Binti niliemtelekeza na bili bar, kumbe kawaeleza mabinti wote kazini, sasa ni vibuti tu

Kuna binti ambae tunafanya kazi pamoja na ambae nilimtoa outing siku moja, kinyume na matarajio akaniletea kundi la wasichana wenzie kunifilisi nami nika apply umafia wa hali juu kwa kuwakimbia na kuwatelekeza na bili kubwa waliyotumia wenyewe, mi nilikunywa bia 3 tu

Sasa kumbe tangu siku hiyo ameendesha kampeni kali ya kunichafua hapa kazini kwa mabinti wenzie kiasi kwamba hata nikiomba kampani ya kawaida tu kwenda lunch mabinti hunitazama chini hadi juu na mwisho kunisonya msonyo mkali sana na kuondoka zao huku wakitamka maneno kwa methali na mafunzo, wengine wakiniambia "" unalo babu"" sasa sijajua maana yake hadi sasa

Yote tisa, kumi nikaona nijaribu bahati yangu kwa binti mwingine ambae ni mtaratibu sana, yupo kivyake vyake na anaishi ki british sana hapa kazini, baada ya mazungumzo ya siku kadhaa, nikaona nimtafutie zawadi ndogo kusindikizia ujumbe wangu wa mahaba, weekend hii nikaenda dukani pale sinza duka moja linauza chupi tu za akina dada nikawaeleza nia yangu wakanifungia vizuri kwenye package maalum


Leo asubuhi tulipo sign in tu nikaangalia kushoto na kulia watu hawanitazami nikaenda haraka kwenye meza yake na kumpa kishkaji na kumwambia ni zawadi yake ni zawadi yake
Akaipokea nikarudi kwenye idara yangu maana tupo ghorofa tofauti ya 3 na 4

Nashangaa baada kama ya lisaaa moja nashtuka kumuona yule binti akinifuata huku amefura na kunirushia ile chupi usoni ikiwa imeshafunguliwa kwenye package yake na kuanza kunipaka kwamba namuonaje hadi nampelekea chupi,? Kwamba nisimfananishe yeye na flani (yule niliemkimbia bar)
Kumbe yule binti kaeleza kampuni nzima?

Nimepata aibu ya milele leo

Hivi wakuu nimekosea wapi?
Kumpelekea mwanamke zawadi kuna ubaya?
Mbona tulikua tunaenda vizuri tu tangu juzi? Au ni sumu amepewa na yule binti mwingine?
acha ufala wewe mademu wako hapo kazini tu.jogoo la shamba
 
kuna binti ambae tunafanya kazi pamoja na ambae nilimtoa outing siku moja, kinyume na matarajio akaniletea kundi la wasichana wenzie kunifilisi nami nika apply umafia wa hali juu kwa kuwakimbia na kuwatelekeza na bili kubwa waliyotumia wenyewe, mi nilikunywa bia 3 tu

sasa kumbe tangu siku hiyo ameendesha kampeni kali ya kunichafua hapa kazini kwa mabinti wenzie kiasi kwamba hata nikiomba kampani ya kawaida tu kwenda lunch mabinti hunitazama chini hadi juu na mwisho kunisonya msonyo mkali sana na kuondoka zao huku wakitamka maneno kwa methali na mafunzo, wengine wakiniambia "" unalo babu"" sasa sijajua maana yake hadi sasa

yote tisa, kumi nikaona nijaribu bahati yangu kwa binti mwingine ambae ni mtaratibu sana, yupo kivyake vyake na anaishi ki british sana hapa kazini, baada ya mazungumzo ya siku kadhaa, nikaona nimtafutie zawadi ndogo kusindikizia ujumbe wangu wa mahaba, weekend hii nikaenda dukani pale sinza duka moja linauza chupi tu za akina dada nikawaeleza nia yangu wakanifungia vizuri kwenye package maalum


leo asubuhi tulipo sign in tu nikaangalia kushoto na kulia watu hawanitazami nikaenda haraka kwenye meza yake na kumpa kishkaji na kumwambia ni zawadi yake ni zawadi yake
akaipokea nikarudi kwenye idara yangu maana tupo ghorofa tofauti ya 3 na 4

nashangaa baada kama ya lisaaa moja nashtuka kumuona yule binti akinifuata huku amefura na kunirushia ile chupi usoni ikiwa imeshafunguliwa kwenye package yake na kuanza kunipaka kwamba namuonaje hadi nampelekea chupi,? Kwamba nisimfananishe yeye na flani (yule niliemkimbia bar)
kumbe yule binti kaeleza kampuni nzima?

Nimepata aibu ya milele leo

hivi wakuu nimekosea wapi?
Kumpelekea mwanamke zawadi kuna ubaya?
Mbona tulikua tunaenda vizuri tu tangu juzi? Au ni sumu amepewa na yule binti mwingine?
usife moyo dogo ...iko siku utatoka kwenye uvulana.... Na kuwa mwanaume.
 
Kwani kinachokusumbua nini? Acha kujihangaisha nao kwani unavyoonekana kusumbuka ndio wanavyotaka. Wao walikosea na ulipowashtukia wanataka kukuumiza kwa hicho kisasi chao cha kitoto.
Cha kufanya, acha kutongoza wanawake hapo ofisini, look happy and normal, fanya matumizi ya kawaida kama siku zote bila kuwa influenced na tabia wanazokuonyesha, Usiwasalimie wala kujisemesha kwao labda kwa mambo ya kiofisi, watajiona wapuuzi, huwezi kulazimisha wenzio wapewe vinywaji bila prior notice wakati uliitwa peke yako kwenye mtoko.
Kuwa normal tu, tafuta mtoto mzuri anaejielewa nje ya ofisi yenu, na awe mkali sana ndio umalizie hasira zako za kimatumizi, kupenda na hata ndoa.
 
Mkuu usituaibishe wanaume. Simamia msimamo wako sawa sawa mkuu, ukiwa na msimamo hutoyumbishwa kaka. Tulia kwanza kidogo kidogo tafuta mrembo mmoja matata sana nje ya office, mgaramie kwa pamba kali sana kisha jumatatu moja mualike hapo office afike mida ya saa za asubuhi na mfuko wa matunda. Heshima itarudi
 
Ila we kaka jamani chupi wakati ndo huo urafiki wenyewe ndo unaanza...... yani of all things chupi mmmh smh
 
Haaa haa eti " unalo Babu" maana ake ni kuwa "unalo na limekuganda ka luba"
 
Umemiss point ya maana. Nia yake (binti wa pichu) ni kuonyesha ofisini kuwa wako wanaokimbiwa lakini yeye kaletewa zawadi.
Btw hauoni mabinti wengine nje ya ofisi?
 
d4i6z.jpg

am here

hii ni stor ya kupika
 
Mkuu usituaibishe wanaume. Simamia msimamo wako sawa sawa mkuu, ukiwa na msimamo hutoyumbishwa kaka. Tulia kwanza kidogo kidogo tafuta mrembo mmoja matata sana nje ya office, mgaramie kwa pamba kali sana kisha jumatatu moja mualike hapo office afike mida ya saa za asubuhi na mfuko wa matunda. Heshima itarudi

mkuu kama unataka kuwapiga bao chukua huu ushauri.
dawa ya wanawake ni kuwapotezea na kutafuta mdada mkali zaidi yao hata kwa kumlipa ili aje awapige bao.
wenyewe wataanza kujileta.
tena ikiwezekana muombe tu hata mdada yeyote mkali mwenye gari anakudrop asubuhi na jioni anakufuata.
mnapoachana na mahug kibao.
mchana anakufuata for lunch.
nakuapia hao wadada wataanza wenyewe kukusalimia.
ila jiandae kujaza mafuta ya gari kila siku.

lakini pia unaweza kuangukiwa na zali la mentali huyu mdada akakuzimikia
 
umeona Eeeeh wasichana walivo na akili ndogo.Hv wenzio wanavotafuta wake humu ndani huwaoni?Hawapendi ujinga huo,wanaingia jf kimyakimya anatafuta binti anaendelea na heshima zake!Tulia bhana,hv mabint wako hapo tu kazini kwako,kwingine hakuna?
 
mkuu kama unataka kuwapiga bao chukua huu ushauri.
dawa ya wanawake ni kuwapotezea na kutafuta mdada mkali zaidi yao hata kwa kumlipa ili aje awapige bao.
wenyewe wataanza kujileta.
tena ikiwezekana muombe tu hata mdada yeyote mkali mwenye gari anakudrop asubuhi na jioni anakufuata.
mnapoachana na mahug kibao.
mchana anakufuata for lunch.
nakuapia hao wadada wataanza wenyewe kukusalimia.
ila jiandae kujaza mafuta ya gari kila siku.

lakini pia unaweza kuangukiwa na zali la mentali huyu mdada akakuzimikia

Nahisi alibeba mdada asiejielewa, sasa Dada anaona kuwa ameaibishwa sana kwa sababu efforts zote za kumtangaza mtu ofisi nzima ni dalili ya kuumia sana na Kujiona hana namna nyingine ya kujiredeem kwa kushindwa kumchuna jamaa na kuharibu tukio zima ambalo alidhani lingekuwa gumzo kwa wadada wenzie na hivyo anajitahidi kujisafisha kwa kutumia mbinu ya kumchafua jamaa.
Mwanamke mwenye confidence angemfuata jamaa aliemkimbia na kumhoji kwanini alikimbia na kumsikiliza anavyojitetea, baada ya kuuchambua utetezi wake angempa pole au kumpa makavu laivu bila chenga na kumtema,.kudelete namba yake na hata kumchunia jamaa . Sasa kwa vile huyo Dada hajielewi na alikuwa akitafuta promo, aliona atafute ubingwa kwa wenzie wamuone mjanja kwa kulipiza jinsi jamaa alivyo kimbia kwa vile anaona company yake inamuona yeye wa ovyo na hivyo namna pekee anayoiona itamsafisha ni kumchafua jamaa kwa kumpaint kwa rangi zote za ovyo.
Jamani chukueni humuhumi JF, mbona kuna madada wanaojielewa sana? Au mpaka tuanze kuwataja majina?
 
Nakuona kama mvivu wa kutega karata zako unapocheza karata jua unaecheza nae pia anaakili na yawezakuwa ni bora kuliko yako.
Huwezi kimbilia kununua pichu eti kwa vile mnaongea vizuri zawadi ziko nyingi na asingekataa ni kwa vile umetaka kumpa ujumbe wa unachotaka kwa kupitia chupi.
Kuwa makini na unae ongea nae usiwaze kirahisi.
Wale ulio waacha bar nakusifu sana hapo unatakiwa utembee kifua mbele imeonyesha wewe sio mburura badala ya kuwa mnyonge na kuwaachia point zote
 
Back
Top Bottom