Binti Yangu na Paka Wake

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
MBALI NA PAKA WAKE NA MWENYE PAKA MBALI NA NYUMBANI

Wingu limetanda na vua linadondoka ile mvua Mwingereza atasema, "It is raining cats and dogs."

Mvua na wingu jeusi huleta kitu kinaitwa, "melancholy."

Ikiwa kwa bahati mbaya hujui neno hilo muulize Prof. Google.

Always at your service.

Hii ni kwa kawaida.
Sasa kwangu mimi changanya na uzee.

Nasikiliza ''rhythm of the falling rain...''
Si ile nyimbo bali nasikiliza sauti ya mvua yenyewe inavyonyesha.

Wakati mzuri wa kuomba dua.

Majonzi yapo sababu ni hali ya wingu jeusi na kiza cha mchana wa saa saba.

Lakini hakuna "thunder and lightning," ile ya "Three Weird Sisters," katika Mcbeth kana alivyoeleza William Shakespeare.

Hawa ''Weird Sisters'' ni Wanga Watatu.

Naam Wazungu walikuwa washirikina wakiamini uchawi.

Mvua na ''melancholy,'' nishaondoka Magomeni Mapipa sasa niko Edinburgh, Scotland milimani kwenye Edinburgh Castle na hali ya kiza na mawingu ndiyo hii naiona hapa Mapipa.

Allah fundi.

Dakika moja ''split second'' nishafika Scotland naiangalia nchi na milima yake na nawaona wale wanga walimtabiria Macbeth ufalme.

Mara nisharudi Dar es Salaam kijana mdogo wa miaka 15 St. Joseph' Convent School mbele yangu kasimama Miss Menez mwalimu wangu wa Literature ananisomesha fasihi ya Kiingereza mkononi kashika Mcbeth.

Haya yote ''effortlessly.''

Bila shida wala kichwa si kizito kuwa kimeelemewa na taarifa zote nilizohifadhi kichwani.

Hakika neema za Allah hazihesabiki.
Nakwenda mbele narudi nyuma.

Bila tabu wala kutumia nguvu yoyote.
Hivi Hard Disc ya kichwa ni GB ngapi?

Vua tu linadondoka kimya kimya sauti ninayoisikia ni sauti ya matone yakigonga sakafu.

Nje ya dirisha la jikoni ukuta wa ua juu kakaa paka wa binti yangu.

Yeye anapenda paka lakini yu mbali na nyumbani angekuwepo angeniambia paka huyu wake ni kizazi cha ngapi.

Paka wake alipokuwapo mwenyewe huwa wakizaliwa anawapa majina.

Kwangu mimi wote nawaona sura moja.

Yeye anawajua kwa sura na majina na huwa anazungumzanao na wakimuudhi huwatishia kuwaadabisha kwa mikwaju.

Paka wanatii amri.

Wakiumwa anawatia kwenye kikapu anawapeleka hospitali kutibiwa tena kikapu kakibeba ndani ya mwendokasi au daladala.

Nimemwangalia paka anajificha mvua.

Paka kanikumbusha mwanangu mbali na nyumbani.

''Mbali na Nyumbani,'' ni kitabu cha mwandishi maarufu wa fasihi Adam Shafi.

Ashiki kitabu hiki.

''Ashiki Kitabu Hiki,'' hicho ni kitabu cha Shaban Robert.

Mvua hii inanishawishi niingie Maktaba nikitafute ''Mbali na Nyumbani,'' nipate kukitalii.

Huwezi kuchoka kumsoma Adam Shafi.

Kanihadithia Adam Shafi.

Anasema alikuwa Ulaya kwa binti yake anaandika kitabu.

Toka asubuhi mwanae ni kuleta kahawa kikombe baada ya kikombe.

Jioni mtoto kapata hamu ya kujua baba yake kaandika nini kutwa nzima.

Adam Shafi akamuonyesha.

''Ba, siku nzima hata ukurasa mmoja hujamaliza!

Chao!

melancholy
noun
a feeling of pensive sadness, typically with no obvious cause.
"an air of melancholy surrounded him"
 
Shikamoo Mzee Mohamed Said,nimeusoma huu Uzi mvua ikinyesha..Huwa sichoki kusoma chochote unachoandika,inaonekana Una akili nyingi Sana toka utotoni,ukabahatika na kubahatika kuona mengi na kufanya mengi katika tasnia ya uandishi,nazidi kumuomba Mwenyezi Mungu azidi kukubariki na kukupa Maisha marefu yenye fanaka.Iko siku nitakutembelea ishaallah🙏
 
Red...
Marahaba,
Ahsante karibu sana.

NImeangalia ID yako Red Label.
HMV walikuwa wanatengeneza santuri na wakaziweka katika category ya red na blue kutofautisha aina ya muziki.

Muziki kutoka Ulaya ilikuwa Red Label na ya Africa ikitolewa katika Blue Label.

ASD_2401.jpg

hmv_pop_182_78.jpg
 
It had to be. Kasomeshwa na wakatoliki St Joseph. 😆😆😆
Gagnija,
Dunia nzima shule za Kikatoliki zinaongoza kwa kusomesha elimu ya sekula.

Nilimesoma kitabu cha maisha ya Benazir Bhuto nimeshangaa kusoma kuwa kasoma St. Joseph's.

Elimu ya msingi nimesomeshwa na Waluteri, Moshi nilipoanza darasa la kwanza 1958.

Hapakuwa na shule tukisoma ndani ya kanisa angalia picha hapo chini.

Lakini kabla ya kwenda Lutheran Primary School nilianzishwa chekechea katika Muslim School.

276306905_1143203219760388_4213218925397671151_n.jpg

Lutheran Church Moshi 1989
277295468_1143204003093643_5580320659638863921_n.jpg

Lutheran Church Moshi 2020
 
Shikamoo Mzee Mohamed Said,nimeusoma huu Uzi mvua ikinyesha..Huwa sichoki kusoma chochote unachoandika,inaonekana Una akili nyingi Sana toka utotoni,ukabahatika na kubahatika kuona mengi na kufanya mengi katika tasnia ya uandishi,nazidi kumuomba Mwenyezi Mungu azidi kukubariki na kukupa Maisha marefu yenye fanaka.Iko siku nitakutembelea ishaallah🙏
Naunga mkono hoja.
 
Kwanini ukasome shule kikafiri kwa mtu kama wewe ambae kabla ulishaenda madrasa na ukafundishwa kuwa" hakika hawatakuwa radhi mayahudi na manaswara mpaka mufuate mila yao?
 
Red...
Marahaba,
Ahsante karibu sana.

NImeangalia ID yako Red Label.
HMV walikuwa wanatengeneza santuri na wakaziweka katika category ya red na blue kutofautisha aina ya muziki.

Muziki kutoka Ulaya ilikuwa Red Label na ya Africa ikitolewa katika Blue Label.

ASD_2401.jpg

hmv_pop_182_78.jpg
Aisee Safi Sana,sikuwahi kujua maana yakez,Ila me red label kumradhi inamaanisha kinywaji changu pendwa though Kwa kiwango kidogo.Shukrani Mzee wangu tuko pamoja...
 
Mna...
Pale kanisani kulikuwa na shule ya chekechea nilipelekwa kusoma.
Post #5 umeandika Lutheran primary school ulianza darasa la kwanza 1958, kabla ya hapo ulisoma chekechea Muslim school.

Kumbukumbu sahihi ni ipi? Ulisoma chekechea Lutheran school?!
 
Post #5 umeandika Lutheran primary school ulianza darasa la kwanza 1958, kabla ya hapo ulisoma chekechea Muslim school.

Kumbukumbu sahihi ni ipi? Ulisoma chekechea Lutheran school?!
Gag,
Kulikuwa na chekechea na darasa la kwanza hapo kanisani.
 
Gagnija,
Dunia nzima shule za Kikatoliki zinaongoza kwa kusomesha elimu ya sekula.

Nilimesoma kitabu cha maisha ya Benazir Bhuto nimeshangaa kusoma kuwa kasoma St. Joseph's.

Elimu ya msingi nimesomeshwa na Waluteri, Moshi nilipoanza darasa la kwanza 1958.

Hapakuwa na shule tukisoma ndani ya kanisa angalia picha hapo chini.

Lakini kabla ya kwenda Lutheran Primary School nilianzishwa chekechea katika Muslim School.

276306905_1143203219760388_4213218925397671151_n.jpg

Lutheran Church Moshi 1989
277295468_1143204003093643_5580320659638863921_n.jpg

Lutheran Church Moshi 2020
Kumbe 🤔🤔👍👍
 
Back
Top Bottom