PreGE2025 Billioni 19.8 Zawekezwa Hospitali ya Rufaa Simiyu

PreGE2025 Billioni 19.8 Zawekezwa Hospitali ya Rufaa Simiyu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Waziri wa Afya Jenista Mhagama amezitaka hospitali zote nchini kusimamia na kulinda miundombinu iliyopo, kwa kuwa Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya kwa kuboresha miundombinu na vifaa tiba.

Waziri Mhagama amesema hayo alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simuyu kwa lengo la kukagua ubora na huduma zinazotolewa, kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika wodi ya mama na mtoto, kukagua ujenzi unaoendelea katika jengo hilo na kuzungumza na watumishi wa hospitali hiyo.

"Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameirahisisha sana kazi yetu ya tiba nchini, ameifanya iwe nyepesi, kuna mashine na miundombinu ya kila aina, hapo mtoaji huduma amerahisishiwa kwa kiasi kikubwa sana, na hiyo ndio faida ya Serikali sikivu," amesema Waziri Mhagama

Ameongeza kuwa Serikali imetoa shilingi bilioni 29 kwenye huduma za afya ambapo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 19.8 hivyo miundombinu iliyopo inapaswa kulindwa.

"Ombi langu jingine kwenu ninyi watumishi mzingatie maadili katika utoaji wa huduma zenu, wakataeni wale wanaokwepa kiapo chao cha maadili na kujiingiza kwenye makosa ya jinai, tuzingatie viapo vyetu na kutoa huduma kwa utu na usiri mkubwa," amesisitiza Waziri Mhagama



Chanzo: TBC DIGITAL
 
Back
Top Bottom