Binti wa miaka 14 atoweka nyumbani.

Chimemena

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,376
452
Habari zenu wana JF.
Heri ya Xmass na maandalizi mema ya kuukaribisha mwka mpya.
Familia inaomba ushauri wenu.
Najitokeza mbele yenu kuomba msaada wenu wa mawazo, nina mdogo wangu wa kike ana miaka 14 amemaliza class 7 mwaka huu, tayari kashavunja ungo.
Huyu binti kawa mapepe sana baada ya kuonja asali ya duniani. Kuanzia jumamosi ya tarehe 22 awetoweka nyumbani na kukimbilia kusikojulikana lakini nimejaribu kuuliza marafiki zake wanasema kaenda kwa mchumba wake. Mpaka sasa hajarudi nyumbani licha ya kumtafuta kwa uwezo wetu na kuwauliza wanafamily wengineo wanasema hawajamwona.
Awali ya yote kabisa huyu binti mwezi wa 10 tulipata kusikia kuwa ni mjamzito wa miezi miwili na akafanikiwa kutoa hiyo mimba.
Tuko katika taharuki kubwa kutaka kujua huyu binti kaelekea wapi? nani anayemdanganya?
Wasichana wa kileo jamani sijui wapi wanaelekea na hii dunia.
Mwenyezi mungu awanusuru
 
Tupo radhi kukosolewa popote pale tulipoteleza katka malezi ya huyu binti, ni aibu kubwa kwa familia yetu.
 
Tupo radhi kukosolewa popote pale tulipoteleza katka malezi ya huyu binti, ni aibu kubwa kwa familia yetu.

Haitasaidia sana tukiwakosoa; ila mtafuteni huyo 'mchumba' wake muoongee naye kwa kutulia, kama kumuoza mumuoze lkn mkiwa na mpango wa kumpeleka walau VETA
 
Haitasaidia sana tukiwakosoa; ila mtafuteni huyo 'mchumba' wake muoongee naye kwa kutulia, kama kumuoza mumuoze lkn mkiwa na mpango wa kumpeleka walau VETA

Aozeshwe..!!?
Binti bado mdogo sana kuyakabili majukumu ya ndoa.
 
hajatoroshwa,
katoroka,

hao rafiki zako wawatajie alipo....

Na huyo mwanaume mbakaji afikishwe kwenye vyombo vya dola......

Too bad mtoto wa namna hiyo kubadikika kazi sana, mpaka yamkute...... Msichoke kumuongoza na kumuombea....
 
Aozeshwe..!!?
Binti bado mdogo sana kuyakabili majukumu ya ndoa.

Wewe unaona ni mdogo, lakini yeye tayari anajiona kaiva ndiomana kahama kabisa nyumbani.

Mnataka awazalie hapo nyumbani?

Mtafuteni huyo mchumba wake kupitia kwa hao marafiki kisha muozesheni tu!
 
Peleka taarifa Polisi, baada ya hapo we jitulize ndani tu...binti akienda kwa mchumba huwa anarudi
 
Huwa wanarudi tu after sometimes, kwa sasa muwabane rafiki zake kujua alipo.
Siwezi kusema mmemlea vibaya kwa sababu pia nina case kama hiyo, kiufupi tu ni kipindi kibaya sana kwa mabinti kwa sasa.
Atapumzika akipata ujauzito mwingine, manake atachoka kuzichomoa!
 
Aozeshwe..!!?
Binti bado mdogo sana kuyakabili majukumu ya ndoa.

Sheria imeruhusu mpaka miaka 15, nadhani walijua binti atahimili.
Na pia kashaanza hayo maisha kama mwana ndoa, maana kahamia, sasa asimudu vp?
 
Wewe unaona ni mdogo, lakini yeye tayari anajiona kaiva ndiomana kahama kabisa nyumbani.

Mnataka awazalie hapo nyumbani?

Mtafuteni huyo mchumba wake kupitia kwa hao marafiki kisha muozesheni tu!

ahsante kwa ushauri wako.
Hao marafiki zake ni mabinti wa hapa jirani, siku anaondoka aliwaaga kwamba anaenda kwa sweetie wake nao wakadhani kama utani, mpaka leo mtoto hajarudi.
 
ahsante kwa ushauri wako, taarifa tayari tumeshatoa police.

Kama umeshaenda police chukua picha yake ambayo si ya muda mrefu haraka sana uende nayo hadi ITV ili aonyeshwe leo kwenye Jiji Letu kwamba kapotea ili kama tumemwona huku mtaani tukutaarifu. Usisahau kutoa namba yako/zako za simu kwa watu wa ITV ili iwe rahisi sisi kukupigia kama tukimwona.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Subiri mwaka mpya upite atarudi tu hakikisheni anapimwa mimba
 
Back
Top Bottom