Binamu, binamu ananikwanza nifanyeje mwenzenu

Binamu, binamu ananikwanza nifanyeje mwenzenu

nina binadamu yangu, mtoto wa shangazi yangu kabisa mama yake wa kwanza kuzaliwa akafuata baba yangu, kiukweli ananikwanza huyu binadamu sijui nifanyeje, mwaka 2011 alianza kutaka kunioa akaenda hadi kwa mjomba wake ambaye ni baba yangu, nikamwambia haiwezekani japo kikwetu kwetu kuoona binadamu c mbaya lkn kwa upande wangu siko tayari kuolewa na binamu.

Baada muda kupita alitafuta mwamke na kuanza kuishi nae, lkn july 8 mwaka huu akamuacha yule mkewe na kurudi tena kwangu tena karudi kwa speed kali sana, ananisumbua mara kwa mara anakuja usiku kunigongea huku nikiwa nimelala usiku wa manane, sina raha nimfanyeje huyu binadamu kwani me nina mambo zangu, siihitaji kuwa nae yaani simuhitaji, nimezungumza nae sana naona hanielewi. Nifanyeje sasa!!.

hao ni waha ndio wanatabia chafu yakutembea na ndugu zao. Binamu ni ndugu yako acha uchafu utaridhi mambo ya family zote mbili hiyo itakuwa familia. Kimbia mwambie akome kabisa
 
Wote uliowakataa ulienda kwa mama zao!!!!!!

Wewe ni kiboko aiseee


watu8 huyu kwa sasa anachokifanya ni km kutumia nguvu kwa nini simtaki
na pia huyu ndi ndugu yangu kile ninachomwambia kuwa me sikipendi yy ndo anazidi
kwa madai kuwa me ndo mkewe toka kwa mungu
siwezi jua aniwazia nini kwa mara ya mwisho kunigongea ili kuwa jana
aligonga wala sikumfungulia, wakati anaendoka anasema wajifanya jeuri utaona tu
 
kwangu naona km ni laana hiv, mtu yeyote ambaye nitasikia kuna kaundugu udungu siwezi lala nae
hiyo nishasema kitambo, kwa maombi yako nitafanikiwa

Nizungumzie hapa....huyu mtu ana lake jambo kwani kama kamuacha aliyemuoa wewe una lipi usiachwe???? Kuja kukugongea usiku ni ujasiri wa kuweza kukubaka au kukudhalilisha na mwanamme mstaarabu na mwenye hekima na busara na mwenye kumheshimu mwanamke hizi sio mbinu za kumpata mwanamke.....Ushauri...Inabidi ughangamale kama msichana na uweke ubinamu pembeni na umwambie "sihitaji kuwa na wewe kwani sikupendi na kama ukilazimisha ndani ya siku 2 nitaenda kukuripoti police ili upewe tahadhari ya kutonifuata"....wakati huu uonyeshe sura ya kukerwa na tabia zake na kama hatatekeleza nenda kamripoti police kwani amini huyu anaonekana mwenye uwezo wa kukutenda baya muda na saa yeyote.
Nikupongeze kwa kutetea haki yako ya mapenzi kwani ni wanawake wengi wameshindwa kufanya hivyo na kujikuta wanadhulumiwa na wazazi au ndugu. Kama litakushinda uko huru kuniPM nikupe mbinu zaidi hata kama muda mrefu utakuwa umepita kuanzia sasa. Mwisho kuna madhara pia ya Kibayolojia kwa watu wenye homoni zinazofanana kama wewe na binamu yako kushiriki mapenzi na hata kuzaa hivyo usikubali hili jambo pia kwa afya sahihi ya uzao wako. Mungu akutangulie hadi ushinde hiki kishawishi.
 
  • Ninauza Tindikali kwa bei poa kabisa.
  • Ukinipatia namba yako kama upo Dar es salaam tunafanya delivery free of charge.
  • Lita moja buku 3 tu.
  • For more info nicheki PM.
 
watu8 huyu kwa sasa anachokifanya ni km kutumia nguvu kwa nini simtaki
na pia huyu ndi ndugu yangu kile ninachomwambia kuwa me sikipendi yy ndo anazidi
kwa madai kuwa me ndo mkewe toka kwa mungu
siwezi jua aniwazia nini kwa mara ya mwisho kunigongea ili kuwa jana
aligonga wala sikumfungulia, wakati anaendoka anasema wajifanya jeuri utaona tu

Ok then kama na vitisho vimeanza hapao si sawa!!!

Wanasema mcheza kwao hutunzwa kama ni kweli alomfuata mjomba wake ambaye ni baba yako inamanisha na.mama yako (kama yupo) naye atakuwa anafahamu. Sishauri uende kwao kwa sababu waweza kuta wao ndo wamekupendekeza wewe baada ya jamaa kuhangaishwa huko alikotoka.

Nakishauri anzia kwenu kwa wzazi wakimbushe ilivyokuwa na ilipofikia then muombe mzee wako apeleke ujumbe kwa dada na shemeji yake kuwa wewe una maamuzi tofauti na mahitaji ya huyo jamaa na una maisha yako tayari na uweke wazi kuwa kama hili hawatalishughulikia basi utafuata mkondo wa sheria hususan hapo kuwa utaona!!!!!

Kama ungekuwa dada yangu kesi hii wala si ngumu asilani
 
Muonjeshe ili akinai!!hatakufuata tena

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Sidhani kama kumripoti polisi mdogo wako ni sahihi!
Si dhani kumgonganisha na bwana wako ni sahihi! Anaweza akarusha makofi kwa bwana wako! Si unajua anakajastification "...mimi huyu mdogo wangu..!"
hapa nakubaliana na waliokushauri upeleke kesi kwa wazee! Kabla ya kufanya hivyo ningeshauri umuonye, akiendelea mwambie unapeleka kesi kwa Mamito wake! Akiendea fanya kama ulivyomtahadharisha!
Kitu ki1 usisahau! Yule ni ndugu yako, kama yeye kapanguka, wewe usijipangue kwa maamuzi makali dhidi yake (police na kumgonganisha)
ili kesi ikimaliza muwe peace!
 
Nimekupata mkuu


Ok then kama na vitisho vimeanza hapao si sawa!!!

Wanasema mcheza kwao hutunzwa kama ni kweli alomfuata mjomba wake ambaye ni baba yako inamanisha na.mama yako (kama yupo) naye atakuwa anafahamu. Sishauri uende kwao kwa sababu waweza kuta wao ndo wamekupendekeza wewe baada ya jamaa kuhangaishwa huko alikotoka.

Nakishauri anzia kwenu kwa wzazi wakimbushe ilivyokuwa na ilipofikia then muombe mzee wako apeleke ujumbe kwa dada na shemeji yake kuwa wewe una maamuzi tofauti na mahitaji ya huyo jamaa na una maisha yako tayari na uweke wazi kuwa kama hili hawatalishughulikia basi utafuata mkondo wa sheria hususan hapo kuwa utaona!!!!!

Kama ungekuwa dada yangu kesi hii wala si ngumu asilani
 
Mpeleke kwa kamanda kova atapata kesi ya ujambazi na hatia ya kumiliki bastola

Hapa atakuwa amemaliza kabisa kero. Ila umesahau ile kesi maarufu ya kuwa kwenye mtandao wa matapeli wa Dar es salaam.
 
mmmmmmhhhhh! wanawake kweli tupo wachache siku hizi.
 
Dawa ni kutafuta 'boyfriend wa mda'
awe bouncer
akijileta apewe mkongo'to wa haja
hatarudia...

au usiku uko na kitandani na kidume
akigonga unamwambia fungua tu
aingie akuone una underwear tu kitandani na kidume kiko kifua wazi
harudii,trust me
 
Nina binadamu yangu, mtoto wa shangazi yangu kabisa mama yake wa kwanza kuzaliwa akafuata baba yangu, kiukweli ananikwanza huyu binadamu sijui nifanyeje, mwaka 2011 alianza kutaka kunioa akaenda hadi kwa mjomba wake ambaye ni baba yangu, nikamwambia haiwezekani japo kikwetu kwetu kuoona binadamu c mbaya lkn kwa upande wangu siko tayari kuolewa na binamu.

Baada muda kupita alitafuta mwamke na kuanza kuishi nae, lkn July 8 mwaka huu akamuacha yule mkewe na kurudi tena kwangu tena karudi kwa speed kali sana, ananisumbua mara kwa mara anakuja usiku kunigongea huku nikiwa nimelala usiku wa manane, sina raha nimfanyeje huyu binadamu kwani me nina mambo zangu, siihitaji kuwa nae yaani simuhitaji, nimezungumza nae sana naona hanielewi. Nifanyeje sasa!!.

Muonjeshe mara moja tu ataacha kukusumbua. Kwani binamu ni nyama ya hamu!
 
Back
Top Bottom