Naomba kufahamishwa na yeyote mwenye taarifa sahihi kuhusu mapato ya mfuko wa taifa wa bima ya afya. Swali langu la msingi "Ni kiasi gani mfuko wa taifa wa bima ya afya hupata kutoka katika mishahara ya wafanyakazi wa serikali kwa mwaka?" hata hivyo kiu yangu ya kufahamu hilo haitaishia hapo kwani nilihitaji kufahamu zaidi "fedha hizo zinazidi au zinapungua kwa kiasi gani ukilinganisha na bajeti ya serikali kwenye wizara ya afya?"