Zee la shamba
Member
- Oct 17, 2007
- 55
- 5
Yule mwanasiasa aliyeibua hadharani sakata la ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania, BoT, Dokta Wilbroad Slaa leo ameibuka na mapya kwa kudai kuwa, eti zile Bilioni 50 kati ya 133 zilizoibwa, ambazo Serikali ilidai kuwa zimerejeshwa, ni changa la macho.
Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Dk. Slaa amedai kuwa licha ya Tume iliyoundwa kufuatilia suala hilo kutangaza kuwa Bilioni 50 kati ya bilioni 133 zinazodaiwa kuibwa zimerejeshwa, amepata taarifa nyeti na za uhakika kwamba pesa hizo hazijarudi.
Dk. Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu kupitia chama cha upinzani cha Chadema, amedai kuwa kilichofanyika ni kwamba hao wanaodaiwa kukwapua mapesa hayo, walikwenda mbele ya Tume hiyo wakiwa na wanasheria wao na kisha kuingia mkataba wa kurejesha pesa hizo taratibu.
``Nimefuatilia na kubaini kuwa hakuna pesa wanazorejesha kwa sasa, isipokuwa wanakwenda na wanasheria wao na kuingia mkataba wa kurejesha pesa walizochota kidogo kidogo,`` akadai Dk. Slaa.
Ameongeza kuwa suala hilo limemshangaza sana kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na wizi kubadilishwa na kuwa deni.
``Mtu wa chini akifanya kosa anahojiwa na kuchukuliwa hatua haraka sana, lakini hawa wameiba mapesa yote hayo na ushahidi upo, lakini wanabadilishiwa kosa la wizi kuwa deni,`` akadai Dk. Slaa
Amesema ingawa hakuna mlango hata mmoja wa BoT uliovunjwa wakati wa wizi wa fedha hizo, lakini ushahidi wa hundi za kuchukua fedha hizo upo na hivyo kitendo hicho hakiwezi kuachwa kuitwa kuwa ni cha jinai.
SOUCE: Gazeti Alasiri