BlackBerry Network Problem

Tumsifu Samwel

JF-Expert Member
Jul 30, 2007
1,407
159
Wakuu habarini za asubuhi?

nina blackberry yangu 8310 curve nilitumiwa toka Canada ,toka nimetumiwa mwaka jana sijaweza kuitumia kwani inasumbua kwenye network ina potea na kurudi na hata ikitulia siwezi kupiga simu wala kupokea ila mnara wa network unaonekana uko full na kuna kimshale kina cheza cheza, haikamati mtandao wa Zain na vodacom nikiweka sim card ya vodacom/zain kila kitu kinaonekana kwenye hizo line tatizo lina kuwa kwamba kwenye network haipatikani na wala kimnara cha mawasiliano hakionekani..


Niliwapigia zain na kuwaambia tatizo langu wakaniambia ni wapelekee,nilipo wapelekea walijaribu kuweka setting zote lakini hawakufanikiwa wakaniambia simu yangu ime blockiwa kwenye server ya blackberry hivyo siwezi kutumia kwenye mtandao wowote wa simu ambao una mawasiliano na backberry server akaniambia ndio maana haikubali sim card ya zain/voda kwani mitandao hiyo ina services za blackberry server akaendelea kuniambia tigo/zantel itakubali kwa kuwa hazina huduma ya blackberry,akaniambia solution ni kupeleka kwa mafundi wakai-flash siku ipeleka kwa kuwa ninazo software za kuflashia BB na jana nimei-flash na kuweka BB OS upya lakini tatizo limebaki pale pale. .

Sasa ukija tigo/zantel inakubali vizuri tu tatizo lina kuja kwamba siwezi kupiga simu na kupokea simu wala sms na hii inatokana na network kutotulia na wakati napo karibu kupiga simi kwenye bar ya network kuna kidude kama mshale hivi kina jitokeza na kuanza ku-blink blink..

Nimeingia kwenye setting/ advanced option/sim card, nika type MEDP zikaonekana hizi setting hapa chini (kwenye picha) ambazo zinaonekana ziko disabled zote na hamna option ya kuzi
attachment.php

anable,nime jaribu ku-type MEP na Ku-hold ALT + 2 iliku-anable sijafanikiwa kwa kweli..
Naomba mdau yoyote ambaye anaweza kunisaidia ni jinsi gani nita unlock hii BB yangu nitashukuru sana…

Natanguliza shukran zangu kwenu.
 
nenda kwenye drive c,program file,common file,research in motion,apploader, delete file limeandikwa vendor hilo ndio linatumika kublock
 
nenda kwenye drive c,program file,common file,research in motion,apploader, delete file limeandikwa vendor hilo ndio linatumika kublock
Asante kwa ushauri wako ndugu, ngoja niufanyie kazi, naona kuna file mbili la Vendor na vendor.temp ni delete zote au ni delete hilo moja la vendor pekee?
 
Nimenufaika na hii thread. Asante Dr. Phone. Cuthbert, kale kamshale kanobleak bleak ndio link ya radio sign toka kwenye BB yako kwenda BB inerprise server ya BB, ndio uthibitisho BB yako iko online ila iko blocked.

Angalizo, kama ilipigwa, na ilikopigwa iliacha 'issue', ukitumia Zain au Voda, hiyo handset itaregister upya hivyo kuweza kutract down.
 
Hizi simu ni vigumu sana kuzi unlock kwenye network, kwani inapo kuwa hewani wanai-monitor moja kwa moja.
 
Try Nokia 3310...Its a solid Rock mobile phone....haina mbwembwe zote hizo...utapiga na kupokea simu bila matatizo kaka........
 
Hah hah ilipigwa ju kwa ju nini huko Canada,BB kwa kawaida hapa TZ kama imepatikana kihalali na haikufungwa ,huwa zinafanya kazi tu kama kawaida,hapo mwanzo mimi nilikuwa na BB Storm 9500 nilipata kutoka Uingereza ,hiyo BBS ilikuwa imesajiliwa na Vodafone,kutumia kama simu ilikuwa poa kwa mitandao yote lakini mambo ya BIS ikawa ni Vodacom tu ndio unaweza access lakini kwa Zain ikawa haiwezekani.Nilichofanya ni kutafuta BBB 9000 ambayo ndio natumia Zain.Kwa kifupi BB zina mfumo mgumu sana wa ku-unlock.Huenda jaribu kumuona jamaa mmoja pale mtaa wa Mosque anaitwa Muna au jamaa pale Soppers plaza IB shop ghorofani.
 
Back
Top Bottom