binamu,cousin,niece,nephew....

Kwa waswahili wa pwani wana Ami wakimaanisha baba mkubwa na baba mdogo. Mjomba inatumiwa kwa upande wa mama tu
 
Neno 'mkaza mjomba' (mkaza wa mjomba) hupatikana zaidi maeneo ya pwani hususan kule Tanga wanalitumia sana neo hili wakimaanisha mke wa mjomba,kiingereza chake nafikiri ni 'aunt'. Kama wengine walivyoelezea

ok thanx
labda nikuulize kwa kiingereza 'mkaza wa mjomba' lol

halafu kama unajua kwa kiingereza mjukuu,kitukuu.kilembwe...lol
 
JINSI WATU WANAVYOHUSIKA KIDAMU/KINDUGU


Adult
mtoto ubarobaro (hali ya kufikia umri wa kubaleghe
kwa mvulana/kijana wa kiume)
Ancestor
mhenga, wa-, babu, ma-
Aunt
shangazi (dada wa baba)
mama mdogo (dada mdogo wa mama)
mama mkubwa (dada mkubwa wa mama)
Brother
Kaka
Brother-in-law
shemeji (wa kiume)
Cousin
(First) binamu ya karibu, (Distant) binamu ya mbali
Daughter
Binti, mtoto wa kike
Daughter-in-law
mkwe (wa kike), mkemwana
Family
jamaa, ukoo
Father
baba, baba mzazi
Father-in-law
baba mkwe
Granddaughter
mjukuu wa – (wa kike)
Foster brother
kaka wa kuchangia ziwa
Grandfather
babu
baba mzaa baba (paternal)
baba mzaa mama (maternal)
Grandmother
bibi
bibi mzaa baba (mama wa baba mzaa) (paternal)
bibi mzaa mama (mama wa mama mzaa) (maternal)
Grand-nephew
mjukuu wa kiume wa mjomba (shangazi)
Grand-niece
mjukuu wa kike wa mjomba (shangazi)
Grandparents
bibi na babu
Grandson/daughter
mjukuu wa kiume/kike, mtoto wa mtoto wa mtu
Grand-uncle
mjomba wa baba au mama
ndugu wa kiume wa babu au bibi
Great granddaughter
mtoto wa kike wa mjukuu
Great great granddaughter
mtoto wa kike wa kitukuu
Great great grandson
mtoto wa kiume wa kitukuu, kilembwe
Great grandson
mtoto wa kiume wa mjukuu, kitukuu
Mother
mama
Mother-in-law
mama mkwe *
Nephew
mpwa (wa kiume), binamu (mtoto wa kiume wa ami)
Niece
mpwa (wa kike)
Son
mwana, (waladi, [kishairi]), mtoto wa kiume

mtoto mwenye umri wa baina ya 7 na 12. (=kijana)
Sister
dada
Sister-in-law
shemeji wa kike, wifi
Son-in-law
mkwe (wa kiume)
Uncle
mjomba (kaka wa mama)
ami/amu (kaka wa baba)
baba mdogo (kaka mdogo wa kiume wa baba )
baba mkubwa (kaka mkubwa wa kiume wa baba)
mkaza, wa-
mke wa, bibi. Mkaza mjomba = mke wa mjomba
Woman’s female in-law
wifi (mainly a woman’s word)
kingng’ina
greatgreatgreatgrandson

Sijui kama jedwali hii itasaidia maelewano. Inapatikana mahali mbalimbali kwenye kamusi kama ile ya TUKI n.k. Naomba kwa nia ya kuikamiliisha wanatovuti wachunguze na kusahihihsa makosa na kujumuisha istilahi inayokosekana.
 
Back
Top Bottom