Binti wa miaka 11 ajifungua salama

Binti wa miaka 11 ajifungua salama

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,176
Reaction score
60,549
02_11_73bb3k.jpg

Nangakwa Lowasa (11) akiwa amempakata mtoto wake (amefunikwa na rubega) katika Hospitali ya Wilaya ya Siha, Machame mkoani Kilimanjaro hivi karibuni. (Picha na Arnold Swai).

WAKATI Serikali ikikuna kichwa kukabiliana na wimbi la mimba kwa wanafunzi, binti mwenye umri wa miaka 11 mkazi wa Ngarananyuki mkoani Kilimanjaro, Nangakwa Lowasa, amejifungua mtoto mwenzie salama nyumbani kwake kwa usaidizi wa wakunga wa jadi.

Binti huyo kutoka jamii ya Kimasai iliyoko wilayani Siha mkoani hapa, amewashangaza wengi baada ya kujifungua bila kupata tatizo lolote, na kwa sasa anaishi na mume wake aliyejulikana kwa jina moja la Narida, anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35.

Gazeti hili wiki hii lilizungumza na binti huyo katika wodi ya wazazi ya Hospitali ya Wilaya ya Hai iliyoko Machame alikolazwa baada ya kuugua malaria mara baada ya kujifungua ambapo licha ya kutokwenda shule kabisa katika maisha yake, pia hajui hata lugha ya Kiswahili.

Kutokana na mazingira aliyokulia, Nangakwa aliyekuwa akizungumza kwa msaada wa mfasiri, haoni tatizo lolote kwa yeye kujifungua mtoto na hata kuwa na mume.

Binti huyo alisema aliolewa mwaka jana na kwa sasa anaishi na mume wake Narida, na kwamba wakati wa kujifungua, ingawa ilikuwa nyumbani na kwa njia za kienyeji, hakupata tatizo lolote.

Pamoja na kwamba katika hali ya kawaida, alikuwa akihatarisha maisha yake kwa kujifungulia nyumbani, Nangakwa hakuwa na namna kwa kuwa kwa mujibu wa maelezo yake, hajawahi kwenda kliniki tangu alipopata ujauzito mpaka alipojifungua.

Binti huyo alisema akiwa na umri wa miaka mitano alikuwa tayari ameshalipiwa mahari na mume wake huyo na alipofikisha miaka kumi, wazazi wake walimshauri kuolewa, ambapo alisisitiza kwamba kwake ni jambo la kawaida.

Alisema hajawahi kwenda shule ndio maana hajui kuongea hata kidogo lugha ya Kiswahili na maisha yake na ya mumewe ni ya ufugaji.

Mama mkwe wake ambaye alikuwa akimuuguza hospitalini hapo, alikataa kuzungumza na gazeti hili na kwa jinsi ilivyokuwa, inaonekana alikuwa akijua kuwa ni kosa kisheria kwa kuwa alisema anahofia kuchukuliwa hatua na alifikia hatua ya kumkimbia mwandishi.

Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya 1971, inayopingwa na wana harakati, mtoto wa kike anaweza kuolewa akiwa na umri wa miaka 14, lakini baada ya wazazi kuafiki achukue hatua hiyo.

Hata hivyo, sheria hiyo inapingana na Sheria ya Makosa ya Kujamiiana ya 1998, ambayo imeeleza wazi kuwa mtoto yeyote chini ya miaka 18 akiingiliwa kimwili atakuwa amenajisiwa.

Gazeti hili lilizungumza na wagonjwa waliokuwa katika wodi hiyo ambapo wote walielezea kushangazwa na binti huyo kujifungua mtoto, ambapo walisema ni uonevu mkubwa usio stahili kwa jamii ya sasa.

Wagonjwa wenzake hao walisema binti huyo bado anahitaji malezi ya baba na mama, pamoja na haki yake ya msingi ya kwenda shule. Hata hivyo, waliomshauri aolewe akiwa na miaka kumi tu ni wazazi hao ambao walipaswa kumpa malezi bora.

Kutokana na hali hiyo, mmoja wa wagonjwa hao ambaye hakutaka kutaja jina lake, aliiomba Serikali kuwachukulia hatua wazazi wa mtoto huyo pamoja na mumewe.

Pia aliiomba Serikali itoe elimu ya athari za mimba za utotoni vijijini hususani kwa jamii ya Wamasai, ili waondokane na hali hiyo inayowanyima fursa watoto wa kike kukosa malezi ya baba na mama pamoja na elimu.
 
siku hizi ni kama kawaida, ila huyu amewahi sana, nilishangaa morogoro, Ludewa watoto wa miaka 12-15 wengi wana watoto wenzao na jamii imekubali tu! so sad!
 
02_11_73bb3k.jpg

Nangakwa Lowasa (11) akiwa amempakata mtoto wake (amefunikwa na rubega) katika Hospitali ya Wilaya ya Siha, Machame mkoani Kilimanjaro hivi karibuni. (Picha na Arnold Swai).
Eee bwana wee!! Tujuze vema,ni mtoto wa Lowassa yupi???? Ni yuleyule 2nayemjua ama ni majina yamefanana tu! Hebu tujuze
vema!
 
WAKATI Serikali ikikuna kichwa kukabiliana na wimbi la mimba kwa wanafunzi, binti mwenye umri wa miaka 11 mkazi wa Ngarananyuki mkoani Kilimanjaro, Nangakwa Lowasa, amejifungua mtoto mwenzie salama nyumbani kwake kwa usaidizi wa wakunga wa jadi.

Binti huyo kutoka jamii ya Kimasai iliyoko wilayani Siha mkoani hapa, amewashangaza wengi baada ya kujifungua bila kupata tatizo lolote, na kwa sasa anaishi na mume wake aliyejulikana kwa jina moja la Narida, anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35.

Gazeti hili wiki hii lilizungumza na binti huyo katika wodi ya wazazi ya Hospitali ya Wilaya ya Hai iliyoko Machame alikolazwa baada ya kuugua malaria mara baada ya kujifungua ambapo licha ya kutokwenda shule kabisa katika maisha yake, pia hajui hata lugha ya Kiswahili.

Kutokana na mazingira aliyokulia, Nangakwa aliyekuwa akizungumza kwa msaada wa mfasiri, haoni tatizo lolote kwa yeye kujifungua mtoto na hata kuwa na mume.

Binti huyo alisema aliolewa mwaka jana na kwa sasa anaishi na mume wake Narida, na kwamba wakati wa kujifungua, ingawa ilikuwa nyumbani na kwa njia za kienyeji, hakupata tatizo lolote.

Pamoja na kwamba katika hali ya kawaida, alikuwa akihatarisha maisha yake kwa kujifungulia nyumbani, Nangakwa hakuwa na namna kwa kuwa kwa mujibu wa maelezo yake, hajawahi kwenda kliniki tangu alipopata ujauzito mpaka alipojifungua.

Binti huyo alisema akiwa na umri wa miaka mitano alikuwa tayari ameshalipiwa mahari na mume wake huyo na alipofikisha miaka kumi, wazazi wake walimshauri kuolewa, ambapo alisisitiza kwamba kwake ni jambo la kawaida.

Alisema hajawahi kwenda shule ndio maana hajui kuongea hata kidogo lugha ya Kiswahili na maisha yake na ya mumewe ni ya ufugaji.

Mama mkwe wake ambaye alikuwa akimuuguza hospitalini hapo, alikataa kuzungumza na gazeti hili na kwa jinsi ilivyokuwa, inaonekana alikuwa akijua kuwa ni kosa kisheria kwa kuwa alisema anahofia kuchukuliwa hatua na alifikia hatua ya kumkimbia mwandishi.

Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya 1971, inayopingwa na wana harakati, mtoto wa kike anaweza kuolewa akiwa na umri wa miaka 14, lakini baada ya wazazi kuafiki achukue hatua hiyo.

Hata hivyo, sheria hiyo inapingana na Sheria ya Makosa ya Kujamiiana ya 1998, ambayo imeeleza wazi kuwa mtoto yeyote chini ya miaka 18 akiingiliwa kimwili atakuwa amenajisiwa.

Gazeti hili lilizungumza na wagonjwa waliokuwa katika wodi hiyo ambapo wote walielezea kushangazwa na binti huyo kujifungua mtoto, ambapo walisema ni uonevu mkubwa usio stahili kwa jamii ya sasa.

Wagonjwa wenzake hao walisema binti huyo bado anahitaji malezi ya baba na mama, pamoja na haki yake ya msingi ya kwenda shule. Hata hivyo, waliomshauri aolewe akiwa na miaka kumi tu ni wazazi hao ambao walipaswa kumpa malezi bora.

Kutokana na hali hiyo, mmoja wa wagonjwa hao ambaye hakutaka kutaja jina lake, aliiomba Serikali kuwachukulia hatua wazazi wa mtoto huyo pamoja na mumewe.

Pia aliiomba Serikali itoe elimu ya athari za mimba za utotoni vijijini hususani kwa jamii ya Wamasai, ili waondokane na hali hiyo inayowanyima fursa watoto wa kike kukosa malezi ya baba na mama pamoja na elimu
 
Mmmhh no comment! How can u make love with a kid
 
WAKATI Serikali ikikuna kichwa kukabiliana na wimbi la mimba kwa wanafunzi, binti mwenye umri wa miaka 11 mkazi wa Ngarananyuki mkoani Kilimanjaro, Nangakwa Lowasa, amejifungua mtoto mwenzie salama nyumbani kwake kwa usaidizi wa wakunga wa jadi.

Binti huyo kutoka jamii ya Kimasai iliyoko wilayani Siha mkoani hapa, amewashangaza wengi baada ya kujifungua bila kupata tatizo lolote, na kwa sasa anaishi na mume wake aliyejulikana kwa jina moja la Narida, anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35.

Yaani inaleta hasira jamani!!!!!.....Mimi nikafikri labda kepewa mimba na mwanafunzi mwenzake, kumbe kaolewa!!!....:A S 13::A S 13::A S 13::A S 13:This is too much jamani!!!
 
Kutaja sheria tu haitoshi. Hawa wananchi ambao hata kiswahili hawajui kuwatajia vifungu vya sheria haisaidii. Wananchi hawa hawajawezeshwa kwa hiyo hawajui kama kuna maisha mbadala yanayohusisha shule na vingenevyo. Kwao traditional life ndio mahali pake.
Hali kama hiyo si kiashiria tu cha uvunjifu wa sheria bali umasikini na ujinga uliokithiri. Kuna tatizo kubwa saana kwenye nchi yetu si kama wengi wetu ambavyo hutafsiri kirahisi au kutoa majibu rahisi kwenye maswali magumu. Wajibu hapo si kuwa na magereza na mahakimu wengi wa kufunga watuhumiwa bali kuwawezesha wananchi kujikwamua katika maisha ya sasa na kuwajengea misingi bora ya baadae kwa kuwafahamisha haki zao za msingi kama raia.
 
Asante kwa taarifa..pia ungetujulisha kama ni Lowassa wa Richmond au la..
 
Nadhani Mwenyezi Mungu aliwahisha sana ile gharika ya Sodoma na Gomora...wanaume wa aina hii ni wakutiwa kiberiti! Pia kwa mleta hoja Hospitali ya wilaya ya Siha ipo siha sio machame ambayo ipo Hai!
 
mimi nilidhania Fisadi papa Richimonduri Basi mada zako ni za kidaku
 
Kutaja sheria tu haitoshi. Hawa wananchi ambao hata kiswahili hawajui kuwatajia vifungu vya sheria haisaidii. Wananchi hawa hawajawezeshwa kwa hiyo hawajui kama kuna maisha mbadala yanayohusisha shule na vingenevyo. Kwao traditional life ndio mahali pake.
Hali kama hiyo si kiashiria tu cha uvunjifu wa sheria bali umasikini na ujinga uliokithiri. Kuna tatizo kubwa saana kwenye nchi yetu si kama wengi wetu ambavyo hutafsiri kirahisi au kutoa majibu rahisi kwenye maswali magumu. Wajibu hapo si kuwa na magereza na mahakimu wengi wa kufunga watuhumiwa bali kuwawezesha wananchi kujikwamua katika maisha ya sasa na kuwajengea misingi bora ya baadae kwa kuwafahamisha haki zao za msingi kama raia.
Inasikitisha. Hapa ndipo serikali yetu imefeli na hakuna mwelekeo wa kujinasua. Ikiwa jukumu la serikali ni kuongoza (sio kutawala), yetu imeshindwa. Ukosefu wa huduma za kijamii na uwepo wa huduma duni, nafikiri ndiko kunakowafanya wazazi kuchukua maamuzi ya kiajabu. Mzazi masikini ampeleke mtoto wake shule kufanya nini? Amalize darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika. Hata abahatike kufika kidato cha nne, aongeze idadi tu katika orodha ya wanaofeli? Akisha kufeli ndo arudi nyumbani kuchunga ng'ombe?
Hapo penye rangi ndipo serikali isipopataka. Raia wafamu haki zako za msingi? Wakizijuwa si watazidai? Serikali haitaki hilo. Bora wabkie mbumbu iliwao waendelee kutawala.
 
Yaani inaleta hasira jamani!!!!!.....Mimi nikafikri labda kepewa mimba na mwanafunzi mwenzake, kumbe kaolewa!!!....:A S 13::A S 13::A S 13::A S 13:This is too much jamani!!!

Inasikitisha sana kusema kweli. Nimemuangalia huyo binti kwenye picha ambayo amempakata "mwanae" nimemuonea huruma kweli kweli. Imagine libaba la miaka la miaka kati ya 30 na 35 linamshupalia mtoto wa miaka 11 kumnanihii! Wote walioruhusu hii harusi pamoja na mume wanastahili kuwekwa lupango.
 
Hawa wananchi ambao hata kiswahili hawajui kuwatajia vifungu vya sheria haisaidii. Wananchi hawa hawajawezeshwa kwa hiyo hawajui kama kuna maisha mbadala yanayohusisha shule na vingenevyo. Kwao traditional life ndio mahali pake.

Back
Top Bottom