Binadamu kuanza kuishi mars rasmi mwaka 2022

Secret Star

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2011
Posts
1,861
Reaction score
2,099
Mjasiriamali Elon Musk ametangaza mpango wake wa kuunda makao ya binadamu katika sayari ya Mirihi (Mars kwa Kiingereza),ingawa wanaotaka kunufaika watahitajika kulipa pesa nyingi. Tiketi ya kusafiri hadi kwenye sayari hiyo inakadiriwa kugharimu takriban $200,000.Bw Musk, aliyeanzisha kampuni ya kibinafsi ya usafiri wa anga za juu kwa jina SpaceX, alitangaza mpango huo katika kongamano la kimataifa la wataalamu wa anga za juu (IAC) mjini Guadalajara, Mexico, Jumanne. Mpango wake, unajumuisha mfumo wa usafiri ambao utaweza kusafirisha watu 100 hadi Mars, safari yote ikichukua siku 80. Baadaye, safari hiyo inatarajiwa kuchukua siku 30 pekee.Bw Musk amesema ili kufanikiwa na kuhakikisha gharama kwa kila mtu ni $200,000, basi lazima kuwe na njia ya kutumia tena mitambo ya uchukuzi itakayotumiwa. Bw Musk anataka binadamu wa kwanza waende Mars mwaka 2022 Amezungumzia mpango wa kuunda koloni ya watu milioni moja hivi ambao wataweza kujitosheleza na kusema mpango huo utachukua miaka 10 hivi kutimizwa.Ili kufikisha watu milioni moja, Bw Musk amsema: "Ninataka watu watazame kwamba ni jambo linalowezekana, jambo tunaloweza kutimiza katika uhai wetu ... na kwamba yeyote anaweza kwenda huko akitaka."Chini ya mpango wa SpaceX, safari ya kwanza ya kupeleka watu sayari hiyo itafanyika 2022.Chombo cha kwanza kupeleka watu Mars Bw Musk anataka kukiita The Heart of Gold, jina linalotokana na chombo kinachozungumziwa katika kitabu cha Douglas Adams The Hitchhiker's Guide to the Galaxy. Kitarushwa kutoka Kituo cha Anga za Juu cha Nasa cha Keneddy, sehemu 39, ambayo ndiyo sehemu iliyotumiwa kurusha roketi na vyombo vya anga za juu chini ya mpango wa Apollo. Itachukua miaka 100 kuwa na watu milioni moja sayari ya Mars Chombo cha kwanza cha kusafirisha watu kitafanyiwa majaribio katika kipindi cha miaka minne ijayo. Mwishoni mwa wiki, Bw Musk alitangaza kwamba majaribio ya kwanza ya roketi kwa jina Raptor ambayo itatumiwa kurusha chombo hicho pamoja na kifaa cha kuiweka kwenye mzunguko anga za juu (booster) yalifanyika.Tangi la mafuta ya kifaa hicho limeundwa na kufanyiwa majaribio na Bw Musk alionesha picha ya tangi hilo na wafanyakazi. Mwonekano wa mfano wa tangi hilo kwa ndani Mfumo wa kifaa hicho cha kuweka chombo cha anga za juu kwenye mzunguko wa sayari, pamoja na chombo chenyewe, kwa pamoja unafamika kama Mfumo wa Usafiri wa Sayari hadi Nyingine (ITC). Mitambo hiyo miwili kwa pamoja ina urefu wa mita 122, na inazidi mfumo wa Saturn V wa Apollo ambao ulitumiwa kwenda mwezini.ITS kubwa zitaweza kubeba hadi abiria 200. Bw Musk amesema injini ya Raptor imefanyiwa majaribio Texas Mjasiriamali huyo anapanga kwamba wakati wa safari hiyo ya siku 80, watu wataishi kwa pamoja na kutazama filamu, kuhudhuria mihadhara na kucheza michezo isiyoathiriwa wa mvutano wa sayari. Mpango wote utafadhiliwa na faida kutoka kwa SpaceX. Bw Musk anatazama mpango huo wa kupeleka watu Mars kuwa "ushirikiano mkubwa wa umma na sekta ya kibinafsi" na anasema "hivi ndivyo Marekani ilivyoanzishwa". Vyombo vya anga za juu vitatumwa kila baada ya miaka miwili Mars inapokuwa imekaribia sana dunia. Umbali kati ya sayari hizo mbili utakuwa kilomita 57.6 milioni mwaka 2018. Sayari hizo zinapokuwa mbali sana, huwa umbali kati yake ni kilomita 400 milioni. Miaka ya karibuni, umbali huo umepungua kufikia kilomita 100 milioni pekee. Mwanzilishi huyo wa SpaceX anataka kuwezesha binadamu kutalii "Mfumo wa Jua"Bw Musk anasema chini ya mpango wake, kunawezekana kuwa na vyombo 1,000 vikisafiri angani. Gharama ya kusafiri baadaye inaweza kushuka hadi kati ya $100,000 na $140,000. Mtu akitaka kurejea duniani, ataweza kufanya hivyo "bila malipo".
 
Attachments

  • 7860908-green-nature-in-the-morning-wallpaper.jpg
    7860908-green-nature-in-the-morning-wallpaper.jpg
    141.9 KB · Views: 82
  • mars_globes_wet_dry-1024x576.jpg
    mars_globes_wet_dry-1024x576.jpg
    23.7 KB · Views: 108
Huyo bwebwe tu Anajitangaza ila hamna lolote kwanza hakuna kiumbe hai kilichofika Mars kutokea duniani mpaka sasa ivi, NASA wenye ndo wanasafari ya kupeleka wanasayansi 2030 kwa ajili ya kuexploer hio sayari sasa huyo anaepiga porojo ana uhakika gani wa mtu kusurvive huko?
 
Haya mwanasayansi tumekusikia, watu hua mnabisha vitu ambavyo hata uhakika hamna, wala hujajisumbua kufanya research yoyote, Elon Musk sio mtu tu mropokaji, akiongea kitu hua anahakikisha anakifanya, alianzisha PayPal ikawa kampuni kubwa sana duniani, akaja akaanzisha SpaceX, ndiyo kampuni ya kwanza duniani kuweza kurusha re-usable rocket ikaruka na ikarudi, hili swala hata NASA hawajawahi fanya, ndiye aliyeanzisha Tesla Motors, kampuni inayoongoza kuuza electric vehicles duniani, kama umezisikia Tesla cars, gari very high quality na wanatoa charge bure sehemu nyingi marekani, unanunua mara moja unasahau mambo ya mafuta wala umeme. Na hii ya Mars japo mleta mada ameongeza chumvi kidogo kusema 2022, Elon hakusema 2022, alisema tu kua wanatengeneza rockets zitakazowezesha binadamu kwenda Mars, timeline aliyotoa alisema inaweza kua longer, kama kuna mtu anayeweza kurusha watu waende mars ni huyu jamaa.

We unavoongea utasema unajua hata properties za mars, unadhani hawa watu ni wajinga kua hawajalifikiria hilo? Hehehe! hua mna-underestimate scientists hasa hawa wenye akili kuliko mtu yeyote yule ukoo wenu mzima, ungekua umesoma engineering hata introduction tu ungejua kua mambo ya safety ni kitu kila mtu anajiuliza cha kwanza kabisa.
 
Mkuu mbona unaponda hoja zangu bila kuleta zako naona unasifu inshu za paypal na space X, Mimi nimesema mars hakuna kiumbe hai kilichofika na kama ni vyombo vipo tu vinachunguza na kutuma details rovers, Naelewa Hali ya mars ilivyo kuanzia Miezi yake phobos and demons gravity yake ni robo ya dunia,Mars iko karibu na dunia na Huitwa red planet kutokana na kuwa na rangi kuna details za ugunduzi wa uwepo wa maji japo haiko verified, Nasema ivi huyo jamaa kaongea tu hio 2022 ni kweli kasema hio habari niliona but sio rahsi ivo, Mars itakuwa karibu na dunia 2030 ni kama zitapishana hapo ndio plane ya Nasa kupeleka Astronouts,Cosmologist na astromer kuichunguza
 
Hakuna kiumbe kilichofika kwa sababu hatujawahi kutuma kiumbe chochote kule, mbona mwezini kulikua hamna kiumbe ambacho kimefika ila tulikua wa kwanza kutua? Kinachotuzuia mars kwenda ni nini? technology ikiwepo watu wataenda tu, hata technology ya kwenda nje ya solar system ingekuwepo tungeenda tu, ndio binadamu tulivyo, curiosity haiwezi ikaisha hata siku moja, scientists sio kama watu ambao wamejifunga kwenye dini kiasi kwamba wanahisi kutoka nje ya dunia ni nje ya maagizo ya Mungu. Tukiwa wazima ndani ya miaka 50 ijayo tutakua tumeshatua Mars subiri utaona, na kama sio SpaceX basi mwingine atafanya tu. Hata leo hii uwezekano wa kwenda Mars upo kwa atakayetaka sema technology ya sasa ni ghali mno hakuna mtu anayeweza kulipia, na kwa sasa hivi ni one way hakuna kurudi ndio maana no one is ready to take that risk.
 
Hakuna kiumbe kilichofika kwa sababu hatujawahi kutuma kiumbe chochote kule, mbona mwezini kulikua hamna kiumbe ambacho kimefika ila tulikua wa kwanza kutua? Kinachotuzuia mars kwenda ni nini? technology ikiwepo watu wataenda tu, hata technology ya kwenda nje ya solar system ingekuwepo tungeenda tu, ndio binadamu tulivyo, curiosity haiwezi ikaisha hata siku moja, scientists sio kama watu ambao wamejifunga kwenye dini kiasi kwamba wanahisi kutoka nje ya dunia ni nje ya maagizo ya Mungu. Tukiwa wazima ndani ya miaka 50 ijayo tutakua tumeshatua Mars subiri utaona, na kama sio SpaceX basi mwingine atafanya tu.
Mkuu Kwanza niseme sio kuwa hatujaamua kutuma kiumbe ni kuwa hakuna uhakika wa usafiri wa kutuhakikishia usalama wa kutua mar na kuondoka kurejea dunia so bado technology yakusafiri na kurudi haipo kabisa ipo ya kwenda tu nayo ni kwa vyombo ambavyo vikimaliza kazi hulipuka Natamani kuchimba zaidi kwanini hakuna uhakika wa go and return ila sina uhakika kama nikitumia technical language utanielewa...Pili hakuna kiumbe kilichotua mwezini na kurejea dunia Neil Armstrong 1969 hakutua mwezini ile ilikuwa cold war ya Russia na United state yani walikuwa wanatambiana tu na Us aliamua kufake moon landing na mchezo wote ulimalizikia Area 51 Nevada, Kwanini nasema Us haikupeleka mtu mwezini clips za sehemu wanazodai ni mwezeni zina full mapunguzu kama umecheki bendera inapepea ile hali ktk mwezi hakuna atmosphere ni vacuum pili helmet ya Armstrong ili reflect kopa la Pepsi pia reflection za miale mbali mbali zilionekana ni mchezo wa kuigiza tu Hebu waza america waende mwezini 1969 mpaka leo wasiende tena ile hali tech imekuwa advance mara tatu ya miaka io wanaenda, Note science inatanuka na mimi ni mwanasayans natambua ipo siku mwanadamu atatoka kabisa nje ya solar system its matter of time tu, Mambo ya kutamba sasa ile hali technology bado haijakuwa enough kuarchieve ni imagination tu ,Kuwa na imagination ni mwanzo mzuri mana thought(mawazo) ndio huunda kitu(Touchable)
 
Hehe unasema ukitumia technical language sitokuelewa! em jaribu tuone, nimesoma engineering, najua physics vizuri tu, em tumia hiyo technical language tuone.

Mwezini binadamu tuligusa, utake usitake, nimeshajua nabishana na mtu ambaye anaamini conspiracy theories zilizopo mtandaoni, nyie jamaa hua mnapumzikia sana maana mnajifanya mnajua sana sayansi ya kusomasoma kwenye viwebsite vinavyotungwa na wapiga hela. Leo hii kuna telescopes za kuweza kuona mwezini, kuna rovers pia mwezini, hata picha za footprints zipo, mwisho wa siku utakuja kusema zile footprints zimewekwa na rovers ili kutudanganya. Hehehe Area 51 bs.

We sio mwanasayansi, unatudanganya tu, sayansi ipi uliyosoma ya middle school? Mtu aliyesoma science angalau university level hawezi kuja na conspiracy theories ambazo hazina any evidence zaidi ya photoshopped photos.

Alafu hivi unachobisha ni kipi? maana nimesema technology haipo ya kwenda na kurudi na wewe unasema haijakua enough, hapo unaona kuna utofauti gani?
 
Mkuu hata mimi nimesoma engineering na ni mhandisi sasa sijui unataka kujitapa nini au unataka tubishane field za uhandisi najua ww Ni mtu Wa CS ...field yangu mimi ndo imezaa hio CS back to the topic nipe evidence sasa kuwa American astronomer kuwa wali land on moon mimi nimekupa ushahidi kidogo tu juu lete wako sasa, Ivi unafanya mchezo kitu kutoka mwezini kirudi duniani? Hio source ya Energy itakayopaisha chombo na kukipa Escape velocity kuaicha mwezi ni nini? Mana kwenda gravity pulls hukipa energy chombo ivo kutumia less fuel, chombo kikiondoka duniani hutumia energy kubwa kufikia 11 Km per second ili ki escape Gravity ya dunia kikiwa huko angani no air resistance fuel kidogo hukibust na kukipa extremely speed, Sasa niambie Tu escape velocity ya mwezini ukishatua hapo unai escape vp hio gravity mpaka urudi salama Duniani?
 
Hehe naona umeenda hadi kufungua profile yangu, sijasema nataka kubishana na wewe kuhusu tulichosoma, wewe ulisema una technical language kua ukiongea sitoielewa, nikakwambia nitaielewa vizuri tu maan hata mimi ni engineer, sasa unasema najidai kitu gani? angalia hata kiingereza unachoandika "extremely speed" ndio kitu gani?

Unasema umenipa ushahidi, hehehe umenipa ushahidi upi?
Yaani hata escape velocity huielewi? we jamaa unanipumzikia, naomba uende usome upya physics, alafu soma vizuri lunar module ya apollo ujue ilivyotengenezwa na walifanya nini kuescape kutoka mwezini, escape velocity ya mwezini ndiyo evidence yako? 2.4km/s? hehehe

Jamaa nenda google tusipotezeane muda, hii ndiyo message ya mwisho ninakujibu, sina muda wa kupoteza na watu ignorant wanaojifanya wanajua.
 
Ngoja nikuache mkuu Umesoma physcis advance tu tena theoretically Mimi nimepiga Applied Physics na bado naifanyia kazi,Naona unajitapa tu tangu awali ndio imebidi nikuambie mimi pia muhansishi tena wa core not subfield
 
Hehe naona umeenda hadi kufungua profile yangu, sijasema nataka kubishana na wewe kuhusu tulichosoma, wewe ulisema una technical language kua ukiongea sitoielewa, nikakwambia nitaielewa vizuri tu maan hata mimi ni engineer, sasa unasema najidai kitu gani? angalia hata kiingereza unachoandika "extremely speed" ndio kitu gani?

Unasema umenipa ushahidi, hehehe umenipa ushahidi upi?
Yaani hata escape velocity huielewi? we jamaa unanipumzikia, naomba uende usome upya physics, alafu soma vizuri lunar module ya apollo ujue ilivyotengenezwa na walifanya nini kuescape kutoka mwezini, escape velocity ya mwezini ndiyo evidence yako? 2.4km/s? hehehe

Jamaa nenda google tusipotezeane muda, hii ndiyo message ya mwisho ninakujibu, sina muda wa kupoteza na watu ignorant wanaojifanya wanajua.
Huwa sipendi watu wanaojitapa kama wewe halafu kwenye kutekeleza ni mizigo na hamna msaada wowote kwenye taifa hili zaidi ya mayowe mengi yasiyo na chembe ya aibu
 
We naye umetokea wapi? huna kazi?
 
Nyinyi wahandisi mnaobishana na kupeana kejeli kwenye huu uzi kuna michango chanya mmetoa kwa serikali yetu katika kuleta maendeleo na kukuza pato la taifa
 
Hawa wahandisi wanafanyaga nini wakati deal zote zinaenda kwa wageni wao wanaishia kubishana tu ns kukosoana
 
Mkuu hata mimi nimesoma engineering na ni mhandisi sasa sijui unataka kujitapa nini au unataka tubishane field za uhandisi najua ww Ni mtu Wa CS ...field yangu mimi ndo imezaa hio CS back to the topic nipe evidence sasa kuwa American astronomer kuwa wali land on moon mimi nimekupa ushahidi kidogo tu juu lete wako sasa, Ivi unafanya mchezo kitu kutoka mwezini kirudi duniani? Hio source ya Energy itakayopaisha chombo na kukipa Escape velocity kuaicha mwezi ni nini? Mana kwenda gravity pulls hukipa energy chombo ivo kutumia less fuel, chombo kikiondoka duniani hutumia energy kubwa kufikia 11 Km per second ili ki escape Gravity ya dunia kikiwa huko angani no air resistance fuel kidogo hukibust na kukipa extremely speed, Sasa niambie Tu escape velocity ya mwezini ukishatua hapo unai escape vp hio gravity mpaka urudi salama Duniani?
Mwezin kuna gravity sawa na duniani kwani?[emoji2] [emoji2]
 
Back
Top Bottom