Blackberry walikwama wapi (utawala wa iphone & android)?

Miki123

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
288
502
Brackberry moja ya kampuni iliyouza smartphones kwa sehemu kubwa ya dunia. Unaikumbuka app ya BBM ilivyokuwa inaelekea kuipeteza facebook.

Ilifika hatua brackbeery ilikuwa na marketshare ya zaidi 50% marekani na 20% duniani, unajua ukiliteka soko la US kwa kiasi hiki basi hata huko kwingine ni rahisi.

61gJ8KtFmiL._AC_SX466_.jpg


Mtu aliyemiliki smartphone za brackberry alionekana mjanja, lakini kuanzia mwaka 2011 mambo yalikuwa tofauti, simu za iphone na android zilianza kutawala na soko la brackberry limekuwa likianguka kama maji yanayotelemka toka mlimani.
1587884501293.png

Leo hii hizi simu zinazidiwa hadi na tecno, mtu akiambiwa achague kati ya blackberry na tecno atachagua tecno nina uhakika.

BB walilazimika kuhmia kutumia android os baada ya kampuni ya kichina ya TCL kununua upande wa kuunda hardware lakini wapi hal si hali. Toleo la mwisho la Blackberry ni Blackberry key 2 le la mwaka 2018 hakuna toleo jipya, hii inaonyesha jamaa bado kabisa.
blackberry-key2-le-1.jpg

Hawa jamaa kwa nini wameshindwa kushindana kabisa?
 
Jamaa niliwakubali sana hawa sijui walikwama wapi mm niliituma mpaka z10 ndio ilikuwa blackberry yangu ya mwisho kutumia.
 
Kwamba BB na Tecno mtu anachukua tecno.nyinyi wanazi wa tecno mna tabu sana.

Ukiiweka BB culve 9900 na tecno 12 kama hujamwambai anayechagua chochote,kwamba hamna hata whatsapp mule mtu ataokota BB,amini nakwambia,bidhaa premium haishuki mvuto believe me.

Kilichoitoa BB sokoni ni uvamizi wa OS huru kabisa duniani, android wakati BB os ameshakubali matokeo,apple nayeye akapata mwanya wa kuwa mpinzani mkuu wa android,hakuwa tayari kurudia makosa ya BB.

Kilichomnywa BB ni kosa dogo tu,OS na simu yenyewe kwa ujumla ilikuwa haimpi mteja furaha ya mwisho, nakumbuka simu niliyokuwa nayo ilikuwa haina torch,mpaka uistall bb store,haina screenshot mpaka uistall bb store.camera ya mbele hamna.akina apple na android wakaona fulsa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BBM na Facebook ni vitu viwili tofauti.

BBM ni Instant messaging Platform/ App

While

Facebook ni Social networking platform/ App

Kuna concept muhimu sana watu huwa hawajui kuhusu hii mitandao. Sio kila mtandao unaokuwezesha kuwasiliana ni Social netiwork.

Mfano Whatsapp sio social network na haina sifa hizo kwa sababu ili uweze kiwasiliana na mtu lazima mfahamiane out kwanza ndio uwasiliane nae on whatsapp

While Facebook unaweza mtafuta hata Donard trump ambae huna hata namba yake na ukawasiliana nae.

Soo mitandao kama BBM, Messenger ni mitandao/ inayoitwa instant messaging app ambazo zinatoa huduma ya mawasiliano ya papo kwa papo.

In sight of mambo ya BB, Hao BBM ilikiwa ni lazima wafichwe tuu na facebook. Maana facebook ina sifa mbili. Ambazo ni Instant messaging ( Massenger) na facebook ya kawaida kwa ajili ya social networking

Issue ingine ni DATA PLAN. Ililazimu ili upate huduma nzuri za internet inahitaji huwa na bundle la blackberry kitu ambacho watu wengi walikuwa hawapendi

Furaha zaidi watu waliipata kwenye OS huru/ Opensource baada ya kuwa vitu vingi ambavyo kwenye BB havikuwepo. Ki ufupi jamaa walishindwa kujua dunia inataka nini.

Emaphakadeni
 
miki123,
Kosa lao kubwa ni kufikiri wanajua watumiaji wanachotaka, na kushindwaung'amua mwelekeo wa soko la simu, Pia msumari wa mwisho illikuwa Blackberry stormwaliyoitoa pasipo kufanya research na kutuliza muda eti wapambane na iphone.

Walipoona iphone CEO wao alistaajabu na kusema able wamehamishia mac kwenye simu ila akahisi haitofanikiwa kwakuwa zitafanya mitandao icrash kwa kuzidiwa na demand ya data na pia kutokaa na chaji.

Wao wallidhani simu kukaa na chaji ni hitaji lamuhimu sana kwa mtumiaji. Pia back in the days wakati BB messenger imeshika hatamu, waliwahi ombwa na igeuzwe kuwa standard messeging application kwa simu zote, wakaringa.

Hilo lilikuwa kosa kubwa sana.
 
Nafaka, mkuu blackberry storm imetoka 2008,iphone ya kwanza imetoka 2007.

kwa muonekano wa kwanza haikufikiriwa hata kidogo kama apple atakuja kum charange BB.mwaka mmoja still apple hakuchukuliwa kama amefanikiwa,zaidi ya kuonekana bado idea yake ni mbovu.

balaa limeanza 2010.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
miki123,
North America (usa na canada) wanapenda vya kwao zaidi, ni eneo ambalo hype na marketing gimmicks vinasaidia zaidi kwenye mauzo kuliko uwezo wa Kitechnology ulio nao.

Zilivyokuja iphone na Hype zake wote walikimbia BB na kuhamia kwenye iphone.
 
mkorinto,
Mkuu mpaka blackbery anatoa blackberry storm ni kwmba alifuatwa na verizon atengeneze simu itakayo compete na iphone, maana ilikuwa wazi kwamba apple kafanya kitu cha ajabu kweli ambacho kiliwatisha watengeneza simu wengi. Wakaingia maabara na muda uko limited wakatoa boko la blackberry storm.

Lilipofail, na baadae huduma zao za bb services zikaja kubuma mauzo yakashuka wakahisi labda watu wanataka new os, yani mpaa muda huo walikuwa bado hawajajua wanapokosea, huenda wangejua mapema wakarukia basi la android lingewasaidia.

Hivi unajua wakati Steve Jobs ana introduce iphone, Google walikuwa tayari wako mbioni wanatengeneza simu ambayo ingeingia sokoni, after launch ya iphone walicancel project na investment ya hiyo simu na kauanza upya.

Apple aifanya kitu kibaya sana aliaua balaa
 
Nafaka, usiseme apple, sema steve jobs.

huyu jamaa hakuwa mtu wa kawaida.kwanza huwa sipendi na sioni kama ina haja ya kuwasifu apple kama kampuni na kumzika jamaa kizembe namna hiyo.

jamaa aliwaza mbali tu kwamba,simu inatakiwa iwe na kioo kikubwa,button ziondolewe.wengine wakahisi utani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom