Binadamu wa kwanza ni yupi? Wa Olduvai au Adam

Status
Not open for further replies.

RayB

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
2,751
196
Hii ni hoja binafsi ambayo leo nataka kutafakari pamoja kati ya vitu hivi viwili vinavyochanganya. Napenda kuzungumzia kitu kinaitwa 'Binadamu wa kwanza'. Wakati vitabu vyetu vya dini vinatuambia kuwa binadamu wa ni Adam na akafatia Eve, lakini sayansi na hasa wale wana historia wanasema binadamu ni matokeo ya Evolution tukitokea kwa wanyama wenye asili ya sokwe na tena kwa kuongeza zaidi ni kuwa binadamu wa kwanza inaaminika kuwa alitokea Tanzania maeneo ya kule Olduvai.

Vitu hivi naamini vinakanganya na ni kila mmoja alishawahi kufikiria lakini hakuweza kuingia ndani zaidi na kujua lipi ni lipi. Tanzania waamini wa dini ni wengi kuliko wasioamini na zote zinaamini katika lile la kwanza lakini bado watu hao wanaitangaza Tanzania kuwa ni sehemu ya kutalii kwani moja ya vivutio vyake ni sehemu ile ambako binadamu wa kwanza anaaminika kuishi. Na sisi sote tumepitia katika masomo haya na tulikuwa tuaamini hivyo na kisha tukafaulu kweli na wewe muumini mzuri ulifurahia sana ulipofaulu somo hili tena ukapata vizuri sana lile swali lililouliza kuwa binadamu wa kwanza aliishi wapi? Je tulifanya makosa?

Naamini nitapata mawazo mbali mbali na changamoto nyingi katika hili pale tu mtakapotoa hofu ya kujiuliza tena hili swali
 
Kwanza kabisa, hivi vitabu vya dini ni myths tu.Vinasema dunia imeumbwa miaka 6,000 iliyopita wakati tunajua kutoka historia kwamba Egyptians tayari walikuwa wakiishi kwenye bode la mto Nile kwa wingi hata kabla ya hapo. Na kuna miamba iliyopimwa na kuonekana ina miaka 4.5 billion. Kwa hiyo huwezi kumzungumzia Adam na biblia katika context ya kisayansi halafu watu wakakuchukulia seriously.

Pili archaeology inaweza kutuambia the oldest remains zimegunduliwa wapi, haiwezi kutuambia mtu wa kwanza alikuwa wapi.

Tatu, kama unaamini scientific theories inabidi ueleze vizuri unamaanisha nini unaposema "binadamu". Unamaanisha Homo sapiens sapiens au unaweza kuwaunganisha kina Zinjathropus, Homo Erectus na kina Neanderthal man?
 

Kiranga;Ur still missing some very important clues espoecially on the issue of the advocacy of the the holly scriptures as well as on the existence of God. That's why I'm envieing for an extra JUKWAA, jukwaa la falsafa. Now here we go just to clarify your confusion especially on the issue of when rocks (miamba) began to exist "HAPO MWANZO MUNGU ALIZIUMBA MBINGU NA NCHI, NAYO NCHI ILIKUWA UTUPU ......" ....."ROHO YA MUNGU IKATULIA JUU YA VILINDI VYA MAJI, MUNGU AKASEMA,...."Hii imanamaanisha nini?1. Siku ya uumbaji roho yake ilitulia juu ya vilindi vya maji, halafu akaanza kuumba2. Wakati anaanza uumbaji siku hiyo, maji, mbingu na nchi vilikuwepo tayari, yaani ardhi na miamba yake na maji yake tayari vilikuwepo toka nyuma, possibly miaka mingi zaidi kuliko hata sayansi inavyosema!Contradictions sikatai zipo nyingi mno lakini kwa hili inabidi uliangalie vizuri!
 
kuwa binadamu wa kwanza inaaminika kuwa alitokea Tanzania maeneo ya kule Olduvai.

kwa kuku update
kuna nyayo za binadamu wa kale zaidi kuliko yule wa Olduvai, zipo sehemu iitwayo LAETOLI ndani ya hifadhi ya ngorongoro


Photograph by John Reader.
What makes these prints an almost unbelievable discovery are that not only are they clearly made by fully bipedal[FONT=Trebuchet MS, arial, helvetica, sans-serif]1[/FONT] creatures, but are also almost indistinguishable from modern human footprints, despite being formed millions of years earlier than the earliest known fossilised human footprints.
unaweza soma zaidi hapa [ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Laetoli[/ame]
 

Inawezekana ni yule yule wa olduvai alitembelea na huko si unajua tena walikuwa ni watu wa kutembea sana
 
RayB, hebu tizama article ya huyu jamaa, it is quite convincing (At least to me)!

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]
Bible and Scientific Reasoning: Is Adam the First man?
By: Ehimwenma E. Aimiuwu
2006

[/FONT][FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][/FONT][/FONT]
[/FONT][FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][/FONT]
 
SMU nashukuru kwa long article ambayo imani nyingi na hasa hizi kubwa dogma kuhusu hawa na adamu sasa hizo ni moja ya influential ideas na naamini upande wa pili kulikuwa na majibu yao na pia uksoma Genesis inaeleza kuwa hao watu walitokea wapi ingaw haiwataji kwa majina bali ni uzao wa adamu na hawa na wakamultiply kihivyo still ni mkanganyiko tu kwa kweli
 
Nakuandalia meelezo kuhusu binadamu kwa kwanza, wa pili, watatu na wanne, n.k. I mean RED MAN, BLACK MAN, WHITE MAN na YELLOW MAN. n.K. kutoka katika unpopular history kutoka katika spiritual science Hupo hapo? Baadaye nitakuhadithia sababu za wewe kuwepo hapa katika Earth Planet ni nini, maana uenda una fanana na kitoto kinachosoma shule ya vidudu au chekechea, kikiilizwa kwa nini kipo pale shuleni kinamnukuu aliyekipeleka alivyosema kama alikiambia.
Jiandae.
 

JUst bring it up no need of this intro thats why am here for learning and contribution to what i know so no need of using harsh words just be wise and contribute you ideas
 
swali zuri mkuu....

kwa wanadini...ni Adam

kwa waumini wa nadharia ya Darwin.......binadamu wa kwanza alianza katika umbile la nyani.

huyu wa olduvai gorge....sifahamu anaingia wapi hapo....nadhani ni mwanadamu wa kale zaidi ambaye tumewahi kuona athari yake kwa hizo nyayo...sidhani kama ni wa kwanza kwa yoyote kati ya nadharia hizo mbili..
 
Biblia ni mythology ya Wayahudi w kale tu, haina authenticity.

I mean kweli unaweza kukiamini kitabu kinachosema jua linazunguka dunia?

Unaweza kuamini kitabu chenye inconsitencies kama za biblia?

I mean hata ukitoka kwenye old testament na kwenda kwenye new testament, Mark, Luke, John na Paul wanajicontradict each other. Hiki ndicho kitabu cha kukiamini kama "gospel truth" kweli?

And this is just from the New Testament, sijaingia kwenye old testament huko kuonyesha kwamba Jesus Christ si Masiha kwa sababu hajakamilisha nabii za masiha.Unafikiri kwa nini Wayahudi wenyewe ambao hivi vitabu ni vyao hawamkubali kama Masiha?

http://www.evilbible.com/contradictions.htm

 

Hivi ni wangapi wanaoamini dini (hao wengi) na wasio amini (hao wachache) au unakisia tu iko hivyo? Ninaamini kila mwadamu ana dini! Hata hao tunaowaita 'atheists' wana dini. If you don't believe in one thing (e.g. A) you certainly beleve in something else (e.g. B, C, D... or Z)! It's impossible to believe in nothingness unless that nothingness is also something.

Binadamu wa kwanza kulingana na scriptures ni Adam na Eva (mume + mke). Whether huyo Adam + Eva ndio mmojawapo au wote wawili ndio waliogunduliwa Olduvai Gorge au hapana bado haipingani na scriptures. Hivi huyo mtu wa kwanza (Olduvai) alikuwa anaitwa nani? Was he single or married? Does the whole world believe so au ni historia ya EA au Afrika tu inasema hivyo?

2. Object ya imani ni Mungu na ya science ni experiment. Imani inahusu vitu 'spiritual' na science 'material' - two aspects of one reality. Ya kwanza, inahusu kuwa na uhakika wa vitu ambavyo hatuwezi kuvithibitisha au kutovithibitisha lakini tunaamini vina maana katika maisha yetu na kweli vipo. Science inahusu vitu ambavyo tunaweza kuvielezea kwa akili yetu.

Imani inahusu uwepo wetu na hatma ya maisha yetu (ya baadaye). Science inahusu vitu tunavyoweza kuvigundua tu (haizungumzii vile ambavyo hatuwezi kuvigundua). Imani inahusu vitu ambavyo ni beyond our understanding and perception (transcendence) - inatuasa tuishi kiadilifu na kwa upendo. Science inahusu vitu ambayo tunavijua tu (immanence) na tunaweza kuvifanya.

Kwa hiyo, ukisoma science ina approach yake na imani ina approach yake pia. Imani inatufanya tujione tunatoka kwa Mungu anayetulinda na kututunza na anataka tuishi kwa upendo na kuheshimiana na science inatufanya tu'explore' kwa akili yetu tu mazingira yanayotuzunguka na namna gani tunaweza kuyatumia ili kuboresha maisha yetu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…