Blackmailed, please help! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Blackmailed, please help!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtu B, Oct 18, 2009.

 1. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nimehamia nyumba ingine hivi karibuni, ya kupanga. Ni upande wa nyumba, chumba kimoja na sebule. Kasheshe ni jirani wa upande wa pili. Dada mmoja hivi. Hapo miaka ya nyuma kidogo nimewahi kuwa na tabia (mbaya) ya kutembelea maeneo ya burudani ambako wanapatikana 'dada poa', na mara kwa mara nilikuwa namchukua huyu dada. Nimeacha hiyo tabia siku hizi. Lakini tangu nimehamia hapa, huyu dada kuniona tu anaanza tabia ya kunichangamkia sana na kuonesha kunifahamu mno. Mimi naona aibu kuonekana nikiwa nae hasa kwa sababu ya shughuli yake, na pia kwa sababu tabia hiyo nilishaiacha. Lakini alivyogundua namkwepa, ameanza tabia mpya, ya kuja kwangu kuomba hela. Na kwa kuwa sipendi aonekane kwangu, huwa nampa hela anayoomba haraka ili aondoke. Sasa kazoea na naona ananinyanyasa. Majuzi alikuja kuomba elfu 20, nikaona amezidi nikamweleza siwezi kumpa. Akatishia hatoondoka hadi nimpe hizo hela, na nikizidi kumbania atafichua siri yangu. Kusema kweli natishika, na kodi nimeshalipa ya mwaka! Ushauri plz.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Wewe acha ubwege wewe,hakuna aibu kwa mwanaume kuchukua dada poa,
  aibu kama wewe ungekuwa unajiuza na kulambwa.....
  Wewe mwambie hutaki akaseme popote.....
  Mwambie mkeo huyo dada ni cd uliwahi kununua huduma zake zamani,

  ukiendelea kumlipa basi kuna siri nyingine labda na sio huyo ya kununua
  huduma.....
   
 3. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nilipo highlight! Usisuthubutu kumwambia mkeo uliwahi...mwambie huyu malaya tuu ananifuata ...fuata...halafu huyo cd usimuendekeze kihivyo..biashara si iliisha zamani..don't be weak brother.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hujaweka sawa hapa: je unaishi na mkeo/familia?Kama uko mwenyewe, ni wazi hawezi kuogopa kuja na kuomba chenjichenji/rizki, maana kama wewe umeamua kuachana na tabia hizo, yeye hujamtaarifu, and any offer or refusal must be communicated to the intended party! Kwahiyo anatest zali ili kamavipi mpeane huduma kwa hapohapo jirani!Lakini kama unamaanisha, mkataze kwa kumwangalia machoni...i mean be serious, maana hakudai kitu(unless kama ulikuwa unamkopa huko nyuma)!
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,813
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana nawe kabisa Mkuu Tumain, na Mkeo siku zote atakuamini wewe badala ya changudoa. Usimpe tena hata senti tano achana na woga wako na uwe tayari kukabiliana naye kwa nguvu zote.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  bubu huoni kuwa ukimtangaza huyo dada kuwa alikuwa
  ni changudoa ndo itasaidia kumuumbua na aibu itampata...
  Na pia ukimweleza mkeo kuwa uliwahi kununua huduma zake
  zamani kabla hujampata yeye......itasaidia kumfanya
  ajue kuwa zamani ulikuwa hujatulia lakini sasa umetulia..
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kumwambia mkeo is a NO NO ....(na kwmbia hii from mwanamke point of view).....kama unaye huyo mke manake hukusema.

  wanawake wanatabia ya kutopenda kuambiwa ukweli japo wanaujua, kumkiria kosa lako mwanamke japo la zamani ni mbaya.

  usimpe pesa huyo changu, akikutangazia wewe unakauka kwa mkeo unamwambia aa zamani nilikuwa namuona viwanja ....sasa ananifanya ananijua sana (mkeo hapa atajua kaa ulitoka nae, lakini ataridhika kuw hakuambiwa maneno hayo direct)
   
 8. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wakubwa ni kuwa mie bado sijaoa, hapa nilipohamia najitahidi kujiweka sawa, ili mazingira ya kumpata mchumba yawe ya kumjengea matumaini huyo mchumba mtarajiwa. Lakini huyu cd naona ananichafulia kiaina, mfano ikitokea siku nikampata ninayeona anafaa, nina hofu kuwa majirani wanaweza kumwambia kuwa nina mazoea na huyo cd. Halafu sijui nimepatwa na hofu ya kiasi gani, sithubutu kuzungumza na huyu msichana kwa zaidi ya dakika 5, kila wakati nakuwa na hofu kuna watu wanatuona na kutusikia, na yeye anautumia vizuri sana huo mwanya kuweka madai yake. Siku ile aliyokuja kuniomba (kunipora, maana sikutaka kabisa kumpa) sh elfu 20, alianza kuniita kutoka mbali nilipoingia tu getini! Na alitumia jina la bandia nililokuwa namwambia zamani tulipokuwa tunaonana viwanja. Hiyo ilianza kuniharibia maana hapa majirani wengine wananifahamu kwa jina langu halisi. Nikaanza kuhisi watu wakinisikia nina majina mawili watanihisi vibaya, nikamwomba asitumie hilo jina bandia, akagoma akadai ataniita hivyo kila siku ati ndivyo alivyonizoea!

  Na pia nilishamwambia kuwa nilishaacha tabia ya kuchukua dada poa, lakini yeye pia akanijia juu: ''...kwani mimi ndio unaniona malaya sasa? Kama mimi malaya na wewe pia malaya..!" Sasa kila nikiona maongezi yanazidi kuwa marefu huwa nampa hela aondoke watu wengine wasitukute tukiongelea mambo hayo.

  Sijui niwaelezeje undani wa embarrassment ninayopata, lakini mwenzenu nasumbuka vibaya.
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  pole sana,huyo dada kashagundua wewe uko weak...
  We siku moja mkaribishe ndani
  halafu mshushie vibao vya nguvu.....
  Ikiwezekana na mikanda umcharaze....
  Utakuwa umemaliza kesi.....
  Kuwa strong.....
   
 10. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mkubwa nadhani haya mambo wengi wamepitia kutokana na usingle na mda wa kazi unabana sana hata kumtafuta demu inakuwa sometime ngumu sana so inabidi kuzama sehemu kuchukua mambo fulani......

  ila sasa kuna mdau hapo juu kakushauri kwamba mwambie mke wako kama unae nakuomba usiharibu uhusiano wako kufanya hivyo usimwambie kabisa maana wanawake wapo weak sana yaani.......utamwambia utaona umefanya vizuri kumbe ndio utaharibu kabisa,mwanamke wako anaweza kwenda kutembea na mwanaume mwingine ukigundua ukimuuliza kwa nini umefanya hivyo atakuambia kwamba wewe mbona before ulikuwa unatembea na cd....So kuhusu kuogopa usiogope mkubwa wewe mtoto wa kiume mpe kubwa kuliko tu hatosogea hapo nyumbani,wewe mwambie kwamba sihitaji hudumu yoyote na ukiwa umemkunjia sura hatosogea hapo na wala hatokuomba hela...

  ila kama akija anataka hela alafu unamchekea chekea duu hapo kaka kazi unayo tena kubwa sana.....Unajuwa kama kuahibika sisi wanaume tunahaibika sana yaani lakini sio kwa mwanamke kama huyo......
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Wanawake pia wapo tofauti,wengine hawa mind kujua ukweli
  ili mradi ilikuwa zamani kabla hujakutana nae...
   
 12. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180

  Mkubwa ni sawa lakini hapo ukishamwambia hiyo huo mda mwanamke wako atakuwa katika hali gani akigundua kwamba ulikuwa unakwenda kutafuta CD...Nadhani wanawake sio wakuwaamini kuwaambia kila kitu...ila pia sikatai anaweza kumwambia na inategemea pia...ila kwa mimi siwezi kuthubutu kumwambia mwanamke wangu.......Pamoja mkubwa!!
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,813
  Trophy Points: 280
  Mkuu Boss nakubaliana nawe huyu njemba kumbe bado ni single hivyo anaweza kabisa kusema kwamba aliwahi kununua bidhaa hiyo na sasa ameachana na tabia hizo, lakini yeye na mke mtarajiwa inabidi wakapime ili kuhakikisha wote wako salama.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,813
  Trophy Points: 280
  Unaweza kumuita hata mwizi maana anataka kukuharibia maisha yako sasa. Umemuomba kistaarabu aachane nawe na asitumie jina lako la bandia lakini hataki kukuelewa sasa ama zake ama zako inabidi upange mkakati wa kukabiliana naye au atakuharibia reputation yako mtaani.
   
 15. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 16. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ndugu yangu haupo pekee yako...hata mimi nilikuwa na hako kamchezo ka kwenda kupoza kiu kwa hao wazuri. Siku moja nikagongana nae peupee..tena nilikuwa na maza na watu kibao niliokuwa tunaheshimiana nao. Mwanangu si akaanza ujinga wake maana wale wameishiwa AIBU....oooh darling afadhali nimekuona mbona kimya..

  Basi nilimbalasa kama simjui ilibidi watu wote wacheke. Nilimpa laivu wapi tumeweka makubaliano ya kuwa mapenzi, tumefanya biashara imeisha pale nikamtishie kumpeleka polisi kwa kunidhalilisha. Kwahiyo mwana weka yabisi kwenye macho mpe laivu...mtoto wa kume asifiwe huruma kaka ooh!
   
 17. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Mkatalie mwambie sina pesa, tena na macho yako yawe makavu wala usimchekee. . Tena akija hapo mtimue kabisa mwambie wala huogopi kama siri na aseme.Atakuja kukutilia mchanga kwa gf wako.
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ....wala usithubutu kumtangazia alikuwa anatembeza duka, kuna wengine ukianza wao wanamaliza, "mteja mwenyewe dakika hafikishi, ukikohoa yeye nje na kambilimbi kake!" ...acha kabisa...

  dawa ni kutompa tena pesa, thats it!
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  teeeh teh wajukku zangu bwana..huna haja ya kumpiga mikanda wala vibao.mwambie sikupi hela na niashara yenu iliisha miaka hiyi ulipokuwa unanunua hudumua.au ulimkopa mkuu sasa unaogopa ataharibu?hahahaaaaa
   
 20. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wakubwa nashukuru kwa ushauri. Nimemtoa baru na nafikiri kanielewa. Kumbe na mwenyewe anaogopa kupewa notisi na mwenye nyumba, hapo ndipo nilipoumizia. Na sijatumia hata senti. Yaani nimejiona mjinga sana kwa pesa zote ambazo amekuwa akichukua kwangu. Nawashukuru. Nimejifunza.
   
Loading...