Binadamu wa kwanza ni yupi? Wa Olduvai au Adam

Status
Not open for further replies.
Si kweli kuwa ni 6000. Is God controlled with our watch and timings kwamba kwake siku ni saa 24?
And creation is an ongoing processe ambayo for six days za kibinadamu yaani saa 24x6 haiwezekeni. I believe earth has been there for millions of years.

Which is all the more reason to see that the bible is mostly full of hogwash. Ukifuata vizazi vy biblia utaona dunia imeumbwa 4004 BC.

You simply cannot spin that.
 
If u would ask me this question, the answer would be ..kujua binadamu wa kwanza ni nani na ilikuwajekuwaje inabidi uwepo wakati wa kuumbwa huyo binadamu wa kwanza. Yaani inabidi u-observe hiyo event with your raw eye. Hivo basi binadamu wote hawaqualify kujibu hili swali objectively. Hivo hapa mnagombana na keyboard for a guaranteed FUTILITY.

Karibuni.
 
Hii habari ilishazungumzwa kabla na hii ni moja kati ya mchango mmojawapo

Kabla sijaingia katika mada hii, kwanza kabisa hatuna budi kuelewa kitu kimoja. Nacho ni elimu ya Sayansi (science). Baada ya hapo ndipo tutakuja kuangalia Nadharia ya Evolusheni (Evolution theory). Nadharia ambayo ni maarufu sana mashuleni na kwenye asasi za elimu.

Sayansi maana yake ni Elimu au ujuzi unaotokana na maarifa ya uchunguzi unao randana na majaribio na vipimo mbalimbali vya kinadharia na vitendo. Kwa maana hiyo basi elimu hii ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu tangu enzi za mwanzo kabisa za kuwepo kwake mwanadamu. Kwa maana hiyo kwa ufupi tunaweza kusema kuwa Elimu ya Sayansi ni ujuzi na maarifa ya kukabiliana na mazingira ya dunia yetu hii.

Kutokana na hayo basi ndio maana kukajitokeza wanasayansi mbalimbali wenye ujuzi wa kinadharia na vitendo. Miongoni mwao ni Bwana huyu mwenye uraia wa kiingereza ajulikanaye kwa jina la Charles Robert Darwin.

Kutokana na historia ya kimagharibi kutofautiana na imani za kidini, na maendeleo ya elimu mbali mbali za Sayansi, wanasayansi wengi ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafiti vitu mbalimbali katika elimu, wakajikuta wanatengwa na makasisi na watawa wa kidini hususani dini ya kikristo. Kwa kuelezwa kuwa wanakwenda nje ya imani ya kidini na wanakufuru Mungu. Kwa hali hiyo wakajikuta wanasayansi wengi wakiteswa ama kutengwa au wakiuwawa kwa sababu ya tafiti zao.

Na hali hiyo ikapelekea wanasayansi wengi wa kimagharibi kuwa na upeo mdogo sana au kutokuelewa kabisa elimu ya kumjua Muumba wao. Na hii si kwa matakwa yao bali ni kutokana na kutengwa na kanisa. Kutokana na kutengwa huko, wanasayansi wengi wakawa si wenye kujihusisha na wala hawakuihusisha elimu yao wala uvumbuzi wao na suala la kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Na ndio maana Ugiriki ya kalei (Ancient Greece), iliyokuwa na wanasayansi mbalimbali na kwa bahati mbaya ilikuwa na miungu wengi wa kuabudiwa, na hii ikapelekea wavumbuzi wengi kuwa (Atheism) makafiri wasio amini M'Mungu, kwani wengi wa wanasayansi hao hawakujua ni Mungu gani hasa wa kuabudiwa. Na huku ndipo kulikoanzishwa elimu hii ya nadharia ya evolusheni.

Elimu hii ilipokelewa na wanasayansi mbalimbali, mmoja wao ambaye ni maarufu sana ni huyu tuliyemtaja hapo juu Bwana Charles Robert Darwin. Mwanzilishi hasa ni mwanabailojia wa kifaransa ajulikanae kwa jina la Jean Baptiste Lamarck. Mwanabaiolojia huyu katika moja ya kazi zake, aliwahi kueleza kuwa Twiga anatokana na mnyama ajulikanaye kwa jina la Paa au Palahala. Paa huyu kutokana na tamaa zake za kutaka kula majani machanga yatokanayo na miti iliyo mirefu, akajikuta ni mwenye kujitahidi kurefusha shingo yake ili kufikia majani yaliyo nchani, jitihada zake hizo zikapelekea kizazi chake kidogo kidogo wakawa ni wenye kuwa na shingo ndefu. na hii ni baada ya miaka mingi sana kupita. (French biologist in his Zoological Philosophy 1809).

Mtetezi mwingine aliyefuatisha mawazo yake ni huyu Charles Robert Darwin. Na ndiye aliye iendeleza elimu hii ya evolusheni, mpaka kufikia hapa ilipo. Na imempatia umaarufu sana katika elimu za kimaumbile. Mwingereza huyu ambaye alitumia miaka takribani mitano, akikusanya masalia (Fossils) ya wanyama wa baharini na nchi kavu, na kuyafanyia utafiti mnamo miaka ya 1859. Akaandika kitabu kiitwacho Chimbuko la Viumbe. (The Origin of Species). Nadharia hii imekuwa maarufu sana na kupigiwa debe na wanasayansi mbalimbali, pamoja na wanasiasa wakishirikiana na vyombo vya habari vya kimagharibi na kufundishwa mashuleni. Katika kitabu chake hiki, mwananadharia huyu ameelezea chimbuko la viumbe mbalimbali akiwemo mwanadamu. Mwanadamu ambaye kwa mujibu wa utafiti wake, amemgawanya sehemu takribani nne. Yaani mwanadamu anatokana na Nasaba zipatazo nne nazo ni:

*Australopithecus Robustus (Zinjathropus), aina ya Manyani. Halafu akabadilika kuwa Homohabilis na baadaye kuwa Homoerectus na Mwisho kabisa ni huyu binadamu wa sasa ambaye anaitwa Homosapien. Na kabla ya kuwa Zinjathropus. Binadamu alitokea baharini kwa bahati nasibu. Alianzia na kiumbe mmoja dhaifu sana, aliyekuwa na chembe hai moja. Ambaye alipitia mabadiliko mengi na kwa miaka mingi sana. Kutoka kuwa kiumbe mwenye chembe hai moja na kuwa aina ya jamii ya Pweza na kubadilika kuwa jamii ya Chura na kisha kuwa jamii ya Mjusi na kuwa jamii ya Manyani kabla ya kubadilika kuwa binadamu huyu wa sasa. Na kutokana na mazingira aliyopitia yaani kwa kiingereza ni kutokana na Natural Selection kwa kiswaili ni uwezo wa wanyama kuishi ama kutoweka kwa mujibu wa uwezo wao wa kubadilika kufuatana au kulandana na mazingira.

*(Wataalamu wa kipindi hiki tulicho nacho, wamegundua kuwa Australopithecus au south Afriacan Ape, Homohabilis na Homoerectus ni viumbe ambavyo viliishi duniani kwa wakati mmoja lakini katika mazingira na maeneo tofauti hapa duniani).

Na isitoshe masalia ya Australopithecus au south Afriacan Ape yanaonyesha kuwa ni sokwe wa kawaida tu, na si vinginevyo. Utafiti huu ulisimamiwa na Lord Solly Zuckerman toka England na Prof. Charles Oxnard wa USA. Na hayo yote yametokea kwa bahati nasibu tu. Kwa maana hiyo basi binadamu huyu hawajibiki kwa yeyote yule isipokuwa kwake mwenyewe mtu binafsi. Na hapa ndipo wazimu mwingine mkubwa wa kutomjua Mwenyezi Mungu unapoanza. Kwani binadamu huyu kwa kukosa wa kumuogopa na kukosa mwongozo sahihi, ndio amejikuta akiingia katika matatizo mengi ya kijamii na kiutawala na ubinafsi wa hali ya juu sana. Kwani kila binadamu inabidi ajijali yeye binafsi na kufanya vile atakavyo.

Hebu na tuangalie nini hasa maana ya maneno haya Natural Selection na Mutation kwa mujibu wa U-Darwin (Darwinism).

Natural Selection: Kwa mujibu wa nadharia ya Darwin haya ni mabadiliko yanayotokana uwezo wa wanyama kuishi ama kutoweka kwa mujibu wa uwezo wao wa kubadilika kufuatana au kulandana na mazingira ya asili. Hali inavyokuwa ni kwamba linapotokea janga la kiasili kama vile ukame au mafuriko, kuna viumbe watakao himili misukosuko hiyo, na wapo watakaoshindwa kuimili misukosuko hiyo. Sasa wale watakao himili misukosuko hiyo, ndio hao watakaokuwa wamechaguliwa kuishi kwa mujibu wa Natural Selection.

Lakini hapa bado nadharia hii haielezei ni vipi Natural Selection inaweza kutoa viumbe vipya, kwani ikitokea kuwa kwa kiumbe mmoja kati ya wale waliofanikiwa kuishi katika misukosuko hiyo akakatika kidole au mguu bado kizazi chake kitakuwa ni kizazi kilicho kamilika viungo vyote vilivyo kamili, na wala haitatokea kuwa ni wenye kuzaliwa wakiwa na viungo visivyo timia. Yaani wawe ni wenye vidole pungufu au wawe ni wenye mguu mmoja mmoja, kama alivyo mzazi wao aliye tangulia. Au mfano rahisi ni vipi mafuriko na matetemeko ya ardhi yanaweza kujenga miji? Hii kwa kweli haikubaliki hata kidogo kwani siku zote majanga ya kiasili huleta uharibifu na si kutengeneza.

Mutation: Haya ni mawazo yaliyokuja baadae sana, ni pale watetezi wa nadharia hii ya Darwinism walipoona kuwa hawana hoja zenye nguvu na ushawishi wa kina kuhusiana na dhana nzima ya kile wanachokiamini kuwa hakina mashiko au ushahidi yakinifu (concrete evidence). Ndipo walipokutana kuangalia upya dhana hii. Mjerumani mmoja mwana paleontoolojia aitwae Otto Schindewolf katika miaka ya 1930 (German paleontologist in the 1930s). Alipokuja na dhana hii ya Mutation. Yeye anaamini kuwa mabadiliko ya gene ndio yanayoweza kuleta viumbe wapya. Na hapa ndipo yalipoletwa na kupigiwa mifano mingi tu na kuithibitisha mifano iliyotangulia. Mfano wao wanasema kuwa maisha yanatokana na vitu visivyo na uhai kama vile wadudu wanatokana na mabaki ya vyakula yalioachwa muda mrefu majalalani, na pia minyoo (Worms) wanatokana na nyama zilizo oza au panya wao asili yake ni masuke ya ngano. Mambo haya baadae katika majaribio yalio fanyika kwenye maabara ikagundulika kuwa dhana hizo zote si za kweli, kwani minyoo inatokana na nzi wanaokuja kula zile nyama huwa wanabeba lavae ambazo baada ya kurutubishwa ndipo wanapozaliwa minyoo. Vile vile mabadiliko haya wanayoyaita Mutation katika mwili wa kiumbe yeyote yule yanapotokea, siku zote huleta uharibifu katika Gene za kiumbe yeyote yule. Na hii ni kutokana na muundo wa DNA ulivyo kuwa mgumu kueleweka na kuelezeka kirahisi. Kwani inapotokea uharibifu wa aina yoyote ule katika Gene basi kitakacho patikana hapo ni kiumbe kisicho na uhai au maumbile yasio kamilika. Mfano waathirika wa bomu la atomic kule Nagasaki na Hiroshima Japan. Au walio na maradhi ya pepo punda, Saratani (Cancer) au wale wenye mtindio wa ubongo.

Kutokana na Nadharia hii kutokidhi haja ya wasomi, kwa kushindwa kwake kuelezea viumbe wengine wametokana na nini na kwa sababu gani. Ndio maana wasomi wa karne zetu hizi wameweza kugundua, vitu vingi ambavyo vinapingana na nadharia hii potofu. Na hii ni kutokana na Darwin mwenyewe kushindwa kuthibitisha nadharia yake mwenyewe. Pale aliposema, na nukuu. “…But I believe in Natural selection, not because I can prove in any single case, that it has changed one spicies into another, but because it groups and explains well (as it seems to me) the host of facts in classification, embryology, morphology, rudimentary organs geological succession and distribution...” Mwisho wa kunukuu.

(kwa tafsiri isiyo rasmi ana maana ya …“Lakini nina amini uteuzi wa kiasili (“natural selection”) sio kwamba naweza kuthibitisha japo jamii moja kwamba imebadilika kutoka hali moja hadi nyingine ila kwa sababu inagawanya na kueleza vizuri (kwa nionavyo mimi) ukweli wa mambo juu ya uainishaji, taaluma ya ukuaji wa mtoto tumboni, ufanyikaji na mgawanyiko wa miti na wanyama, viungo masalia na mabadiliko ya udongo na mawe na mchanganyiko wake…”).

Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki? Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza? Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji?
Qur’an 56:57-59

MAVUMBUZI MAPYA:
Hali hii inaonesha kuwa hata Darwin mwenyewe alikuwa na wasiwasi na hakuwa hakika na nadharia yake hiyo ya Evolution. Lakina alikuwa na matumaini kuwa ipo siku tatizo ili la kinadharia litakuja kugunduliwa, hapo sayansi itakapo pata wavumbuzi wapya. Tukichunguza kwa makini tutakuta kuwa wakati wao hawa kina Lamarck na Darwin sayansi ilikuwa bado ipo katika hali ya ujima (hali duni sana). Kwani hata vifaa walivyo tumia wakati wao vilikuwa duni sana, na elimu nyingi zilikuwa hazijagunduliwa bado. Mfano elimu ya Biochemistry, elimu ambayo inahusisha mambo ya kemia na maisha ya viumbe hai. Microbiology elimu inayo husu mambo ya viumbe hai vidogo vidogo. Na ndio maana ikawa rahisi kwao kudhani kuwa binadamu alitokea kwa bahati nasibu tu, na tena bila ya sababu yoyote ile. Kwani kwa wakati wao elimu inyouhusiana na mambo ya Genetic haikuwepo bado. Na hii ni kutokana na zana duni walizokuwa nazo wakati huo.

Soma Mwenyezi Mungu anasema nini kuhusu jambo ili.

Na miongoni mwa watu wapo wanao nunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha. Na (mtu kama huyo) anapo somewa Aya zetu huzipa mgongo kwa kujivuna, kama kwamba hakuzisikia, kama kwamba masikioni mwake mna uziwi. Basi mbashirie kuwa atapata adhabu chungu. Qur’an 31: 6-7

Wanasayansi wa wakati wetu huu, baada ya uchunguzi wa kina na huku wakisaidiwa na vifaa vilivyo bora kabisa, wameweza kuichunguza seli ya mwanadamu na za viumbe mbalimbali vilivyoko duniani, na kugundua mfumo wa ajabu kabisa katika maumbile ya seli hizo. Na ndani ya seli hizo wamegundua kuwa seli imegawanyika sehemu mbalimbali. Sehemu mojawapo muhimu sana inaitwa Cell Nucleus yani kiini cha seli. Katika kiini hicho kuna vitu viitwavyo Chromosome. Humo ndimo kunapatikana Gene. Chromosome hizo zina umbile la Nyuzi nyuzi zenye sehemu mbili, ambazo ni DNA (Deoxyribonucleic acid) na protini (Histamine). Protini zilizoko mwilini mwa wanyama ufanyika kutokana na kitu kinachoitwa Amino Acid. Na unapoitaja DNA hii ni kama benki inayohifadhi taarifa zote za kiumbe, kuanzia tabia mpaka ukuaji wa kiumbe huyo. Utakapotaka kuelezea DNA kwa ufupi basi humo ndimo zapatikana sifa zote za kiumbe hai. Katika DNA kuna vitu vingi sana kiasi unaweza kujaza kurasa million za vitabu na usimalize sifa zake. Hayo ni mavumbuzi ambayo wakati wa kina Darwin hayakuwepo na wala hawakuota kuyavumbua. Wataalamu wa sasa wanasema kuwa kutokea kwa kinasaba kimoja kwa bahati nasibu ni sawa na kuandika namba ya kimahesabu kwa namna hii 1/10x950. Namba hii ina maana kuwa 1 gawa kwa 1 yenye sifuri 950 mbele. Ambayo ni muhali kutokea kwa bahati nasibu, yaani kwa ufupi ni kitu kisicho wezekana. Kwa binadamu wa kawada tu nakadiriwa kuwa na seli zipatazo, trilioni mia moja. Na kwa maajabu ya udogo nusu kipenyo (Radius) cha Nucleus ni cm10 to the power of –12 (0.000000000001) cm. Na radius ya atom ni 10 to the power of -8 (0.00000001) yaani seli ni ndogo kuliko kichembe kimoja cha vumbi, yaani smaller than tiny dust.

Hapa sasa hebu na tuangalie kiungo kimojawapo cha mwanadamu, na maumbile yake na jinsi gani kilivyoumbwa kwa mpangilio wake wa ajabu. Kiungo hicho si kingine bali ni Jicho la mwanadamu. Jicho ni kiungo cha kuonea katika mwili wa mwanadamu. Jicho la mwanadamu huanza kuchukua umbo lake katika wiki ya sita, tangia mimba kutungwa, katika mji wa mimba, katika mpangilio wa ajabu kabisa, sehemu mbalimbali za seli huanza kugawanyika na kujitenga kwa maana ya kila eneo la jicho huanza kuchukua nafasi yake. Mfano baadhi ya seli hujiunda na kuwa konea, ambayo ni sehemu ya mbele ya jicho iliyo ngumu, na yenye kupitisha mwanga. Na nyingine huwa Pupil yaani mboni, na nyingine kuwa lensi ya jicho na nyingine hujitengeneza kuwa ute wa jicho na kadhalika. Jicho la mwanadamu lina sehemu zaidi ya arobaini na kila sehemu ina kazi yake maalum. Jicho ili ambalo imekamilika lina tabia ya kupitisha mwanga, na tena kwa kiwango maalumu, mwanga upitishwa mpaka kwenye retina ambayo ina sehemu zipatazo 11, sehemu iliyo maalum kwa kupokea mwanga, na kusafirishwa kiumeme kupitia katika seli mpaka sehemu ya nyuma ya ubongo inayoitwa tiny spot au centre of vision. Na huko utambuliwa kama picha. Lakini ni kitu cha ajabu sana hufanyika kwani hiyo sehemu inayoitwa tiny spot kuna kiza sana na mwanga hauruhusiwi kufika hapo, bali mwanga ukishabadilishwa kuwa katika hali ya kiumeme (electrical signal), ndipo huruhusiwa kufika huko. Kujitengeneza huku si kwa bahati nasibu bali ni kwa mpangilio ambao kama hauku kamilika basi jicho hilo litakuwa na hitilafu kubwa sana na usumbufu kwa mtu mwenye jicho hilo.

Vilevile tukiangalia macho ya wadudu mfano kereng’ende (Dragonfly) ni mdudu mwenye macho zaidi ya elfu na kila jicho lina lensi zipatazo elfu thelathini (30,000). Mdudu huyu wa ajabu mweye uwezo wa kuona takriban pande zote za Nyuzi 360, mabaki yake (fosil) yaligundulika hivi karibuni, baada ya kuchunguzwa yalionekana kuwa yana umri wa miaka milioni 50. Mdudu huyo hakuonyesha tofauti yoyote na Kereng’ende wa wakati huu tulionao. Kwa hali hiyo basi tunaweza kuona ni jinsi gani ni vigumu viumbe vyote hapa dunian vilivyo hai na visivyo hai kuwa haviwezi vikatokea tu kwa bahati nasibu. Yaani bila ya aliye vitengeneza. Wakati huo huo tunaamini kwa asilimia zaidi ya mia moja kuwa tunapo ona gari ikitembea barabarani au eroplane ikiruka angani basi kuna alie itengeneza na kuiwezesha kuruka.Je vipi kiumbe hai hususani mwanadamu ambaye anajitambua? Akika elimu hii ya Nadharia ya evolusheni itabakia katika mawazo ya wendawazimu wachache na kwenye vitabu vyao hao wasiomini kuwepo kwa Muumba na si kwa binadamu mwenye akili timamu.

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtenenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu Na ardhi kinamtakasa, naye Ni Mwenye kushinda, Mwenye hekima.
Qur’an 59:24

Huyu ndiye Mwenye kuyajua yasiyo onekana na yanayo onekana. Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. Ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu; na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo. Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji madhaifu. Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru.
Qur’an 32:6-9

Brother Yusuf Estes, ktk moja ya nakala zake alieleza mambo haya mawili kama yanaingia akilini:

What if someone called a 'scientist' tells you his 'theory' of how cars are made is like this:
A salvage yard on the south side of town blows up and all the metal pieces fly into the air and fall back down in one place forming a brand new Chevrolet Caprice automobile... with no left over parts… and the motor is running...


Or what if his theory for how a chair is made is:
An explosion occurs in a forest and the trees go flying into the air and then suddenly they combine with some flying cloth to make a beautiful chair... and then it lands in a furniture showroom complete with matching table and lamp...


Now the question is: "Are you really going to accept any of this as 'fact'?
 
If u would ask me this question, the answer would be ..kujua binadamu wa kwanza ni nani na ilikuwajekuwaje inabidi uwepo wakati wa kuumbwa huyo binadamu wa kwanza. Yaani inabidi u-observe hiyo event with your raw eye. Hivo basi binadamu wote hawaqualify kujibu hili swali objectively. Hivo hapa mnagombana na keyboard for a guaranteed FUTILITY.

Karibuni.

Kwa hiyo kujua kwamba Nyerere alikabidhiwa nchi ya Tanganyika na mkoloni wa Kiingereza 1961 ni lazima uwe ulikuwepo uwanja wa taifa umeshuhudia na raw eye (bila miwani wala darubini maana zinaweza kuwa zimewekewa majamboz ukaona kitu sicho) ?
 
Kwa hiyo kujua kwamba Nyerere alikabidhiwa nchi ya Tanganyika na mkoloni wa Kiingereza 1961 ni lazima uwe ulikuwepo uwanja wa taifa umeshuhudia na raw eye (bila miwani wala darubini maana zinaweza kuwa zimewekewa majamboz ukaona kitu sicho) ?

You probably didn't get the point ( as usual). Kuna mdau hapo alipin-point kabla kwamba ni vema ukajaribu kuelewa wanachoongea wengine kabla ya kuleta pathetic rebuttals zisizo na kichwa wala miguu.

Ninachoongea hapo ni ile topmost hierarchy ya kueza kujua ukweli kwa ukamilifu wa 100% kuhusu uwepo kitu au kutendeka kwa tukio. Ukishaondoka kwenye hiyo kukosekana kwa 'raw eye' ndio unakuja kwenye secondary sources ambazo funny enough zinalenga kwenye hizi subjectivity zenu humu. Ndio maana ya post yangu. Tayari mpaka hapo?
 
Siyo kweli! Namba zilizotumika kwenye Biblia zina maana zaidi ya kusema hiyo 6,000. Unakumbuka watu walimwuliza Yesu ndugu yako akikusoea unatakiwa umsamehe mara ngapi, naye akajibu hata 7X70 (490) kwani alimaanisha ukishafikisha hiyo idadi 490 usimsamehe tena nduguyo au alimaanisha msamehe mara nyingi iwezekanavyo? Jaribu kujifunza siyo tu kusoma Biblia bali pia fasihi na maudhui yake (language yake, numerical patterns, imagery na maana).

Hapo utaweza kuona kuwa namba zilizotumika zina maana yake. Kama kweli dunia iliumbwa miaka 6,000 iliyopita, nani aliyekuwepo kurikodi na alitumia nini. Na je, Mungu alikaa muda gani kabla ya kuumba dunia? Na je, ni kweli Biblia iko interested kutwambia dunia ilumbwa lini na wapi? Kama dunia iliumbwa miaka 6,000 iliyopita, ilianza kuumbwa wapi (sehemu gani)/continenti gani?
na kwa nyogenza. imeandikwa kwa mungu siku moja ni kama miaka elfu moja na miaka elfu moja ni kama siku moja. kwaiyo hiyo miaka 6000 pengine ni miaka 6000000
 
na kwa nyogenza. imeandikwa kwa mungu siku moja ni kama miaka elfu moja na miaka elfu moja ni kama siku moja. kwaiyo hiyo miaka 6000 pengine ni miaka 6000000

Which is even more of a reason for precise people who want to find precise answers not to look for them in the bible.

How can you work with a mathematical system that is based on a construct that purpots 1 = 1,000 . Are you people serious?
 
You probably didn't get the point ( as usual). Kuna mdau hapo alipin-point kabla kwamba ni vema ukajaribu kuelewa wanachoongea wengine kabla ya kuleta pathetic rebuttals zisizo na kichwa wala miguu.

Ninachoongea hapo ni ile topmost hierarchy ya kueza kujua ukweli kwa ukamilifu wa 100% kuhusu uwepo kitu au kutendeka kwa tukio. Ukishaondoka kwenye hiyo kukosekana kwa 'raw eye' ndio unakuja kwenye secondary sources ambazo funny enough zinalenga kwenye hizi subjectivity zenu humu. Ndio maana ya post yangu. Tayari mpaka hapo?

It's funny you are talking about 100%. 100% is just an idea, and like infinity, does not exist in the real world. It is like those asymptote graphs we used to draw in O level, they almost touch the line but not really.You can get as close to 100% as much as you like, but cannot attain 100%, the laws of physics took care of that.

There is nothing 100% sure in this world. I take that back, even nothing is not 100% sure, and at the risk of sounding circular, even the assertion "There is nothing 100% sure in this world" is not 100% sure . From DNA paternity tests, to a perfect vacuum, down to your very existence.It's not even like I am trying to flip some Immanuel Kant, Hegel and Karl Popper. Me trying that here. Picture that.

100% is against the known laws of physics, from the speed of light, the second law of thermodynamics down to the uncertainty in the nature of subatomic particles as described by Heisenberg.

You just have to choose your rational comfort level.Below 100%, that is.
 
You only live once, ukifa ndiyo mwisho wa mchezo, hamna pepo wala moto baada ya kifo. Pepo na moto tunaona hapahapa duniani.

Na wewe hii ya you only live once umeitoa wapi? Umejuaje kama kama hakuna pepo (upepo) wala moto baada kifo? Unless uniambie uliwahi kufa na hukukumbana na pepo wala moto hapo ndo ntaweza kukuelewa lakini kama huja experience kifo, huwezi kusema kwa mamlaka kuwa hakuna pepo wala moto baada ya kifo.
 
Na wewe hii ya you only live once umeitoa wapi? Umejuaje kama kama hakuna pepo (upepo) wala moto baada kifo? Unless uniambie uliwahi kufa na hukukumbana na pepo wala moto hapo ndo ntaweza kukuelewa lakini kama huja experience kifo, huwezi kusema kwa mamlaka kuwa hakuna pepo wala moto baada ya kifo.

Mimi mbona nafanya kitu less than kufa na kufufuka kila usiku. Nimeshasema there is nothing 100% sure, not even that statement is 100%, you just have to pick your comfort level. And 99% is pretty good for me.

And based on experience I can conclude that life ends at death with 99% satisfaction. I don't need 100% because I know 100% is unattainable under any circumstance on any question, from a strictly philosophical point of view, hata ningekufa na kufufuka ningeweza ku question kama experience yangu wakati nimekufa ni real au ni ndoto tu. Even the multiplication table is not 100% correct. So to be truthful we don't know that we know what we know, or rather, we don't know for sure that we know what we think we know. We can only tolerate a slimmer margin of errors.
 
Unafuatilia thread au unapenda kuandika tu?

The entire concept of binadamu, whose etimology is derived from Arabic Ibn-Adam, is fallacious.

Ha ha ha ha ha
Kiranga, umeniacha hoi leo. Straight away nikaanza kujiuliza, latin name ya binadamu ni nini vile (homo...whatever), kisha nikajiuliza na ile ya kwetu ya kibantu bantu nini vile... (ntu, mtu, mhno, bantu,... etc). You made me think!!
 
And based on experience I can conclude that life ends at death with 99% satisfaction.

Based on what experience?

So to be truthful we don't know that we know what we know, or rather, we don't know for sure that we know what we think we know. We can only tolerate a slimmer margin of errors.
Word.
 
Unafuatilia thread au unapenda kuandika tu?

The entire concept of binadamu, whose etimology is derived from Arabic Ibn-Adam, is fallacious.
Kuhusu Ibn adam, sidhani hata kama unaelewa maana yake... Swali langu jepesi sana, nimekuuliza binadamu wa kwanza kwa usomi wako ni yupi?
 
Kuhusu Ibn adam, sidhani hata kama unaelewa maana yake... Swali langu jepesi sana, nimekuuliza binadamu wa kwanza kwa usomi wako ni yupi?

The entire concept is a myth, binadamu is a misnomer.Soma juu hapo uone thread ilivyotiririka.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom