Je hii simu inatofauti gani na original?
Nataka kuinunua lakini naogopa.
Je simu za kichina zinakubali internet configuration ya mitandao yetu?
Ku-deal na vitu vya kichina, unahitaji kuwa makini sana hasa kutokana na udanganyifu wa wafanyabiashara wa kibongo.
Wachina kwenye maisha yao kule kwao, huwa wanatengeneza kila kitu kwa ubora tofauti ili kukidhi uwezo wa wanunuaji tofauti tofauti. Yaani hata kama unataka Kiatu cha
Nike au
jeans ya Levi's, wanatengeneza kwa viwango mbalimbali vya ubora, ili hata kama mtu ni maskini sana naye japo avae
Nike hata kama ni kwa mwezi mmoja. Na yule mwenye nazo naye anatengenezewa yake ya bei kubwa.
Kuna vitu unaweza kuwa umenunua Bongo au nchi zingine, ukawa umevipenda ukifikiri vimetengenezwa ulaya, kumbe ni mchina tu.
Hivyo, si kweli kwamba vitu vyote vya wachina ni vibovu, ukweli ni kuwa wafanyabiashara wa kiafrika huwa wanaenda eneo linaitwa '
Xiaobei lu' na '
San yuanli' kule
Guangzhou na
'Wuyi' kule
Zhejiang, wananunua vitu vya ubora wa chini, halafu wanavipeleka Africa na kuviuza kwa bei kubwa kama vile ni vya ubora wa juu. Na hapo ndipo mnapoliwa.
Vinginevyo kama unakaa ulaya, utanunua vitu vingi kutoka China ambavyo vina alama ya CE (kuthibitisha ubora kwa soko la ulaya) na vitu vitakuwa ni vizuri tu. Sie watz na maneno yetu mengi halafu TBS yetu ipo TATU BILA na tunashindwa kuhakikisha ubora wa bidhaa zinazoletwa na wafanyabiashara wetu.
Sasa kwasababu hatuwezi kutofautisha
Original na
fake (hata kama vyote vinatoka China au kwingineko) dawa pekee kwa mteja ni kununua kutoka kwenye duka lenye
warranty walau ya miezi 6. Mambo ya kununua simu kwenye maduka ya Temeke, kwa bei rahisi, halafu unataka iwe na function zote, hapo inabidi uwe na bahati pia.