Binadamu katoka wapi?

Profesa ntare nkobe

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2018
Posts
6,955
Reaction score
8,144
Katika nadhalia ya Dini kwamba binadamu katokana na Adam na Hawa hii haingii hakilini kwangu kwanini kuwepo matabaka ya rangi na kuwepo na jamii tofauti kwanini tusiwe wa rangi moja kama ni weupe au uweusi haiwezekani mzungu akazaa mtoto mweusi au Mwafrika azae mtoto mzungu.

Nadhalia ya pili kwamba binadamu katokana mabadiliko ya kimaumbile hii ina mashiko kiasi kikubwa nikichukua ushahidi wa fuvu la kale pale Olduvai gorge ni wazi binadamu kapitia katika hatua mbali mbali mpaka kuwa binadamu kamili..
 
Jibu maswali haya kwanza :
1.Je tunda lililoiva mtini likadondoka lisipookotwa linaoza na katika kuoza huko hutokea wadudu (funza) sasa Je wale funza walioozesha lile tunda wametokea wapi?
2.Je funza waliotokea na wakati embe ikioza ni sawa na wale waliotekezea kwenye papai,nanasi,pera n.k?
3.Kutokana na tofauti ya hali ya hewa katika maeneo mbalimbali ya dunia.. Je miti ya matunda yaliyopo Africa ni sawa na miti iliyoko Ulaya na Asia?

Ukijibu maswali haya utagundua chanzo cha utofauti uliopo.. Hatua za mabadilko ya binadamu ni ya kila aina ikiwa ni pamoja na wanyama na viumbe wengine wote.
 
Hata hiyo nadharia unayoijua wewe ya Evolution ya moja kwa moja imeshakatiliwa siku nyingi na wanasayansi. Mara kuna fuvu limegunduliwa Morroco sijui China etc. Lakini wanasayansi wengi bado wanaamini binadamu au tuseme genus yetu ya Homo ilianzia Afrika.
Kiufupi hakuna anayejua kwa uhakika binadamu alipotokea mpaka kufikia hapa.
And we may never definitely know.
 
Na kwa kuongezea,
Hapo kale kulikuwa na species nyingi za homo na wakati Homo sapiens akitokea ali co exist pamoja na species nyingine kama neanderthals huko Ulaya. Kwa ufupi zamani kulikuwa na species nyingi sana za binadamu.
Presently kuna species moja tu ya binadamu duniani kote ambayo ni Sapiens. Hizo species nyingine zilivyotoweka kabisa kwenye uso wa dunia mimi na wewe hatufahamu. Hakuna anayefahamu.
 
Aisee! Hii mpya kwangu.
 
anza kufuga kuku wawili jike na dume
vifaranga vitakupa majibu.
 
Duh! Yapi hayo tena?
Inaelezwa na wanasayansi kuwa binadamu wote tuliopo sasa hivi tumetokea kwa mtu mmoja aliyeishi somewhere around 300 BC maeneo ya East Asia.
Kwa vingine vingi zaidi kasome kitabu kinaitwa A Brief History of Everyone Who Ever Lived by Andrew Rutherford na Sapiens cha Harari.
 
Binadamu ndiye shetani, aliyefukuzwa huko mbinguni, ila kwa ubishi na kujitetea hakuna apendaye na kukubali yeye kuwa ni shetani.
Tumekuwa kama watoto akifanya kosa hutafuta visingizio, hakuna historia ya kweli ni visingizio. Tukubali sisi ndiye kizazi cha LUCIFER.
 
Ebu fafanua walau kwa kiasi flani wapate kukuelewa nami niongeze kitu katika hichi ulichosema..
 
Ongezea tu mkuu nitakuja natafuta mkate hapa kwa sasa.
Imeandikwa mtu hataishi kwa mkate tu bali hata maarifa ni chakula cha akili na roho so ukishapata huo mkate ntakusubiria uje uwaelezee kile ulichojifunza then ntarudi ku add nachokijua juu ya hilo
 
Ebu fafanua walau kwa kiasi flani wapate kukuelewa nami niongeze kitu katika hichi ulichosema..
Mungu alitufukuza kule Eden kwasababu ya curiosity yetu, kutaka kujua kila kitu hadi tupitiliza. Tukaanza kumtengeneza shetani ili tumpe maovu yetu, sisi hatutaki kuukubali ukweli na ni nature yetu kujitetea kwa kutafuta wa kumlaumu, tuko hivyo. Tunajua na kuweza kutenda kila kiovu humu duniani lakini hatutaki kuukubali ushetani. Tunasema Mungu alimfukuza shetani mbinguni na akamtupa duniani, tunamuona shetani duniani lakini tunajidai hatumuoni MWANADAMU/SHETANI. Ikiwa dunia haikuwa makao yetu ya asili tuliletwa huku baada ya kukithiri kwa uovu wetu, kwanini hatutaki kukubali ushetani wetu. Huko tulikukuwa tukiishi awali anaishi nani sasa, mfungwa wa maisha huwa anasimulia uovu wake wa awali akiwa gerezani,anasimilia ya nje au uraiani,anatanani asamehewe arudi uraiani, je sisi tunatofauti gani na mfungwa wa maisha kusimulia uzuri wa peponi tukiwa duniani?! Tunasimulia uzuri wa Mungu huko aliko tukiwa duniani, tunatamani tupate msamaha tukaishi kule kwa zamani lakini Mungu hajatusamehe tutaishia huku duniani, pepo hatutaiona tena. Sio kukata tamaa huo ndio ukweli, haya maisha tunajifariji tu lakini huo nadhani ndio ukweli.
 
Kwaiyo mkuu una maana Mungu kawatelekeza huku duniani au sio..!?
 
ni wanyama tulio pandikizwa kutoka katika utawala wa lyrans humanoids,...
Hao jamaa japo sifahamu majina yao halisi ila nina hakika ndio waletao kizungumkuti cha dini na maarifa mengi

Ndio waanzilishi wa dini za kiabrahamu nikiwa na maana ya uyahudi,ukristo na uislamu

Vitabu vya dini hizo ukivisoma bila wenge la kutafsiriwa maana na wanaojiita marabi unatoka na bonge la picha

Tena ukienda kuongezea na vedas za kihindu bila kusahau Tao teaching lazima uwe Guru
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…