihaki za binadam au kikatiba badala yake unanikashifu/unanitus mi nasema tena hata kunitusi kwako pia SIONI TATIZO
   
Loading...