Binadamu ni katili sana R.I.P Chuga

ney kush

JF-Expert Member
Feb 16, 2012
1,373
851
Naam salam wana jukwaa.

Nalipanda jukwaa hili moja kwa moja kutoka Maji Chumvi hapa Jijini DAR ES SALAAM.

Juzi siku ya Jumapili mnamo saa tisa na nusu alfajiri, Mimi pamoja na ndugu yangu tulipata safari ya kupeleka
safety gears Ngere Ngere.

kuna Camp pale ya MAKABURU (wadutch kutoka south africa). Wanajenga uzio kwenye reli hii ya SGR kuzuia tembo (kuna tembo yale maeneo).

Tulifika pale camp then saa moja asubuhi tukafika sehemu ambayo
tulitakiwa tukutane na hao wazungu tuwape vitu vyao.

Sasa tulipofika hiyo sehemu ambayo ndio kazi mbali mbali hufanyika, kuna gate ambapo ndio tulitumia kuingia walinzi wa lile gate ni WAMASAI tulimkuta mmasai moja akatuandikisha tukaingia kuelekea sehemu ambayo tulitakiwa kukaa kuwasubiri hao maboss, hapo tulikuta walinzi WAWILI moja alikua macho mwingine alikua amelala bado.

Tukawa tunawasubiri wazungu waje, wakati tunasubiri hao wazungu , wafanyakazi wakaanza kuingia pia.

Tangu tumefika hapo yule mlinzi hatukua tumeongea nae chochote lakini walipofika wafanyakazi wakasalimiana na yule mlinzi , Yule mlinzi akawaambia "Chuga amefariki".

Chuga ni yule mlinzi mwingine ambaye amelala pale pembeni.

Hapo sasa ikabidi tumchek, Ni kweli Chuga alikua hapumui, amelala chali ,paji la uso wake likionekana limepigwa na kitu kizito maana mifupa ya fuvu ilikua imegawanyika, damu zimevuja na macho Yametobolewa. Simu yake iko pembeni yake nayo imeloa damu.

Nani kasababisha hiki kifo? maana pale hakuna kitu kilichoibiwa na wala ile sehem haionekani kuwa na mali za mtu kutamani kuiba, tuliosoma Cuba tukasema huyu ameuwawa na mtu ambaye walikua na Ugomvi.
Hatukujua nini hasa wamegombana na huyo muuaji lakini inaonekana ni kifo kilichotokana na ugomvi maana ule ni ukatili mnoo.

Yule mlinzi tukamuuliza umetoa taarifa hata kwa wenzio pale getini akasema HAJATOA (RED FLAG), Yani ukute maiti na usitoe taarifa kwa wenzio wa karibu?

Maboss wakapigiwa simu wakafika, polisi nao wakafika wakaondoka na yule mlinzi na wale maasai walikua wote usiku pale kwenye lindo.

Nimepigiwa simu sasa hivi kujulishwa kuwa YULE mlinzi mwenzake na CHUGA amekiri kutekeleza hayo MAUAJI YA KIKATILI sababu ikiwa ni SHILINGI ELFU MBILI MIA TANO(2500).

R.I.P CHUGA
stori zinasema jamaa alikua peace sana
mtu wa watu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom