Bilioni 61 zatumika kulipana posho TANESCO

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,731
15,188
Gazeti la Raia mwema la leo limekuja na ufisadi wa kutisha uliofanywa na shirika la Tanesco kwa miezi kumi iliyopita kwa kutumia zaidi ya billioni 61 kwa kulipana posho viongozi wa shirika hilo la uma kila wanapofanya vikao au ziara mbalimbali za kikazi ndani ya nchi.!

Hata hivyo Zito Kabwe amesifia hali hiyo na kusema hayo ni matumizi ya kawaida tu.
20220430_085626.jpg
 
Tutaandika nini ili Mama amtoe hapo huyo mwanaye Mwezi wa kwanza?

Inakera sana na inakatisha tamaa sana Kwa walipa kodi, kulipa kodi ili viongozi wakagawane?

Nakubaliana na wote wanaodai kuwa katiba ni mbovu, haina meno ya kumng'ata Rais anapomaliza muda wa kuongoza?

Ingelekuwa na meno, Mama asingeweza kukubali kuwa na mawaziri majizi ambayo hata mwaka na nusu hayajamaliza, lakini hasara yaliyoitengenezea nchi, ni mabilioni ya fedha
 
Tutaandika nini ili Mama amtoe hapo huyo mwanaye Mwezi wa kwanza?

Inakera sana na inakatisha tamaa sana Kwa walipa kodi, kulipa kodi ili viongozi wakagawane?


Utaambiwa acha kelele tafuta shughuli yakufanya upate pesa yako bila kujua hio pesa wanaokuambia uitafute serikali inachake hapo na inatafunwa usiku na mchana…wacha tunyonywe damu mpaka siku ya kudondoka ifike…
 
Huku Maharage anadai hana fedha za kuhimili mita za 27000 shs
Hili la posho ni kila wizara, mashirika na idara za serikali. Zile semina magumashi za kwenye mahotel ya bei mbaya na posho za kila aina zimerudi kwa kasi ya ajabu. Nadhani ni moja ya strategic ya rais Samia kujaribu kurudi watu kwenye enzi za Kikwete ili wamsifu, asijue kuwa Kikwete ndiye chanzo cha maangazi ya CCM.
 
Nimekumbuka na zile $ 30mil za maintanance.

Hayo mapesa huwa wanayachezea kwa kisingizio cha kuongeza pesa kwenye mzunguko, hii ndio akili ya waswahili wanaotuongoza.

Na kuna mazuzu huwa wanashangilia watakwambia hata wakati wa Kikwete hali ilikuwa nzuri mtaani, pesa ilikuwepo, wasijue wanaokula vizuri hizo pesa ni wale walioko mezani.
 
Kipindi Cha magufuli hizi bilion 60 zilikuwa sio pesa kina Doto James wamepiga sana. Huamin muulize makam wa Rais afu hoji Ile ripoti ya ukaguzi wa BOT!!!.
Acha watu wale pesa maana watu wakidai katiba mpya itakaemshughulikia Kila mtu mnakuja na hoja za kiccm. Ni ujinga kuleta Uzi wa pesa za umma wakati unapinga kuwa na KATIBA MPYA ambayo ndio msingi wa kuwa Taasisi imara zitakazomshughulikia Kila mtu bila kuangalia ni nani na yupo nyuma ya nani.
 
Kuna kipindi ninefanya kazi hotel mojawapo dodoma tulipata kushinda zabuni ya kupeleka break fast kwenye ofisi za NSSF na TANESCO aseee ile chai tuliokuwa tunaipelekea pale kila siku sio ya kitoto aseee pesa inaliwa na mchana watumishi almost wootw wanakuja kula buffet hotelin jaman nyie nyie nyie nyie nyie
 
Back
Top Bottom