Binti mfalme achaguliwa kuwa balozi

Binti mfalme achaguliwa kuwa balozi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Bintimfalme Rima mwana wa Bandar al-Saud 2018
Bintimfalme Rima anafuata nyayo za babake wa kambo ambaye alishikilia wadhfa huo hadi mwaka 2005
Saudi Arabia imetangaza kwamba binti mfalme Rima bint Bandar al-Saud atakuwa balozi wake nchini Marekani -akiwa mwanamke wa kwanza kuwa balozi wa ufalme huo.

Uteuzi wake ulifanywa hadharani kwa amri ya ufalme huo siku ya Jumamosi. Bintimfalme Rima aliishi Washington DC nchini Marekani katika kipindi kirefu cha utoto wake.

Anachukua wadhfa huo wakati mgumu , huku Saudia ikijaribu kukabiliana na hisia za jamii ya kimataifa kuhusu mauji ya mwanahabari Jamal Khashoggi.

Baada ya kutoa taarifa zenye utata , ufalme huo baadaye ulikiri kwamba Khasshoghi ambaye alikuwa mfanyikazi wa ufalme huo, aliuawa baada ya kuingia ubalozi wa taifa hilo uliopo Instanbul mwaka uliopita.

Kabla ya kifo chake mwandishi huyo alikuwa akiliandikia gazeti la The Washington Post ambapo mara kwa mara alikuwa akiikosoa serikali ya Saudia.

Saudia imekana kwamba mwanamfalme Mohammed Bin Salman alihusika katika kifo chake madai ambayo idara ya ujasusi nchini Marekani inatiliashaka.

Wabunge nchini Marekani wamejaribu kuishinikiza Ikulu ya Whitehouse kuchunguza kisa hicho.

Hivi majuzi wanachama wa bunge la Congress walichunguza uhusiano kati ya Saudia na Marekani katika maeneo mengine, ikiwemo kuhusu teknolojia ya Kinyuklia pamoja na vita nchini Yemen.

Afuata nyayo za babake

Binti mfalme Rima atachukua jukumu lote la nduguye mdogo mwanamfalme , mwanamfalme Khalid bin Salman, ambaye ameteuliwa kuwa naibu waziri wa ulinzi nchini humo

Rais Trump ameshutumiwa kuhusiana na uhusiano wake wa karibu na mwanamfalme huyo wa Saudia anayehusishwa na kifo cha Khasshogi
Anafuata nyayo za babake Bandar bin Sultan al-Saud ambaye alishikilia wadhfa huo wa ubalozi wa Marekani hadi 2005.

Kwa sababu ya jukumu lake , alitumia kipindi kirefu cha utoto wake nchini Marekani.

Anashkilia shahada ya sanaa ya masomo ya kumbukumbu kutoka chuo kikuu cha George Washington University.

Tangu kurudi kwake mjini Riyadh 2005, binti mfalme Rima amefanya kazi katika nyanja za kibinafsi na zile za umma.

Ameshikilia nyadhfa tofauti za kibiashara , ikiwemo ile ya afisa mtendaji mkuu katika kampuni ya Harvey Nichols Riyadh.

Bintimfalme huyo anaonekana kuwa mpiganiaji mkuu wa haki za kibinaadamu za wanawake katika taifa ambalo linakosolewa kwa rekodi yake ya usawa wa kijinsia.

Hivi majuzi alikuwa akifanya kazi katika halmashauri ya michezo nchini Saudia akiwa na lengo la kuimarisha idadi ya wanawake wanaoshiriki katika michezo.

Pia anajulikana kwa kazi yake nzuri katika kampeni dhidi ya saratani ya matiti.

BBC
 
... walibana sana lakini taratibu naona wanaachia; oooh! kwa mujibu wa dini yetu mwanamke lazima achungwe na mumewe au ndugu wa damu popote aendapo; oooh! mwanamke haruhusiwi kuchangamana miongoni mwa wanaume; oooh! mwanamke anatakiwa kuwa nyumbani tu akihudumia familia! Ujinga mtupu!

... mdogo mdogo naona mabadiliko yamehamia kule shinani kwenyewe!
 
Kuna tofauti sana kati ya dini ya Uislam na nchi ya Saudi arabia narudia tena "dini ya Uislam na nchi ya Saudi arabia"
 
Muda wote unawaza malumbambano ya kidini tu mkuu,fanya ubadirike.
 
Kuna tofauti sana kati ya dini ya Uislam na nchi ya Saudi arabia narudia tena "dini ya Uislam na nchi ya Saudi arabia"
... unajua oficia title ya Mfalme wa Saudia? Ni hii: The Custodian of the Two Holy Mosques. Unaposema hakuna tofauti kati ya Saudia na uislamu nashindwa kukuelewa Mkuu.

Labda niiweke vizuri; katika zile nguzo tano za Uislamu, ile ya swala tano kila ukiitimiza unaelekeza kichwa kibla ilipo hiyo misikiti mitukufu ambayo Mfalme wa Saudia ni Custodian wake. Ile nguzo ya hija, kila ukiitimiza al-Kaaba inakuhusu na ndipo ulipo ule Msikiti Mkuu ambao Mfalme wa Saudia ni Custodian wake! Halafu uniambie hakuna uhusiano? You must be joking!
 
The Custodian of the Two Holy Mosques ni kwa mujibu wa sheria zao za Utawala wa kifalme, yeye mfalme kama kiongozi wa nchi, siyo kwa mujibu wa maandiko matakatifu ya Quran na Sunna. Soma ujue mambo kisha eneza ujuzi wako, taifa la kiislam huwa linaongozwa na kiongozi mkuu aitwaye "Khalifa" na taifa katika hali hiyo huitwa "Khilafa", kwa lugha nyepesi kama kweli unataka kujua ukweli na kuwa huru, hivi sasa kuna mataifa yenye waislamu duniani lakini hakuna taifa la kiislamu, With Saudi arabia included.
 
Mfalme hawezi kuwa kiongozi wa waislam ndugu yangu, Wakati Mtume Muhammad(SAW) anapewa utume ibada zenye kumfuata baba yetu wa imani (Ibrahim) zilikuwa zikifanywa kuelekea Baitul Maqdis Palestina, baadaye Qibla kikageuzwa na kuwa Alqaaba, unaweza kuona uhamaji wa eneo na utume katika nyakati tofauti, kama una swali uliza ndugu yangu
 
Pia the Third Holliest Mosque ni Baytul Maqdis, hivi sasa iko chini Ya Israel na Custodian wake ni Israel PM, hii haiifanyi Israel taifa la kiislam
 
... unajua oficia title ya Mfalme wa Saudia? Ni hii: The Custodian of the Two Holy Mosques. Unaposema hakuna tofauti kati ya Saudia na uislamu nashindwa kukuelewa Mkuu.

Labda niiweke vizuri; katika zile nguzo tano za Uislamu, ile ya swala tano kila ukiitimiza unaelekeza kichwa kibla ilipo hiyo misikiti mitukufu ambayo Mfalme wa Saudia ni Custodian wake. Ile nguzo ya hija, kila ukiitimiza al-Kaaba inakuhusu na ndipo ulipo ule Msikiti Mkuu ambao Mfalme wa Saudia ni Custodian wake! Halafu uniambie hakuna uhusiano? You must be joking!
Dini yoyote/jambo lolote ukitumia akili yako kulichanganua lina mapungufu yake.

Ukishajua hivi hata hauna haja ya kukaza na kushupaza kichwa. Unapenda saana kuukosoa uislamu ilihali dini zote zinamapungufu kwa fikra za kibinaadamu.
 
Imfikie: Hajjat FaizaFoxy
 
Kwa sababu haikushuka Uswahilini
Waarabu oyeee.

ﻭَﻛَﺬَﻟِﻚَ ﺃَﻭْﺣَﻴْﻨَﺎ ﺇِﻟَﻴْﻚَ ﻗُﺮْﺁﻧًﺎ ﻋَﺮَﺑِﻴًّﺎ ﻟِﺘُﻨْﺬِﺭَ ﺃُﻡَّ ﺍﻟْﻘُﺮَﻯ ﻭَﻣَﻦْ ﺣَﻮْﻟَﻬَﺎ ﻭَﺗُﻨْﺬِﺭَ ﻳَﻮْﻡَ ﺍﻟْﺠَﻤْﻊِ ﻻ ﺭَﻳْﺐَ ﻓِﻴﻪِ ﻓَﺮِﻳﻖٌ ﻓِﻲ ﺍﻟْﺠَﻨَّﺔِ ﻭَﻓَﺮِﻳﻖٌ ﻓِﻲ ﺍﻟﺴَّﻌِﻴﺮِ
 
Hahahaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dini yoyote/jambo lolote ukitumia akili yako kulichanganua lina mapungufu yake.

Ukishajua hivi hata hauna haja ya kukaza na kushupaza kichwa. Unapenda saana kuukosoa uislamu ilihali dini zote zinamapungufu kwa fikra za kibinaadamu.
Ndiyo hapo mkuu wakati anawasema hao waarabu huko kwake nako watu wanaachana tu siku hizi hakuna cha mwili mmoja wala nini.
 
... unajua oficia title ya Mfalme wa Saudia? Ni hii: The Custodian of the Two Holy Mosques. Unaposema hakuna tofauti kati ya Saudia na uislamu nashindwa kukuelewa Mkuu.

Labda niiweke vizuri; katika zile nguzo tano za Uislamu, ile ya swala tano kila ukiitimiza unaelekeza kichwa kibla ilipo hiyo misikiti mitukufu ambayo Mfalme wa Saudia ni Custodian wake. Ile nguzo ya hija, kila ukiitimiza al-Kaaba inakuhusu na ndipo ulipo ule Msikiti Mkuu ambao Mfalme wa Saudia ni Custodian wake! Halafu uniambie hakuna uhusiano? You must be joking!
Maana ya "custodian" ni nini?
 
Kuna tofauti sana kati ya dini ya Uislam na nchi ya Saudi arabia narudia tena "dini ya Uislam na nchi ya Saudi arabia"
papa alipoenda UAE si mlisema wale sio waislamu, waislamu wapo saudi arabia tu? leo unasema kuna tofauti kubwa ya uislamu na saudia ipi?
 
.... Kiongozi, hakuna kitu kibaya kama unafiki! Mara hii wameshasahau!
 
Back
Top Bottom