Binti afufuka Mwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Binti afufuka Mwanza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtarajiwa, Oct 20, 2009.

 1. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushirikina upo wakuu msibishe!!
  Monday, 19 October 2009 07:28 [​IMG]binti alipokuwa shule ya msingi:

  [​IMG]binti alikodaiwa kuzikwa: Wakati wa mazishi yake huko Sweya Nyegezi, Kata ya Mkolani.

  [​IMG]Hapa akiwa katika Hospitali ya Bugando, wodi C-1 anakofanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa akili.

  *Madaktari Bugando wazungumza

  Na Jovin Mihambi, Mwanza

  "SIKUAMINI macho yangu baada ya kugundua mwanangu ambaye nilimuuguza katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kuanzia Septemba 30 mwaka 2005 na baadaye kufariki dunia Oktoba 3, mwaka 2005, tukamzika baadaye ninakutana naye akiwa hai!"
  Hayo ni maneno ya Bi. Stella Joseph ambaye ni mama mzazi wa binti anayedaiwa kufariki na baadaye kukutwa shambani miaka minne baadaye, Bi. Juliana Gembe (pichani).

  Baada ya kifo chake, inadaiwa kuwa mwili wake ulizikwa katika makaburi ya Sweya-Nyegezi, Kata ya Mkolani, wilayani Nyamagana kwa heshima zote zikiwemo misa, sala na maombolezo kutoka kwa wakazi wa maeneo ya Sweya.

  Aakizungumza na gazeti hili kwa uchungu, Bi. Joseph amesema kuwa binti yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria na alikuwa amelazwa katika wodi namba nane katika hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

  Alsema baada ya binti yake kufariki dunia, uongozi wa hospitali ya Bugando ulitoa kibali cha mazishi chenye Nambari 0861800 cha Oktoba 3, 2005 na marehemu kuzikwa siku hiyo hiyo kwa kufuata utaratibu wote wa mazishi, na baba
  paroko wa Parokia ya Mtakatifu Augustino, aliendesha ibada ya kumuombea marehemu.

  Mama huyo anasema hazikuwepo hisia wala imani zozote za kishirikina kwa sababu yeye ni mcha Mungu na kuwa anajali sana maombi, hata kuliko dawa za hospitali au mitishamba kwa ajili ya kuponya magonjwa mwilini.

  Anasema kuwa wakati akimuuguza mwanawe, mgonjwa huyo alikuwa akimwambia kuwa alikuwa anaona watu kadhaa wanafika kwa wingi kitandani mwake na kutaka kumchukua, na kuwa hata wakimchukua, atarudi tu na wala hawezi kuishi nao milele.

  "Mama, naona watu wananisogelea kwa wingi kitandani hapa, eti wanataka kunichukua eti wanipeleke nikalime, ila mimi wakidhubutu kunipeleka, mie ni jeuri nitarudi tu
  muda wowote," alisikika binti huyo akimweleza mama yake maneno ambayo yamenukuliwa na mama huyo.

  Akisimulia jinsi binti huyo alivyopatikana akiwa hai, Mjumbe wa CCM, Shina Nambari 5 Kitongoji cha Buhima, Malimbe-Nyegezi, Bw. Sadik Ramadhani, amesema kuwa mnamo Oktober 15, mwaka huu majira ya saa 10.00 jioni, alishtukia umati wa watu ukifika nyumbani kwake na kumweleza kuwa kwenye ubalozi wake ametokea kiumbe wa ajabu mwenye jinsi ya kike ambaye ni wa kutatanisha.

  Bw. Sadik alisema kuwa aliongozana na umati huo wa watu hadi mahali ambapo binti huyo alikuwa amekaa, huku akiwa akionekana kuchoka, kavalia matambala akiwa hawezi kuongea ila kwa ishala wakati alipokuwa akiulizwa kama anahitaji chakula.

  Bw. Sadik amesema kuwa alimchukua binti huyo hadi nyumbani kwake huku akiandamana na watu hao na kumpikia ugali ambao alikuwa anaumeza bila kutafuna.

  Amesema wakati akimchunguza zaidi, aligundua kuwa ulimi wake ulikuwa ndani na hauonekana huku akiwa na meno mawili moja likiwa juu na lingine chini. Pia mgogoni mwake kulikuwa na michirizi kama ya mtu ambaye alikuwa akichapwa fimbo.

  Bw. Sadik anasema binti huyo kwa muda mrefu alikuwa amefumba macho hata mtu akijaribu kumfumbua
  anayafumba tena, hali ambayo anaendelea nayo hata wakati huu akiwa katika wodi C-1 katika Hospitali ya Bugando akichunguzwa akili yake.

  Bw. Sadiki amesema kuwa kadri watu walivyokuwa wakimininika kwenda kumwangalia, baadhi yao walimtambua kuwa ni binti ambaye alifariki mwaka 2005 na baadaye kuzikwa. Wengine ni wale ambao walikuwa wanasoma naye katika Shule ya Msingi, Nyamalango iliyoko Nyegezi, jijini Mwanza.

  Amesema kuwa giza lilipoingia, ilibidi awatawanye watu wote waliokusanyika katika nyumba yake hadi siku iliyofuata wakati alipowasiliana na mtendaji wa Kata ya Mkolani ambaye alifika nyumbani kwake akiwa na polisi, wakamchukua hadi Bugando kwa uchunguzi zaidi.

  Mama mzazi wa binti huyo anasema alipokuchunguza halama zote alizokuwa nazo binti yake wakati wa uhai wake, alithibitisha kuwa ni mtoto wake ambaye alifariki mwaka 2005.

  Dk. Rodrick Kabangira wa Hospitali ya Rufaa Bugando katika wodi C-1 inayolaza wagonjwa wenye matatizo ya akili, amesema kuwa ugonjwa alionao binti huyo, unatokana na mtu kuishi mbali na jamii na pia kuishi sehemu moja bila ya kuongea na mtu.

  Naye Bw. Adina Sefania ambaye ni Mkuu wa Idara ya Afya, katika hospitali hiyo, alisema kuwa tayari idara yake ilishapokea matukio mawili ya aina hiyo lakini hili la sasa lina utofauti kidogo kutokana na kujitokeza mtu mmoja tu ambaye anadai kuwa mgonjwa ni binti yake.

  Amesema kesi aliyowahi kuipokea, ni ile ya mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la Peter, ambaye alifariki huko Ukerewe, na baadaye akaonekana na kukajitokeza ndugu wawili ambao walikuwa wakimgangania na matokeo yake alipopima vipimo vya DNA kwa ndugu waliokuwa wakimgangania, mmoja wapo ndiye aliyeonekana kuwa ana uhusiano naye.

  Amesema kuwa serikali, ilipotoa kibali cha kufufua kaburi hiyo, walikuta kisiki ndicho kilikuwa kimezikwa katika kaburi hiyo badala ya kukuta mifupa ya binadamu.

  Amesema kuwa hata hospitalini Bugando, itabidi vipatikane vipimo vya binti huyo pamoja na wazazi wake ambavyo vitasaidia kubaini kama huyo binti ni wa kwao au vinginevyo ndipo ndugu zake wataweza kupata fursa ya kwenda polisi ili kupata kibali
  cha kumchukua katika hospitali hiyo akipata nafuu.

  Hata hivyo, kiongozi mmoja wa ngazi ya juu katika hospitali alisema hakuna haja ya vipimo hivyo ambavyo ni gharama kwa vile ndugu walimtambua kutokana na alama na wakaleta picha alizopiga akiwa hai, ambao ni ushahidi tosha wa kuruhusu jamaa kumchukua binti yake endapo atapata nafuu.
   
 2. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,454
  Likes Received: 7,220
  Trophy Points: 280
  du uchawi utaisha lini?
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mashikolo. getegete..........mmmmh
   
 4. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Africa ndivyo ilivyo!
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  eeeh makubwa madogo yana nafuu jamani eeeeh
   
 6. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  I wish huyo binti akipata nafuu atawatambua hao wahalifu ili sheria ichukue mkondo wake, sitajali kama wananchi wataamua kuchukua sheria mikononi mwao.
   
 7. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,454
  Likes Received: 7,220
  Trophy Points: 280
  inabidi wachawi waseme huwa wanafanyaje fanyaje hadi kuwaaminisha watu mtu flani kafa kumbe wamefanya manoeuvres yao
   
 8. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  hatari kubwa hii, si ndio huko huko mambo ya albino yalikoshamiri? na uuaji wa vikongwe wenye macho mekundu...
   
 9. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii wanaita msukule!!!Nishawahi kusikia pia hawa watu wana uwezo wa kuruka na ungo mpaka ulaya au marekani au popote pale duniani.Sasa kwanini wasiiweke wazi hii science ili wale vichwa?HIi express service ingeharibu biashara yote ya ndege!!!
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hii ni sayansi ya kiafrika mwana wane teh teh..tuko juu
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Miafrika si hatusamini vya kwetu kama ingekuwa nchi za wenzetu (mfano Uraya) mbona ingesha endelezwa sana tu...
   
 12. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,454
  Likes Received: 7,220
  Trophy Points: 280
  sasa kwa nini siku moja wasiende au huko ulaya wayaibe maviwanda yote wayalete hapa,mabarabara yote,maviwanda ya ndege kule toulouse na hamburg wayalete huku
   
 13. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  tehe tehe tehe
  Labda wanaogopa kuitwa mahakamani wakiweka wazi.Si unaona wataalam wa gongo wanavyoteseka wakati kuna mapombe makali kushinda gongo yanaruhusiwa madukani...eti zimepimwa,za viwandani ulaya!!!!
   
 14. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndiyo hapo sasa
  halafu wataalam wa namna hii utakuta wamechoka kishenzi yaani masikini wa kutupwa
  uchumi wanao wanaukalia!!
   
 15. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwanini sayansi hiyohiyo isitumike kujenga barabara, mahospital, mashule, flyovers etc?
   
 16. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  nimesikitika sana ngosha! uchawi ni mbaya sana, uwe uchawi mweusi au uchawi mweupe wa wazungu. msiponde saana uchawi wa kibongo hata wazungu ni wachawi. msione muvi za harry poter na vempires mkadhani hamna mambo kama hayo, yapo sana!
  mara popobawa, gongagonga mara chumaulete! mweh!
   
 17. stanluva

  stanluva Senior Member

  #17
  Oct 20, 2009
  Joined: Apr 7, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni confidential mkuu! Ikijulikana kuwa umetoa siri kwa namna yeyote ile hamna rangi hutaacha ona mkuu!
  But kwa hii issue ya huyo dadaa dah! Mungu ndo anajua sipati picha pale itakapo julikana mhusika ni nani maana watampigaje?

  :rolleyes: :rolleyes: :rolleyes: :rolleyes: :rolleyes: :rolleyes:
   
 18. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kwa kisukuma inaitwa Mitunga. Hutokea sana na wengine hupelekwa Gamboshi kwa ajili ya kulima mji ambao mchana ni kijiji na usiku ni city babu kubwa umeme na magari ya kifahali lakini mchana ni nyumba za majani.
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  sasa kama dada hawezi kuongea atawataja vip hawa watu waliofanya uharifu huu???
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  hizi za ma vempires mie nikajua ni ubunifu tu
   
Loading...