Binti akatwa masikio yote na Baba Mkwe!

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
740
Haya ndiyo mapenzi ya dhati kwa mujibu wa wenzetu wa Mkoa wa Mara?
Masikiomgecho.jpg


Binti akatwa masikio yote katika kituko cha ndoa ya kulazimishwa
Na Frederick Katulanda, Tarime

MSICHANA Robhi Thomas (15), amekatwa masikio yote na kujeruhiwa mabegani na vidole vya mkono wa kulia na baba mkwe.

Binti huyo ambaye anadai kuwa aliolewa kwa lazima baada ya baba yake kupokea mahali ya Sh350,000 alipata mkasa huo kufutia ugomvi uliotokea kati ya wazazi na baba mkwe aliyetambulika� kwa jina la Mwita Thomas Mrimi.

Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Rusuti, Tarafa ya Tarime mjini Kata ya Inchage Aprili 18, mwaka huu usiku, wakati Robhi akiwa nyumbani kwa mume wake Thomas Mwita (18).

Kufuatia ugomvi wa wazazi wa Robhi na mkwewe nyumbani kwao, baba wa mume wake aliporudi alimwita mtoto wake Thomas na kumuagiza amfunge kamba mkewe , naye akafanya hivyo.

Akisimlia mkasa huo alisema baba mkwe alikwenda nyumbani kwa wazazi wake na kulalamika kuwa walikuwa wakimfundisha tabia mbaya, hatua ambayo ilizua ugomvi na kutokana na majibizano ya muda mrefu, mzee huyo aliokota kipande cha kuni na kumpiga nacho mama yake mdogo ambaye alikimbilia ndani na kutoka na panga na kupigwa nalo kwa kutumia ubapa wake.

"Baada ya kuanyiwa hivyo alikuja nyumbani, kamuita Thomas na kumwamuru anipeleke nikiwa nimefungwa kamba, naye akinamusha usiku na kunifunga kwa kamba mikononi na kunitoa nje.

"Baba mkwe alinieleza kuwa nyumbani kwenu wamenidhalilisha sana hivyo lazima na nikushikishe adabu, kisha akaanza kunikata sikio la kushoto taratibu kama anachinja nyama na la kulia na kunijeruhi sehemu nyingine," alidai Robhi akiwa katika hosptali ya Mkoa wa mara ambako amelazwa kwa matibabu.

Robhi amejeruhiwa sikio lote la kushoto na kuondolewa sehemu kubwa ya ngozi mpaka eneo la shavu na sikio la kulia lililokatwa na kubaki likining'inia.

Pia Rhobi alitaktwa kwenye mabega yote mawili, shavu la kulia pamoja na vidole vyote vya mkono wa kushoto.

Alidai kuwa baada ya mkwewe kumkata, alitupa chini kipande chasikio hilo kutupwa ambacho kugombewa na mbwa.

Kamanda wa Polisi mkoani Mara, David Ole Saibullu alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa mtuhumiwa alikamatwa siku nne baada ya tukio hilo na kwamba polisi bado inamsaka mume wa Robhi ambaye alitoroka muda mfupi baada ya tukio hilo.

SOURCE: Mwananchi
 
Kakalende naona unapotosha watu manake hata mimi ni mwenyeji wa mkoa wa Mara ila ukatili kama huu ni wa mtu binafsi na wala hauna uhusiano wowote na mapenzi
 
This is extremelly cruel I can't believe what am reading!Hivi Tz katka karne hii bado kuna ukatili namna hii kwa wanawake? tena msichana mwenyewe yuko under-age ana miaka 15 na ameolewa? kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni! Hivi kuna chombo gani kinachotetea hao watoto wanaolewa wakiwa na umri mdogo halafu wanaishia kunyanyaswa namna hii jamani!!! Si kosa lao ni mila potofu zinawafanya wanakuwa victim wa mambo hata yasiyiwahusu! Poor girl!
 
ndio maana watu wa kwetu wakawa wanaogopa kuozesha watoto wao watu wa bara kwa tabia kama hizi.

nnaamini si wote ila mambo haya husababisha watu kuwajumuisha wengi
 
Huu ni ukatili wa kutisha kutendwa na mwanadamu! Hili ni fundisho kwamba si kila mwenye sura ya binadamu ni binadamu! wengine ni viumbe tofauti na binadamu. Huyu ni zaidi ya mzungu wa Austria aliyemteka binti yake na kuzaa naye watoto saba! huyo naye si binadamu! Hawa wanahitaji recategorisation
 
Ah! Huyo jamaa ni mshenzi tu hapo sioni uhusiano wowote na mapenzi bora huyo binti angekatwa hayoo masikio na mumewe ingeeleweka may be tungesema ni wivu au fumanizi fulani lakini yamekatwa na baba mkwe jamani eh!!!???.
Dunia ni watu na watu wenyewe ndio hao au mzee alichombeza kabinti ili asafishe nyota kidogo kakamtolea nje akaamua kumgeuza kama pimbi....Kudadadeki mzee inabidi atulie kolokoloni kwanza...
 
Back
Top Bottom