bima ya taifa ya afya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

bima ya taifa ya afya

Discussion in 'JF Doctor' started by MamaParoko, Nov 26, 2009.

 1. MamaParoko

  MamaParoko JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 465
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jamani naombeni maoni yenu kuhusu bima ya taifa ya afya, kuna mvutano kazini kuhusu kujiunga nayo, je kwa waliowahi kutumia mnaonaje huduma za bima hiyo? ni za kuridhisha au?
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  WHAAAAT!!!.......FULL WASTE OF RESOURCES!...is all i can SAY ABOUT THIS SERVICE...

  Ni ya kishenzi mbaya kabisa....Mi ninapoishi ni kwamba mahospitali yoote wanawakataa wateja wa Bima ya Afya...!

  Ni wasanii wa hatari, they just are there to rip money from Poor contributors, while delivering a miserable service in return...huh!

  I suspect there are hidden hands with this service...Its there to foster some peoples interests!
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu inategemea uko katika shirika au sekta gani!!! Kama ni serikali, then unatakiwa ufuate sera ya serikali kuhusu social security ya wafanyakazi wake...

  Ila kwa ukweli bima ya afya haitoshelezi mahitaji!
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Nov 27, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Bima ya afya kwa kweli ni usanii, hospitali nyingi haziwathamini wagonjwa wanaotumia bima ya afya.
   
 5. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,638
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  MamaParoko bila shaka uko pale kwa wasomi! Ngoja nami nikae mkao wa kuisikia humu ili sera yake ikiletwa kwetu niwe nilishaijua
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu, kwanza tukubali kwa kiasi fulani NHIF imepiga hatua sana kwenye kujiweka katika ramani ya health care financing hata Tz, their website is also far better than most of our government isntitutions (including hata ile ya wakuu)

  Now, challenges bado ni nyingi kwasababu ya namna NHIF inavyo-integrate na local government na vituo vya afya visvyo na direct management ya serikali (FBO, VA na private), hapo kidogo patahitaji collective approach
  wenye bima hizi hawathaminiwi kutokana na limitations za services na products zinazotokana na caps! hivyo kuonekana ni wa hadhi duni kulinganisha na mifumo mingine ya bima ya afya

  Kuna huge problem kwenye accountability hasa kwenye hospitals zinazopata multiple supports - utakuta hospitali zinapata dawa za misaada halafu wanacharge wagonjwa kwenye forms za NHIF na hili linapelekea NHIF kuibiwa. Inawezekana kabisa hili tatizo linasukwa na baadhi ya NHIF staffs na pesa kupigwa panga

  NHIF imekuwa ikijivunia hata efforts ambazo si za kwao ilimradi wao wanasapoti hospital basi chochote chenye improvement wanaclaim wakati si kweli
  NHIF imeshindwa ku-adress suala nyeti la dawa accountability wakati kwenye fact sheet yao inaonekana wazi kwamba ni muhimu

  I am sure wanaelekea kuzuri lakini humuma zao zinahitaji kuwa more integrated na mifumo iliyopo na waboreshe accountability, nina imani hii ni epa nyingine isipoangaliwa vyema kutokana na baadhi ya halmashauri kuweka magonjwa na dawa feki kwenye fomu feki kuongeza kipato
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  NHIF ni bonge la EPA. Na kuonesha kuwa kuna mkono wa mtu, Bunge tayari limepitisha sheria kuwa kila mfanyakazi lazima ajiunge nalo. Mfano jamaa yangu anatoa 3% ya mshahara kwa mwezi (>60,000/- kwa mwezi) na mwajiri anamchangia kiasi kama hicho. Je kuna uhalali wowote wa kutungiwa sheria ya kulazimisha wafanyakaji kujiunga na NHI?
   
 8. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama wapo serious na wanajua wanachokifanya, kwa mfano serikali kama mwajiri ilitakiwa kugharamia huduma za afya, nyumba na elimu kwa wafanyakazi wake na familia zao, kinyume chake mbali na kodi wanazokatwa kuchangia huduma za kijamii ikiwemo afya, mfanyakazi huyu anatakiwa kuchangia tena bima ya afya ambayo mwisho wa siku haimsaidii!
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu, pesa ya uchaguzi yhiyo!!! we subiri sheria itapitiwa tena mwaka 2011
   
 10. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi nimewahi kutumia ni nzuri. hasa ukipata green card tumia hospitali zinazoeleweka kama agakhani hakuna matatizo. kwa broun card ndio kuna matatizo

  angalizo: kupata greencard unatakiwa kuwa na mshahara kuanzia Tshs. 864,030/- kwa mwezi au zaidi, chini ya kiwango hiki utapata brown card
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu tatizo sio wewe kupata huduma, tatizo ni hiyo huduma unayopewa kugeuzwa dili kati ya hospitali na wafanyakazi wa NHIF

  Sadly, hata zile dawa za magonjwa nyemelezi ya ukimwi na vipimo vya maabara vinavyolipiwa huingizwa kwenye fomu na watu kupata reimbursement kutoka NHIF

  bora nikae kimya maana huko ni soo
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hii bima ya kipumbafu sana wife anayo baba yake ni mwanachama lkn hospitali zote wanakataa, utasikia yaani huna kadi nyingine? wakiiona tu utawaona wanavyosikitika, simu zitapigwa hapo kuulizana mpaka utibiwe ht masaa mawili yatakuwa yamepita
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  I hope kuna waandisi wa habari wataongea na wakurugenzi wa NHIF halafu watoe wiki ijayo kwenye magazeti kama ilivo kawaida yao ya kukopipesti JF
   
 14. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2009
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu umesema ukweli unapokua na Green card kuna unafuu kidogo,, ila wengiwetu tuna Brown card kutibiwa ni baadhi ya hospitali,,hupatiwi huduma katika hospitali yoyote.

  Nilitaraji kama ni bima ya Afya ya TAIFA kipaumbele kingewekwa kwa watu wa kipato cha chini alau katika suala hili muhimi la Afya.

  Kwa kiwango hicho cha mshahara huduma hiyo ni kwa watu wa tabaka fulani la wenye nacho wengine tutakua ni wachangiaji tu
   
 15. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #15
  Jan 1, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Jamani tuweni wa kweli kwa nafsi zetu. Unafuu wa tiba ya Green Card unatokana na kiwango cha mchango. Mimi ninayo hiyo Green Card lakini ningepewa nafasi ya kuchagua kutoka ningetoka maana ninachanga kiwango kikubwa na kwa uwezo wa mungu mahudhurio yangu hospital hayaendani na mchango huo. Hata hivyo kwa vile ni bima inatukuwa kama nimewekeza. sasa iweje huduma ipatikanayo iwe sawa na yule ambaye anachangia kidogo? Tusahau mambo ya zamani anayeumia zaidi kimichango apate huduma zaidi logic inadictate hivyo wala siyo ubinafsi
   
 16. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Mimi nina green card lakini masuala ya madawa ni usanii mtupu, Vipimo na kumuona daktari haina shida lakini hata daktari akikuandikia dawa za mwezi mzima unapewa za wiki moja tu. hii ya madawa imenikumba leo hapo agakhan dar es salaam na nilipoulizia nikaambiwa wanatoa madawa ya wiki moja tu, eti hiyo ndiyo sera ya bima ya afya ya taifa.
   
Loading...