Binadamu hafi, bado mnabisha tu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Binadamu hafi, bado mnabisha tu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtambuzi, Aug 21, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hivi karibuni mwanasayansi mmoja nchini India, amekiri kwamba binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena na kupewa mwili mwingine . Hii ina maana kwamba, sisi pia tumeshawahi kuishi huko nyuma kabla hatujafa na kurejea tena tukiwa na miili mipya, tuliyo nayo hivi sasa.
  Mwanasayansi huyu Vikram Raj Singh Chauhan, amesema ana uhakika ataweza kuthibitisha hilo baada ya kukutana na mtoto wa umri wa miaka sita ambaye anakumbuka maisha yake ya nyuma kwa kiwango kikubwa sana. Mtoto huyo wa kiume, Taranjijt Singh anasema aliwahi kuishi miaka michache nyuma, ambapo alifariki kwa ajali ya pikipiki akiwa bado mdogo.


  Mtoto huyo akiwa na umri wa miaka miwili alianza kusema kuhusu maisa yake ya nyuma na alikuwa akitoroka sana nyumbani . Alikuwa akiwaambia wazazi wake kwamba anakumbuka kijiji alichokuwa akiishi na hata jina la shule aliyokuwa akisoma.


  Alikumbuka pia jina la baba yake wa zamani {kabla hajafa}. Awali ilionekana kama aina fulani ya kisirani cha mtoto, lakini ilibidi wazazi wake waanze kuwa na wasiwasi kwa kadiri alivyokuwa akiongezeka kiumri.

  Mtoto huyo alikumbuka pia siku aliyokufa . Aliwaambia wazazi wake kwamba, alikufa September 10,992. Alikufa baada ya kugongwa na pikipiki wakati akiwa kwenye baiskeli akiwa anakwenda shuleni asubuhi. Baada ya ajali hiyo alipata majeraha kichwani na alifariki siku ya pili baada ya ajali.

  Baba yake wa sasa hivi, Ranjit Singh, anasema, mtoto wake alipozidi kusisitiza kuhusu maisha yake ya zamani, waliamua na mkewe kumpeleka huko kijijini anakodai kwamba, ndiko alikoishi kabla hajafa. Awali hawakuweza kumpata mtu ambaye alikuwa anafanana na maelezo ya mtoto huyu. Mkazi mmoja wa kijiji hicho aliwaomba waende kijiji cha jirani kinachofuata.

  Kwenye kijiji hicho walikwenda kwenye shule ya kijiji ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo alithibitisha kamba, September 10, 1992 alikufa mwanafunzi wa shule hiyo kwa ajali ya pikipiki. Kupitia shuleni hapo, walibaini mahali wazazi wa mtoto yule aliyekufa kwa ajali ya pikipiki, walipokuwa wakiishi.

  Ni kweli waliwakuta wazazi ambao walithibitisha kufiwa na mtoto katika tarehe na njia iliyoelezwa. Baba wa sasa wa mtoto huyu, Tanjit Singh alieleza kwamba, mtoto wao aliwaambia kwamba madaftari aliyokuwa nayo wakati wa ajali yalilowa damu baada ya ajali ile na alitaja kiwango cha fedha ambazo zilikuwa kwenye mkoba wake a shule.

  Mama wa zamani wa mtoto huyu ambaye kwa maana hiyo ni mama wa mtoto aliyefariki mwaka 1992 aliposikia hivyo aliangua kilio kikubwa , kwani maelezo hayo yalikuwa sahihi bila doa la kosa. Alisema vitabu na fedha hizo bado vipo, kwani aliviweka kwa kumbukumbu ya kifo cha mwanaye .

  Baadae mtoto huyu alirudi na wazazi wake wa sasa nyumbani kukiwa na maswali yasiyo na majibu. Wazazi wake wa zamani pamoja na ndugu zake, walikwenda kumtembelea kwao baadae. Mtoto huyu aliibaini picha ya siku ya ndoa ya wazazi wake, ambayo walikuja nayo wakati walipokwenda kumtembelea kwa wazazi wake wapya.

  Awali mwanasayansi, Vikram Chauhan, alikataa kukubaliana na maelezo kuhusu mtoto huyu , lakini baadae alijipa moyo wa kuanza uchunguzi. Alitembelea vijiji vyote viwili , cha zamani alikozaliwa na kufa na hiki cha sasa alipozaliwa.

  Alizungumza na wazazi wote na kupata maelezo ambayo yalimfanya kuona kuna jambo la maana kuhusiana na kifo na ‘kufufuka' kwa mtoto huyu. Kwenye kijiji alichozaliwa na kufa mtoto huyu, muuza duka mmoja alikiri kwamba ni kweli , mtoto kama huyo alikuwepo na yeye alimkopesha madaftari jana yake na alipogongwa alikuwa akielekea dukani kwake kumlipa madaftari hayo.

  Chauhan alichukua sampuli ya mwandiko wa mtoto huyu na ule wa kwenye madaftari ya marehemu. Ilipokwenda kupimwa na wataalamu wa mwandiko, ilibainika kwamba, ilikuwa ni ya mtu mmoja.
  Kumbuka kwamba mwandiko wangu hauwezi kuwa sawa na wa mtu yeyote, kama ilivyo alama za vidole. Kila mwandiko una sifa zake maalum ambazo haziwezi kupatikana kwenye mwandiko wa mtu mwingine.

  Wataalamu wana uwezo wa kubaini mwandiko wa kughushi hata kama umefanywa na mtaalamu wa kiasi gani wa kughushi miandiko.
  Kubwa zaidi ni kwamba mtoto huyu ambaye alishaanza kusoma kwenye maisha yake ya kabla ya kifo, hivi sasa hajapelekwa shule, kwa sababu familia yake ya sasa ni maskini. Hata hivyo katika jambo la kushangaza zaidi alipotakiwa kuandika alifabeti za kiingereza na ki-punjabi aliweza kufanya hivyo bila tatizo. Kama hajasoma ingewezekana vipi kufanya hivyo? Anatumia akili ya zamani ya kabla hajafa.

  Familia yake ya zamani imeomba kukabidhiwa mtoto wao, lakini familia yake ya sasa imesema hapana, huyo ni mtoto wao. Kisheria, bila shaka, familia yake ya sasa ambayo ni maskini sana, wakati ile ya zamani ilikuwa na uwezo, ndiyo yenye uhalali wa kuishi na mtoto huyu.

  Huenda baada ya sayansi kuthibitisha kwamba watu hufa na baadae kurudi wakiwa wanamiliki miilia tofauti, familia kama hii ya zamani ya mtoto huyu, ndipo itakapoweza kupata haki.

  Hata hivyo, bila shaka kila familia kati ya hizo mbili, itakayoishi naye, itakuwa na mashaka ya aina fulani.

  Mwanasayansi kama Chauhan na wengine wanaamni kwamba, kama roho ikihama kutoka mwili mmoja na kwenda mwili mwingine, huenda huko na akili au mawazo na hisia pia. Kinachoachwa ni mwili unaoonekana, lakini hiyo miili mingine huwa pamoja. Hii ina maana kwamba, hata mwandiko utabaki kuwa uleule kama ilivyokuwa.
  Chauhan anasema, hivi sasa anao ushahidi wa kisayansi kuthibitisha kwamba, binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena, lakini hutumia mwili mwingine. Hata hivyo anasema anahitaji muda zaidi kuthibitisha jambo hili.

  Bila shaka, ushahidi wa wazi kabisa kuhusu watoto hawa wa indigo, unaweza kutuonesha kwamba, tunapokufa, maana yake tumepoteza mwili , lakini bado hisia, akili, na roho ambavyo huja kuingia kwenye mwili mwingine ambao utatengenezwa na wazazi wengine wawili au wale wale, vinakuwepo.

  Ni vigumu kupingana na maelezo ya mtoto huyu, ambaye tangu akiwa na umri wa miaka miwili, alikuwa akizungumzia kuhusu kumbukumbu alizonazo juu ya maisha yake ya nyuma. Ugumu wa kupinga unatokana na ukweli kwamba, hatimaye maelezo yake yalithibitika.
  Kama ingekuwa Chauhan sio mwanasayansi, tungeweza kusema, suala hili bado, halijatazamwa kisayansi na hivyo, haliwezi kuelezewa kama jambo halisi.

  Kwa mwanasayansi kuvutiwa na jambo hili na kuanza kulifanyia utafiti huku akikiri kwamba, kuna mambo yenye kutanza, ni hatua kubwa katika binadamu kuingia mahali ambapo atabaini ukweli wa kuwepo maisha baada ya kifo.

  Lakini sio maisha baada ya kifo peke yake bali pia kukubali kwamba huenda binadamu ataendelea kuwepo, kwa sababu uwepo {being} haujapotea na hauwezi kupotea. Mwili wako utaharibika, lakini uwepo wa binadamu hauwezi kupotea.
   
 2. M

  MWENDAKULIMA JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2011
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 961
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Maswali ni mengi kuliko majibu.Kwa nini population inaongezeka? Sayansi inaweza kutoa majibu ya maisha ya kiroho pamoja na kimwili?kama ndiyo yale ya kiroho tunapataje uthibitisho?ni kwanini ni huyu mtoto tu na siyo wengine wengi?au huo mzunguko wa maisha(kufa na kuzaliwa tena) umeanzia kwake?
   
 3. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hekaya za Abunuasi ndio hizi. Wote huu ni uongo mweupeee usio na doa. Siamini kama kweli huyo ni Mwanasayansi otherwise kama ni witchdoctor. Mwanasayansi gani hajui child development psychology? Kama anaijua kutokana na science basi he must face skeptism. Ugunduzi wa kisayansi sio suala la mtu mmoja bali jopo na huchukua muda. Kama ni imani yake atajiju! Lakini ukifa it's over,na utasubiri ufufuo siku ya kiama tu.
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Aug 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [FONT=&quot]Kwa zaidi ya miongo miwili sasa, wanasayansi wamekuwa wakijitahidi kutafuta jibu la swali la, je binadamu anaendelea kuishi baada ya kupoteza mwili wake? Kuna wanaoonesha kwamba wanakubaliana na hilo na kuna wale ambao wanasema huenda hakuna kitu kama hicho.
  Kwa mfano kuna wale wanasayansi ambao wanakiri kwamba, watoto wanaofahamika kwa jina la Indigo, ni watoto ambao wana akili kubwa kuliko zile za binadamu wa kawaida. Tafiti zinaonesha kwamba, watoto hawa walianza kuzaliwa hapa duniani kuanzia mwaka 1975. Ni watoto ambao uwezo wao katika kuelewa mamabo ni mkubwa kuliko tulivyozoea kuona.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Baadhi ya watoto hawa, kutokana na uwezo mkubwa, wamekuwa wakikumbuka maisha yao ya nyuma, kabla hawajafa. Watoto hao wamekuwa wakisema waliishi zamani sana na kufa au kupoteza miili yao na kuja tena kuzaliwa mahali pengine.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Hakuna idadi maalum ya watoto hawa hapa duniani, lakini inadaiwa kwamba, wako wengi kiasi cha kufikia elfu kadhaa. Wanatofautiana pia kiuelewa, wengine wakiwa na kumbukumbu kali na uwezo mkubwa sana kiakili, kuliko wengine, ingawa wote wana ufahamu wa kiajabu.
  Kwa nini wameanza kuzaliwa miaka ya 1975? Kuna nadharia nyingi zenye kujibu swali hilo. Moja kubwa ni ile inayohusisha ukuaji wa dunia na ulmwengu kwa ujumla. Kwamba itafika mahali, maarifa mengi yaliyojificha yataibuliwa. Kizazi cha watoto hawa kinadaiwa kwamba, kimekuja kumwonesha binadamu kwamba, amekuwa akiuchukulia ulimwengu na maisha, ndivyo sivyo.[/FONT]
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyo mtoto amekuwa possessed na majinni yalio m possess yule aliyefariki kwanza , Simpo, Hakuna sayansi hapo.

  Wahindi wanajitahidi kila njia kuikomalia itikadi yao ya "caste". Na huyo mtoto utaambiwa amezaliwa katika familia ya kimaskini zaidi ya aliyokuwa akiishi kwanza kama ni adhabu ya kutoroka-toroka nyumbani, angekuwa hatoroki angezaliwa familia ya kitajiri. Hapo sasa.
   
 6. m

  mbweta JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 600
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Yan shetan yupo bize ku rationalize vp ambavo watu waamin mfano ukifa unazaliwa upya kumbe ni hukumu 2 inafwata. Au Mtu akifa hata kwa wizi mtasikia mapenzi ya mungu ipo haja tuwe tunasema mapenzi ya shetani.
   
 7. String Theorist

  String Theorist JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Biblia inatambua mahali pamoja tu walipo wafu wote. biblia haitofa,utishi mahali walip watakatifu waliokafa na pale walipo waovuwalio kufa. na mahali hapa panaitwa "SHEOL"(Kiebrania kwenye agano la kale) na "hades"(kwa kiyunani kwenye agano jipya) yote yana maana moja, yaani KUZIMU. swali huyu mtoto kama anavyo dai, hakupitia kuzimu??.
   
 8. String Theorist

  String Theorist JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Vipi kuhusu hii "Kwasababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote ,wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu laolimesahauliwa. == MHUBIRI 9:5-...
   
 9. String Theorist

  String Theorist JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  MBONA HAKO KAUTAFITI KANAPINGANA NA HAYA MANENO? "...kwa maana saa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale walio fanya mema kwa ufufuo wa uzima. ==YOHANA 5:28-29"
   
 10. String Theorist

  String Theorist JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nimekumbua story moja inayo onesha kuwa mwaka alio kufa Galileo Galilei ndio mwaka aliozaliwa Isaack Newton
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Ooohphuuuuu. Well, hivi nyerere atazaliwa lini?, bora arudi haraka maana nchi haina mkemeji hata mmoja.
   
 12. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Nilishawahi kusoma kitabu cha Vera ADLEY, chenye kuelezea mambo hayo, kwa mujibu wa mwandishi "Roho ndo inayoumbiwa mwili mwingine na haiwezekani mtu kukumbuka past life yake coz memory ni part ya mwili na sio roho"
   
 13. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hao wapuuzi wa kihindu wanataka kuthibitisha imani yao kuu ya Incarnation............
   
 14. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Jesus i love you! niepushe na njia zote za shetani!
   
 15. N

  Nyamanoro JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60
  <br />
  <br />
  Tuliambiwa tukifa roho zetu zitakwenda mbinguni(kwa wale wenye sifa)sasa hivi ya kurejea tena imetoka wapi?
   
 16. Lyamungo

  Lyamungo Member

  #16
  Aug 21, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kumbe kuna recycle bin ya watu? tehehehe. jiandae ukifa uzaliwe tena
   
 17. m

  mataka JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 287
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Mweeee! Makubwaaaaa
   
 18. P

  Pejokiss Senior Member

  #18
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 165
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwel hii kali ila kwa cc tuliolelew kweny maadil ya kidin ni vgumu kuamin kwan toka nikiw sunday school namin kuw ntakufa na cku ya mwisho ntafufuliw na mungu so kwa hl naona ngumu kumeza ijapokuw ni vizur kujifunza mambo mengi ili uweze kupambanua mambo kwenye ulimwengu huu.kwa upande wngu naamn Bible!
   
 19. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #19
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  sa wasemage kabisa nkifa ntazaliwa dume hivi hivi au jibinti niandae kabisa vipedo...
   
 20. Kiteitei

  Kiteitei JF-Expert Member

  #20
  Aug 22, 2011
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 1,253
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  yaaani ina maana kuwa hata wewe unayesoma hapa ulishakufa kitaambo na umerejea tena!?hebu mtu mmoja ajitolee then akirudi mara ingine aje kutuhabarisha huku jf!
  nadhani twaelekea ukingoni mwa hii dunia kwani kila uchao tunapata habari zinazokinzana na maneno matakatifu!
  mambo ya second chance
   
Loading...