Binafsi sipendi wanawake wapambanaji kupitiliza

Binafsi sipendi wanawake wapambanaji kupitiliza

Nelson Kileo

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Posts
3,062
Reaction score
3,280
Direct kwenye mada.

Kuna wanawake wanajikuta wapambanaji sana, kila biashara inayoibuka wanajikuta kushiriki; mara kuuza vitenge, sijui vyombo online mara ana vikoba saba, mara boxer na vest, mara kwnye magauni na chupi za kike wapo!

Aisee kwa mimi inanikera sana kuwa na mpenzi wa namna hiyo, wengi nyie wanawake mna mapepe mkidhani kuzurura hovyo kwenye biashara mbalimbali tutawaona wapambanaji. But hell NO, kwangu (I think pia kwa wanaume wengi) ukiwa na hilo wenge halivutii kabisa.

Why dont you stick kwenye one Bussiness?

Mihangaiko yenu yote wala hailetagi matokeo chanya.

Mimi naonaga wanawake jukumu lao ni moja tu. Kukaa ndani, kulea familia na kutunza nyumba.

Wanawake acheni kuwa wanaharakati.
 
Nafikiri ni hali za maisha zinazofanya mtu apambane huku na huko.
Watu wana majukumu yamewalemea, majukumu yote yanahitaji money unategemea atatulia na biashara moja?

Okay, kubaki kwenye biashara moja inawezekana lakini inabidi iwe ni biashara kubwa ambayo pia inahitaji mtaji mkubwa.

Sasa niambie, mama anayekaanga maandazi asubuhi faida yake haizidi 5,000TZS, halafu mchana ashinde amelala? Hapo ana majukumu ya kutosha na yote yanahitaji fedha.
 
Mngekuwa mnasimamia majukumu ipasavyo kwa hao wanawale wala wasinge haha, wimbi la wapambanaji limeibuka baada ya wimbi la ma marioo kuongezeka ndomana humu ndani kila kukicha nyuzi za wanaume kulalamika wanaombwa pesa.

Any way tafuta goal keeper wako weka ndani hakuna ataekuuliza bro
 
Mkuu acha wapambane wapunguze kuomba hovyo, pia kumbuka ikitokea baba wa familia umerudisha namba kwa Mungu, mtu pekee atakaebakia na mahangaiko ya watoto ni mama, hao ndugu unaowaona ni kama mapambo tu, acha wapambane ukiona wanakosea sehemu wasaidie kwa mawazo ili wanufaike zaidi.
 
Kuna mtu alimwambia mke wake ana tamaa ya hela, kisa mwanamke ni mpambanaji akiona fursa anapita nayo kama ipo ndani ya uwezo wake.

Kumbe wa aina hii mpo wengi, me naona ni mawazo mgando hayo. Mtu kama ana nguvu na utayari wacha ahangaike, tena ungeshukuru Mungu kumpata wa hivyo maana kuna wenzako wanalalamika wake zao kutwa kuwapiga vibomu hela za vikoba na hawataki kujishughulisha.

Maisha yamebadilika sana, ni vizuri mkasaidiana na kupeana 'sapoti' katika majukumu yenu pia inaongeza mapenzi ndani ya nyumba maana maisha yanakua mazuri, siku ukikosa wife anasimamia show bas maisha yanasonga.
 
Huyo mwanamke hapendi kufanya hivyo, sababu kubwa inayopelekea kushika shika kila biashara tena huwa ni biashara zisizohitaji mtaji mkubwa ni majukumu aliyonayo, faida anayoipata katika biashara hiyo ni ndogo kuendesha maisha yake + familia hivyo hujikuta anadunduliza huku na kule ili apate angalau faida itakayomwezesha kuendesha maisha yake.

Na hakuna mwanamme/mwanamke anayependa kutapa tapa katika biashara.
 
Nyie ndio wale mke akipata kazi mna mind kama kaua mtu. Akikuzidi kipato ndio kabisa ndoa inavunjika.

Kiufupi una tabia fulani za kikoloni koloni unapenda kuona mkeo akiwa kama mtumwa wako akunyeyekee akuombe mpaka vocha ya jero.

Amka usingizini mkuu wanawake wenyewe kule Beijing walikubaliana ofikapo 2020 mambo yawe 50/50.
 
Yani umenikuta nafanya kazi napambana unioe uniambie niache Aiseee 😏😏

Utaniambia Kati ya wewe na kazi Nani kamkuta mwenzake 🤔
 
Mngekuwa mnasimamia majukumu ipasavyo kwa hao wanawale wala wasinge haha, wimbi la wapambanaji limeibuka baada ya wimbi la ma marioo kuongezeka ndomana humu ndani kila kukicha nyuzi za wanaume kulalamika wanaombwa pesa.
Any way tafuta goal keeper wako weka ndani hakuna ataekuuliza bro
wimbi la wapambanaji limeibuka baada ya wimbi la ma marioo kuongezeka
😁😁😁😁😁
 
Direct kwenye mada.

Kuna wanawake wanajikuta wapambanaji sana, kila biashara inayoibuka wanajikuta kushiriki; mara kuuza vitenge, sijui vyombo online mara ana vikoba saba, mara boxer na vest, mara kwnye magauni na chupi za kike wapo!

Aisee kwa mimi inanikera sana kua na mpenzi wa namna hiyo, wengi nyie wanawake mna mapepe mkidhani kuzurura hovyo kwenye biashara mbalimbali tutawaona wapambanaji. But hell NO, kwangu (I think pia kwa wanaume wengi) ukiwa na hilo wenge halivutii kabisa.

Why dont you stick kwenye one Bussiness?

Mihangaiko yenu yote wala hailetagi matokeo chanya.

Mimi naonaga wanawake jukumu lao ni moja tu. Kukaa ndani, kulea familia na kutunza nyumba.

Wanawake acheni kuwa wanaharakati.
Mkiacha kututelekeza, mkatugea mahitaji yote bila manyanyaso! Hata nje mguu sitoi! Sa nihangaike na nn kila kitu napewa jamani!
 
Hatukuumbwa kuhangaika ila manyanyaso ya wanaume na kutotunza familia wanawake wanaona bora watafute pesa zao
 
Back
Top Bottom