Binti aliyepata hasara ya maisha.

King'asti huo ni mfano kama mifano alokuwa anaitumia Yesu kipindi kile. km we ni mkristo naamini ushawah kusikia ule mfano wa Yesu kuwa ni rahisi kwa ngamia kupenya katka tundu la sindano. hapo hajamaanisha kwel ngamia anaweza kupenya kwny tundu la sindano. na mifano hutusaidia sana kuelewa mengi ambayo ni vigumu kuelewa.
 
Last edited by a moderator:
Stori za kusadikika hizo, ama ndo utatumia ibadani jumapili? Mchungaji aruhusu mtu kufunga ndoa kutoka kwa waumini bila kuandikisha, kutangaza siku 21 kwa mujibu wa sheria na kufanya mafundisho ya ndoa?

Haya ni mafundisho tu na siyo ukweli. Hakuna mchungaji atakayetoa ruksa hiyo ya ghafla kufungisha ndoa.

Hapo nimemuelewa ni kwamba tusikubali kudanganyika, na pia usimuamini hata rafiki yake kipenzi.



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Hii ni habari ya kweli kabisa, kama wewe huamini kwamba ni ya kweli, endelea kutoamini.
Eti eeh? Nikisali Kanisa lako sadaka naenda kunywea supu!


Du! yaani King'asti mtata aisee, mwenzio atakuwa ametumia kama mfano tu huo jama, lengo ilikuwa kumwaga neno kwa chini pale ........
Ntake radhi. Mi Nataka mifano iliyoenda shule.

charminglady, tofautisha mifano na parables. Afu anasisitiza ni ukweli. Last week nilikutana na mmama akanipa stori kuhusu my old prof. Ati alikataliwa na mume kanisani, padri Akaita anaetaka kumuoa ndo hadi Leo mumewe. Najua ni wivu tu, the lady is super intelligent and has done great things for this country. Niliishia tu kuwa polite na kusema she is a great and strong woman!
 
Last edited by a moderator:
Haya ni mafundisho tu na siyo ukweli. Hakuna mchungaji atakayetoa ruksa hiyo ya ghafla kufungisha ndoa.

Hapo nimemuelewa ni kwamba tusikubali kudanganyika, na pia usimuamini hata rafiki yake kipenzi.



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!

Hivi mnasomaga japo kwa kubrowse? Hamumtendei Haki huyu mtumishi

Hii ni habari ya kweli kabisa, kama wewe huamini kwamba ni ya kweli, endelea kutoamini.
 
oh my God! ROHO MTAKATIFU KAZINI

Nimekaa - nasoma Biblia hapa mezani - na asubuhi hii - natayarisha somo - na MSTARI HUU HUU - ISAYA 9: 15-16 -ndio nimeandika - ingawaje sikuwa na mfano hai - NASHUKURU KWA MFANO AU KISA ULICHOTOA .............NIMEKAMILISHA UJUMBE WANGU.

Yes - Holy Spirit - the Great Teacher at work

Stay blessed:flypig:
 
NAOMBA KUULIZA KUHUSIANA NA KIFUNGU HIKI:

''Yeremia17:5-6, BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kinga yake na moyoni mwake amemwacha BWANA, Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema, bali atakaa jangwani palipo ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu''


1.Tafsiri ya neno BWANA katika bible ni ipi ni Bwana Mungu ama Bwana Yesu?

2. Je? Yesu ni Mwanaadamu ama si Mwanaadamu?

3. Kuna watu ama kuna sehemu nimeona pameandikwa '' Gari hili linalindwa na damu ya Yesu'' hapa ikoje? kutokana na maandishi ya hapo juu?


Naomba kuelimishwa maana kuuliza si ujinga waungwana
 


mimi na nyumba yangu tutamtumikia bwana
 


Kaa kitako sasa na kwa utulivu ili uweze kupata japo kwa ufupi kuhusiana na maswali uliyouliza.
Yesu ni Mungu, na ushahidi wa hili ni kama ifuatavyo.
-> Katika Yohana 20:28 tunasoma Tomaso akajibu, Bwana wangu na Mungu wangu. Na baada ya kuita hivyo, hakuna rekodi yoyote inayoonyeesha kuwa Yesu alimkataza kumuita Mungu, kama Yesu asingekuwa Mungu, ni lazima angelimzuia Tomaso kumuita Mungu kama ambavyo malaika alimkataza Yohana kumpigia magoti, rejea Ufunuo 19:10.
-> Katika kitabu cha Yohana 14:4-11 tunasoma haya yafuatayo. Nami niendako mwaijua njia. Tomaso akamwambia, Bwana sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?. Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba, tangu sasa mmemjua tena mmemwona. Filipo akamwambia, Bwana utuonyeshe Baba yatutosha. Yesu akamwambia, mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, utuonyeshe Baba? Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya. Mnisadiki ya kuwa, mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.
Ushahidi upo mwingi sana lakini acha kwa sasa niishie hapo. Lakini nitaandaa maada juu ya jambo hilo ili waliodanganywa wasidanganywe tena.
 
anaonekana tu.labda iwe hii fani imevamiwa na watu wengine.

Ubarikiwe sana, lakini hayo maneno yako ambayo sikutarani yalopokwe na wewe sijayashangaa sana, maana ni sharti viumbe kama wewe wawepo duniani ili necha ibalansi. Ubarikiwe sana tena sana.
 
Mi nimependa sana huo ujumbe hata kama hadithi ni ya kufikirika lakini nimepata ujumbe mkubwa sana.. Asante ndugu.
 
Ubarikiwe sana, lakini hayo maneno yako ambayo sikutarani yalopokwe na wewe sijayashangaa sana, maana ni sharti viumbe kama wewe wawepo duniani ili necha ibalansi. Ubarikiwe sana tena sana.

baraka daima zitanishukia ila hizi catoon style peleka kwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…