RayB
JF-Expert Member
- Nov 27, 2009
- 2,752
- 196
Hii ni hoja binafsi ambayo leo nataka kutafakari pamoja kati ya vitu hivi viwili vinavyochanganya. Napenda kuzungumzia kitu kinaitwa 'Binadamu wa kwanza'. Wakati vitabu vyetu vya dini vinatuambia kuwa binadamu wa ni Adam na akafatia Eve, lakini sayansi na hasa wale wana historia wanasema binadamu ni matokeo ya Evolution tukitokea kwa wanyama wenye asili ya sokwe na tena kwa kuongeza zaidi ni kuwa binadamu wa kwanza inaaminika kuwa alitokea Tanzania maeneo ya kule Olduvai.
Vitu hivi naamini vinakanganya na ni kila mmoja alishawahi kufikiria lakini hakuweza kuingia ndani zaidi na kujua lipi ni lipi. Tanzania waamini wa dini ni wengi kuliko wasioamini na zote zinaamini katika lile la kwanza lakini bado watu hao wanaitangaza Tanzania kuwa ni sehemu ya kutalii kwani moja ya vivutio vyake ni sehemu ile ambako binadamu wa kwanza anaaminika kuishi. Na sisi sote tumepitia katika masomo haya na tulikuwa tuaamini hivyo na kisha tukafaulu kweli na wewe muumini mzuri ulifurahia sana ulipofaulu somo hili tena ukapata vizuri sana lile swali lililouliza kuwa binadamu wa kwanza aliishi wapi? Je tulifanya makosa?
Naamini nitapata mawazo mbali mbali na changamoto nyingi katika hili pale tu mtakapotoa hofu ya kujiuliza tena hili swali