binamu,cousin,niece,nephew.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

binamu,cousin,niece,nephew....

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by The Boss, Oct 10, 2011.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  wataalamu hebu nifafanulieni hapa

  binamu ndio nani kwa kiingereza?

  na cousin kwa kiswahili?

  na niece kwa kiswahili?

  nephew kwa kiswahili????????

  asanteni.....
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,146
  Trophy Points: 280
  binamu ndio nani kwa kiingereza? = cousin

  na cousin kwa kiswahili? = binamu

  na niece kwa kiswahili? = mpwa

  nephew kwa kiswahili???????? = mpwa

  Kiswahili ni maneno machache sana yenye gender na hata kiingereza kina limits za gender, kiarabu hakina shaka ndani. Usihamanike.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  faiza asante

  hebu niambie tofauti ya binamu na mpwa......

  halafu hapo kwenye niece na nephew.....which is which....??????/
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,146
  Trophy Points: 280
  Binamu ni mtoto wa ndugu wa mama yako ndugu wa baba yako.

  Mpwa ni mtoto wa ndugu zako. Hawa "wapwa" ndio niece (wa kike) na nephew (wa kiume)
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  ok na mpwa yupi ni niece
  na yupi ni nephew....

  usichoke faiza...itwasaidia wengi....
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Oct 10, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Binamu ni watoto kwa watoto (peers). Kama mimi na wewe tuwe watoto wa mtu (kaka) na dada yake ndiyo tutakuwa mabinamu (cousins).

  Kama wewe ni mtoto wa dada yake na baba yangu basi utakuwa mpwa wa baba na mimi nitakuwa mpwa wa shangazi ambaye ndiyo nyoko (nyoko siyo tusi - maana yake ni mama yako). Kwa hiyo mpwa ni kwa mjomba na shangazi.

  Nephew ni mpwa wa kiume na niece ni mpwa wa kike.
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,146
  Trophy Points: 280
  Hawa "wapwa" ndio niece (wa kike) na nephew (wa kiume)
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  sasa 'cousin' hapo ndo naona kama
  umetofautiana na ff au ni maana hiyo hiyo?
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Oct 10, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Wala hatujatofautiana. Cousins ni binamuz. Lakini hao hao binamuz kwa jinsia zao wataitwa tofauti na wazazi. Wa kike ataitwa niece na wa kiume ataitwa nephew lakini wao kwa wao watabakia kuwa cousins (binamuz) bila kujali jinsia zao.
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,146
  Trophy Points: 280
  Nyani kidogo kuna marekebisho.

  Cousins sawa ni "binamus" lakini niece na nephew ni wapwa. Yaani ni watoto wa ndugu zako.
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  unajua kingereza na kiswahili kwenye familly kuna tofauti...

  mfano baba mkubwa na baba mdogo

  wengine wanaita uncle......sijui tuiteje....

  hivyo hivyo shangazi kwa kiswahili ni dada wa baba

  but tunawaita mama wadogo kama aunt na ukiulizwa aunt ni nani?tunasema shangazi...

  its complicated
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Oct 10, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Tuko pamoja. Mama au baba, mjomba au shangazi, ndiyo watawaita hao watoto nephew na niece kulingana na jinsia zao. Watoto kwa watoto hawawezi kuitana nephew na niece. Wao kwa wao wataitana cousins (binamuz). Si ndiyo?
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kwa ufupi nieces na nephews ni watoto wa cousins....

  na cousins ya kizungu ni mtoto wa baba yako mdogo,mkubwa,mjomba,shangazi na kadhalika....sawa???????
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Oct 10, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ngoja nikupe huu mfano ambao nadhani ni rahisi kuuelewa. Chukulia mimi na wewe ni ndugu. Baba mmoja na mama mmoja. Pia tuna dada yetu. Kwa hiyo tumezaliwa watatu.

  Mimi ni mkubwa kwako. Wewe unanifuatia na dada yetu ndiyo kitinda mimba. Kwa hiyo mimi na wewe ni mtu na kaka yake/ mtu na mdogo wake. Mimi ni kaka mkubwa, wewe unafuatia na dada yetu (mdogo wetu) ndiyo wa mwisho kuzaliwa.

  Mimi nimeoa na nina watoto wawili. Mmoja ni wa kiume na mmoja ni wa kike. Na wewe umeoa na una watoto wawili pia. Watoto wako wote ni wa kike. Dada yetu (mdogo wetu) yeye bado hajaolewa ila ana mtoto mmoja wa kike.

  Hao watoto wangu wewe utakuwa baba yao mdogo (kwa Kiingereza uncle). Mdogo wetu wa mwisho atakuwa shangazi yao (au auntie kwa Kiingereza). Mwanangu wa kiume kwako atakuwa mwanao lakini kwa Kiingereza atakuwa nephew. Mwanangu wa kike atakuwa niece.

  Vivyo hivyo, mwanangu wa kiume atakuwa nephew (mpwa) kwa shangazi yake (ambaye ni mdogo wetu wa mwisho). Na yule wa kike atakuwa niece (mpwa wa kike).

  Watoto wako mimi nitakuwa baba yao mkubwa. Lakini kwa Kiingereza hakuna baba mkubwa. Baba mkubwa au mdogo wote ni uncles. Kwa hiyo mimi nitakuwa uncle wao hao mabinti zako wawili. Nitawaita nieces.

  Shangazi yao (kitinda mimba wetu) atawaita hao mabinti zako nieces pia. Sasa huyu kitinda mimba wetu si naye ana mtoto kike - basi huyo binti yake sisi atatuita wajomba na sisi tutamuita yeye niece.

  Watoto wangu mimi, watoto wako wewe, na mtoto wa huyo dada yetu mdogo wao kwa wao ndiyo mabinamu (cousins).

  I know it's kinda convoluted but I hope you'll understand. If not let me know.
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  asante nilikuwa naelewa hivyo
  nahisi umejibu swali langu kuwa mjomba na shangazi ya kiswahili siyo sawa na uncle na aunt....
  nafikiri nimeelewa....
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Oct 10, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Uko sawa. Kwa Kiingereza baba wakubwa, baba wadogo, mama wakubwa, mama wadogo, wajomba, na shangazi wote ni uncles na aunties. Ili kuleta umahsusi zaidi huwaga wana qualify kwa kusema 'on my mother's side' au 'on my father's side'. Kwa mfano, 'my uncle on my father's side' au 'paternal uncle/ aunt' au 'maternal uncle/aunt'.
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  ok thanx
  labda nikuulize kwa kiingereza 'mkaza wa mjomba' lol

  halafu kama unajua kwa kiingereza mjukuu,kitukuu.kilembwe...lol
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Oct 10, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Grandchild, great-grandchild, great-great grandchild.
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,146
  Trophy Points: 280
  Nieces na nephews wanaanzia kwa watoto wa kaka na dada yako halafu mpaka kwa watoto wa cousins ni hivyo hivyo.
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,146
  Trophy Points: 280
  Tuko pamoja.
   
Loading...