Binti akimtambulisha mchumba wake kwa baba yake

Binti akimtambulisha mchumba wake kwa baba yake

Michael Amon

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2008
Posts
8,769
Reaction score
3,644
Binti: Baba nimepata mpenzi lakini yuko mbali sana na hapa Tanzania. Yuko Uingereza, London. Kuna website moja ya watu wanaotafuta wapenzi tulikutana humo, tukawa marafiki kwenye Facebook, tumechat kwenye Whatsapp sana, juzi kwenye Skype amepropose kunioa na sasa uhusiano wetu una miezi minne. Baba nahitaji baraka zako ili uhusiano uendelee vizuri tuoane.

Baba: Dingi akaweka gazeti chini, akakuna kipara kidogo, akavua miwani, halafu akamjibu mwanae:

Vizuri sana mwanangu. Hongera kwa kupata. Sasa fanyeni mpango muoane kabisa kupitia mtandao wa Twitter, watoto mnunue kwenye mtandao wa e-Bay na wawe wanawatembelea kupitia e-mails zenu na siku ukimchoka huyu mumeo basi umuuze kwenye mtandao wa Amazon! Kizazi cha hovyo kabisa! Mnadhani kila kitu ni mtandao! Non sense!
 
Ahaa utapata mwingine kupitia badoo

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom