Bingwa wa kubikiri Malawi akamatwa kwa amri ya Rais

Majighu2015

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,924
3,904
Rais wa Malawi, Peter Mutharika juzi alitoa amri ya kukamatwa kwa Eric Aniva ambaye hivi karibuni alibainika kufanya kibarua cha kuwabikiri mabinti wa chini ya umri wa miaka 13 zaidi ya 100.

Amri hiyo ya Rais imekuja baada ya kubainika kuwa mwanamume huyo maarufu kwa jina la ‘Fisi’ anaishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).

Mutharika alisema lazima mwanamume huyo akamatwe na hatua kali zichukuliwe dhidi yake kwa kuwa, kwa makusudi alifanya vitendo viovu akijua anaishi na VVU na lengo lake lilikuwa kuwaambukiza mabinti hao.

Aniva aliingia matatani baada ya kukiri katika mahojiano akijinasibu kuwa anaendesha maisha kwa kuwabikiri mabinti na kwamba hulipwa kuanzia dola nne za Marekani mpaka saba ambayo ni wastani wa Sh10,000 kwa kila mtu.

Mwanamume huyo alisema wazazi wa mabinti huwa wanampa kibarua cha kuwavusha kutoka utoto kuingia katika utu uzima na kwamba hatua hiyo ni sawa na tambiko.

Kwa wale wasio na VVU na niwataalamu wa kubukiri nafasi hiyo iliyoachwa na Mr.Fisi iko wazi
 
hivi hii nayo ndo tamaduni gn kwamba mzazi analipia kabinti kake kabikiriwe,yaani nao wanaifanya ni huduma ya kawaida tu mmmh this is Africa for really
 
Elimu hawana huko..Wanaendekeza mila za mwaka 1620
Saa nyingine nawaza kama ukoloni ulikuwa kitu kizuri kwa wa Africa. Maana walileta elimu na dini .

Angalia sehemu ambazo ukoloni hukufika. Bado wanaendea na mambo ya kijinga kama haya. Kubaka watoto wadogo kwa ruhusa ya wazazi .
 
Ni kweli kwa namna flani wakoloni walituzindua kutoka usingizini. Elimu kitu cha muhimu sana
 
Haya utayKuta kwa watu weusi tu da

Mzungu anapomdharau na kumbagua mwafrika ana maana na hoja ya msingi wakati mwingine
 
Saa nyingine nawaza kama ukoloni ulikuwa kitu kizuri kwa wa Africa. Maana walileta elimu na dini .

Angalia sehemu ambazo ukoloni hukufika. Bado wanaendea na mambo ya kijinga kama haya. Kubaka watoto wadogo kwa ruhusa ya wazazi .
kweli kabisa "desii"
 
Back
Top Bottom