Bima ya afya ya Taifa (NHIF) Ni hisani au haki ya Wafanyakazi Serikalini?

Michewen

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
24,567
32,221
Hii bima (NHIF) ni lazima kwa wafanyakazi wote wa serikali utake usitake utakatwa makato kwenye mshahara wako kuchangia bima hii, kwa maneno mengine NHIF hupata mabilioni ya Tshs.

Kila mwezi kutoka katika michango wote wa Serikali, Kivumbi kinakuja mfanyakazi/wategemezi wake wanapotaka kwenda kutibiwa/kupata huduma za afya katika hospitali zilizoainishwa na Bima hiyo, haya ndo wanayokumbana nayo;

1. Kudharauliwa na watoa huduma (utasikia kama wewe wa Bima ya NHIF subiri, mara dawa hii bima hailipii.

2. Mkusanyiko/foleni kubwa ktk kupata huduma (jiandae siku nzima/masaa 12 kushinda hospitali husika).

3. Kuongezea pesa kutoka mfukoni mwa mgonjwa, pamoja na makato makubwa ya kila mwezi kuna baadhi ya huduma/vifaa tiba NHIF hutoa hela kiduchu sana, mfano miwani ya kusomea NHIF hutoa 25,000/= tu hebu niambieni miwani gani utapata kwa hela hiyo?

5. Baadhi ya magonjwa kutojumuishwa katika matibabu ya kutumia kadi ya NHIF

***NHIF kwani mwawapa wateja wenu hisani kupata huduma ya afya?
 
hii bima ni takataka kuliko kitu chochote,wanakata kila mwezi lakini huduma ni sifuri. pawepo na uhuru wa kujiunga na mifuko mingine ya afya hata kwa kuongeza pesa ili wake zetu wasipate shida wanapopeleka watoto huko mahospitalini. wanawake wanapata shida sana wanatukanwa sana sana. huwa natamani hata kwenda kudai hela yangu aisee. hawa jamaa na ni waswahili utafikiri vindege pori.
 
wanakazana kujenga majengo makubwa sijui kwa ajili ya nani?
wanalipana mishahara mikubwa kwa hela za watumishi ambao hawapati kile wanachostahili
 
daah bora umeliona ndugu yangu yaani hakuna mtu anakereka kama mimi sasa ngoja upoteze kadi uone huo muda wa kuipata jinsi ni changamoto.
hospitali wanawachagulia watu wakati wanamiliki fedha zetu hii ni mbaya sana i wish siku moja nijitoe tu coz manufaa na ufanisi wa mfuko huu ni mdogo sana kwa watumishi ukizingatia na fedha ambayo mtu anakatwa.
 
Mi naomba kuuliza, inamaana hii bima haina msaada?...gharama za hospital na vipimo kwa mtu asiye na bima inakuwaje na alie na bima inakuwaje?
 
secrete ndugu nielimishe, hivi nhif ni lazima kujiunga kwa mwajiri private
 
Last edited by a moderator:
NHIF ni weziiiii... weziiii wakubwaaa...!!!

3% ya GROSS salary kila mwezi wanakatwa wafanya kazi...!!! Hii ni asilimia kubwa sana sanaaaa....!!! na hawana limit kiwango cha juu... mfano. anayepata mil 8
kwa mwezi, hulipa tshs. 240,000 kila mwezi... na hawapunguzi...!!!

na HUDUMA ukienda hospitali ni mbovu sana....

Lazima wanatakiwa waweke OPTION... ya kujiunga kwa HIYARI... au mtu kuchagua mifuko mingine...!!!
 
NHIF jengeni hospitali kila wilaya ili mboreshe huduma. Hakikisheni huduma zunapatikana mpaka vituo vya afya maana misururu ya wanachama wenu mahospitalini ni kuonyesha mmezidiwa na kazi
 
Back
Top Bottom