Binafsi namuelewa Spika Job Ndugai

Binafsi namuelewa Spika Job Ndugai

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,096
Nina mtazamo tofauti kidogo kuhusiana na tabia ya "ukali" wa Spika wa Bunge la JMT, Ndg. Job Ndugai hasa katika Awamu hii ya 5.

Zama zimebadilika. Taasisi na mihimili imeanza kuonesha makali ya kusimamia maadili na principles tofauti na kubembelezana kama tulivyozoea.

Ukali wa Ndugai unaonekana wa ajabu kwa sababu sivyo tulivyozoea. Tulizoea kuchekeana kwenye mambo serious na hata yale madogo madogo ambayo mwishowe yalipelekea vyombo vya uongozi kudharaulika na kutoheshimika. Likiwemo Bunge letu tukufu.

Ndugai anarudisha heshima ya Bunge the hard way. Kuanzia nidhamu za wabunge mpaka wanaofanya nalo kazi na hata wananchi wanaoshindwa kulipa heshima yake.

Anachokifanya Ndugai kwa maslahi ya Bunge, kinafanywa na Rais Serikalini na Judges huko Mahakamani.

Mihimili hii mitatu inafuata falsafa moja kwa sasa. Nidhamu.

Jeshi la Polisi na JWTZ nao tumeona wameanza kufuata njia hiyo hiyo.

Namuelewa sana Job Ndugai. Nyakati zimebadilika. Tuache mazoea.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well said ndugu..huu ndio ukweli wenyewe..lazima watu tubadilike twende na nyakati za sasa..tupo katika vita ya kiuchumi sasa kwa sababu tumeamua wenyewe kupaa kiuchumi..ni lazima sasa tupitie njia ngumu na sio kiulainilaini kama watu walivyozoea..kuelekea uchumi wa kati wa viwanda si mchezo , si lelemama..nakupongeza kwa uelewa huo
 
Ukali kwenye mini? He,no kwenye kuisimamia serikali mf. Kutoheshimu bajeti waliyoipitisha? Au ni kwenye kutetea RAIA na bunge mfano mbunge kupigwa risasi akiwa kazini,je,nikwenye kutunga sheria zinazokabili majizi ya rasilimali??

Ukali unatakiwa uelekezwe kwenye kazi muhimu sio mambo ya hovyohovyo!! Ukali kiss umekosolewa?? Huo ni ujinga wa hali ya juu.

Binadamu wrote tumeumbwa na udhaifu hakuna aliyekamilika hata mmoja kwahivyo kuambiwa mnamadhaifu hiyo ni kawaida kwa mtu usopenda majivuni na kutaka kuogopwa.
 
well said ndugu..huu ndio ukweli wenyewe..lazima watu tubadilike twende na nyakati za sasa..tupo katika vita ya kiuchumi sasa kwa sababu tumeamua wenyewe kupaa kiuchumi..ni lazima sasa tupitie njia ngumu na sio kiulainilaini kama watu walivyozoea..kuelekea uchumi wa kati wa viwanda si mchezo , si lelemama..nakupongeza kwa uelewa huo
Watu hawataki kubadilika. Lazima heshima na nidhamu iwepo. Uhuru wa kuongea haina maana kutusi na kudhalilisha au kusema lolote tu ilimradi.

Kuna wabunge wanatoa kauli za ajabu mpaka ikawa tunajiuliza hawa jamaa wanavuta bangi kwanza kabla ya kuingia kwenye session?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukali kwenye mini? He,no kwenye kuisimamia serikali mf. Kutoheshimu bajeti waliyoipitisha? Au ni kwenye kutetea RAIA na bunge mfano mbunge kupigwa risasi akiwa kazini,je,nikwenye kutunga sheria zinazokabili majizi ya rasilimali?? Ukali unatakiwa uelekezwe kwenye kazi muhimu sio mambo ya hovyohovyo!! Ukali kiss umekosolewa?? Huo ni ujinga wa hali ya juu...
Binadamu wrote tumeumbwa na udhaifu hakuna aliyekamilika hata mmoja kwahivyo kuambiwa mnamadhaifu hiyo ni kawaida kwa mtu usopenda majivuni na kutaka kuogopwa.
Suala la Mbunge kupigwa risasi ulilifuatilia vizuri mkuu?

Unajua role iliyochezwa na Bunge na Serikali kuokoa uhai wa Mbunge huyo katika hatua za awali kabisa kabla siasa hazijaingia na kuanza kupandishiana mabega?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
baada ya wiki 2-3 ukija soma upya hiki ama ukikisoma huko fb unaweza mtukana mtoa mada na kuhisi ni punguani kumbe mada ni yako mwenyewe.

unarudisha nidhamu bila ya kujiuliza kwa nini ilipotea, badala ya kujiukiza kuitwa imara kuna faida gani ikiwa unashindwa simami serikali.

kuitwa dhaifu kuna hasara gani kuliko kushindwa kuwawajibisha wabadhirifu

nidhamu za kipumbavu
 
baada ya wiki 2-3 ukija soma upya hiki ama ukikisoma huko fb unaweza mtuana mtoa mada na kuhisi ni punguani kumbe mada ni yako mwenyewe.

unarudisha nidhamu bila ya kujiuliza kwa nini ilipotea, badala ya kujiukiza kuitwa imara kuna faida gani ikiwa unashindwa simami serikali.

kuitwa dhaifu kuna hasara gani kuliko kushindwa kuwawajibisha wabadhirifu

nidhamu za kipumbavu
Tuheshimiane kwanza ili tusikilizane na kushirikiana. Huwezi kunidharaulisha halafu ukatarajia tutahusiana vizuri.

Mambo mengi sikubaliani na Ndugai, lakini hili la kusimamia heshima ya Bunge namuunga mkono.

Tukosoane kistaarabu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom