GE2025 Billioni 19.6 imetolewa kuboresha Miradi ya Elimu Njombe

GE2025 Billioni 19.6 imetolewa kuboresha Miradi ya Elimu Njombe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi Bilioni 19.6 kwa ajili ya Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari SEQUIP mkoani Njombe

Kati ya fedha hizo jumla ya Shilingi Bilioni 4.360 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo majengo ya madarasa, maabara, mabweni, bwalo la chakula, jengo la utawala na nyumba za walimu katika shule ya Sekondari ya wasichana ya mkoa wa Njombe ambayo imekamilika

Hayo yamebainishwa tarehe 17 Julai 2025 na Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa Njombe Mwl. Nelasi Mulungu ambapo amesema pia Bilioni 1.6 imetolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Mkoa ya Amali ambayo inaendelea na ujenzi katika Wilaya ya Ludewa

Mwl. Mulungu amesema kuwa serikali imetoa zaidi ya Bilioni 12.638 kwa ajili ya ujenzi wa shule 20 za kata katika mkoa huo wa Njombe

Pia amesema kuwa serikali imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mingine katika mkoa wa Njombe ikiwemo ujenzi wa mabweni, nyumba za walimu, na matundu ya vyoo

1752824163078.png


1752824187741.png


Chanzo: Jambo Tv
 
Back
Top Bottom