Elections 2010 Bilioni 50 za CCM zitatugharimu!

Msijali. Hata KANU ilikuwa ina mabilioni wakati ikivaliwa na Kibaki. UNIP vile vile ilikuwa imejaa mapesa lakini ari ya Wazambia ya kutaka mabadiliko ikakiondoa. CCM hivyo hivyo. No ammount of money will save it this time. Watanzania wamechoka ile mbaya. Wanataka mabadiliko.

Hongo watatoa CCM lakini kura atapata Slaa.
 
nitaleta data soon ya ujambazi wa CCM , wamechukua THS. BILIONI 1.8 toka TANAPA aidha pia MAMLAKA YA NGORONGORO wamechukua Bilioni 1.2 nimepokea vielelezo vya SONGAS wamechukua Bilioni 4 naendelea kuunganisha ushaiidi huu ili nimpe Dr. slaa na pia kuuwasilisha Benki ya Dunia na kwa wafadhili ili wachukue maamuzi.


kimsingi alichoandika PhD ni kweli....kabisa wanaojaribu kumpinga wanafanya hivyo kwa malengo maalum kwa kuwa wanajuwa ni ukweli.......wafanyabiashaara wote wakubwa unaowajuwa wewe wameshakamuliwa na hawana hamu ,wanaugulia chinichini....tuliwaeleza wiki iliyopita kuwa tulipata taarifa za harambee ya siri iliyofanyika kwenye hoteli moja masaki....taarifa rasmi hazikutoka lakini ...baada ya siku tatu nipashe la tarehe [kama sikosei 17] ukurasa wa tano likaandika kwa ufupi mno kuwa ...walipata biilioni 4....

karibuni inaandaliwa tena harambee nyingine ambayo hiyo itakuwa ya wazi......hizo ni acha vimemo vya kuomba misaada wanavyopewa wafanyabiashara mbali mbali....

Haya makamupuni aliyotaja PhD ni kweli yameshatoa bilioni..40 ...naongelea bandari,Ticts,dahaco,nssf,ppf,pspf,bot.crdb,nmb,songas,ngorongoro,IKULU,tanapa,kempski group,manji,mm industy,jeetu patel....na mengine....wameshawapa bilioni 40 tayari.......
hIZi harambee za siri na wazi zina lengo ka kukusanya bilioni 10 tu ...zilizosalia hapo.....

amini usiamini...hiyo ndiyo hali halisi....hata za chini ya kapeti ya EPA zilipoanza kuna waliosema ni uwongo......!!....take your own stand on this ...lakini si kuanza kupinga....pale pesa za wanyongwe zinapoliwa!!!
 
naomba hizo data apewe Dr slaa

nawaomba watanzania wenzangu tuungane kuiondoa ccm
 
Vyama vyote vya siasa vinafanya fundraising...sasa tatizo liko wapi ? Ukitoa malalamiko ni vizuri kuthibitisha au sio inakuwa ni majungu tu!

Mapambano,

Ushabiki wa kisiasa pembeni. Kama CCM wana uwezo wa kuchangisha TShs bilioni 50 kwa ajili tu ya kampeni, na ndicho chama kilicho madarakani, kwa nini hii mbinu hawajawahi kuitumia siku zote katika kuchangisha kwa ajili ya shughuli za maendeleo badala ya kusubiri 'misaada' toka nje?
 
Hata Dr Slaa akifia majukwaani kwa kuwaeleza wananchi wizi huo wa CCM wqananchi wengin hawatomuelewa kabisa. Wengi kwanza hawajui TANAPA ni nini.

CCM inajua inachokifanya kwa kutambua kuwa nchi hii is blessed with teeming herds of sheep instead of humans!

Wewe una jukumu la kumsaidia Slaa kumuelimisha baba yako na mama yako na bibi na babu yako na mzee jirani yako kule kijijini, shangazi mjomba etc. Probelm yetu hapa tunafungua midomo tu, lakini hatufanyi kivitendo, si ajabu ni wachache wetu tumejiandikisha kupiga kura.

Kama wachangga wanavyofunga safari wakati wa sikukuu za mwisho wa mwaka kwenda makwao, vivyo hivyo tunapaswa sote kufunga safari kwenda vijijini mwetu wakati huu wa kampeni kwenda kuwajuza na kuwahubiria wazee wetu na kuwaonya kuwa hali yao itakuwa mbaya kwa sababu hali yetu huku mjini pia itakuwa mbaya na kile chochote kitu tunachowatumia kitapungua kama hawatatumia kura yao vizuri kuondoa ukiritimba na udhalimu wa ccm. I tell you CCM ikiingia madarakani tena watanzania watarajie hali ngumu mno ya maisha, mara nyingi raisi hafanyi mengi kwenye kipindi chake cha pili, zaidi ya kuiba, mtakumbuka Mkapa aliharibika katika kipindi chake cha pili, but more precisely baada ya Mwalimu kufariki

Kuna fedha nyingi zilipelekwa NHC kwa ajili ya kujenga nyumba za gharama nafuu (Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa NHC alipohojiwa na Mwakai wa Kuhenga). Nawaasa Chadema waangalie vizuri NHC kwa kuwa ni possible ikawa mojawapo ya conduit ya kufuja fedha za Watanzania. Japo mkurugenzi wake ni mtu makini lakini anaweza kubanwa na machinery za CCM akapotea stepu. This time hawatachota BOT, but watachota kusikojulikana kama Tanesco, NHC etc.

Sh 50BN hazitatosha kwa kampeni za JK na CCM yake. Kama mwaka 2005 walichota 133bn za EPA this time is even more. Na kumbuka mwaka 2005 JK alikuwa anapendwa kwani wengi walikuwa hawajamshitukia kuwa ni feki, this time around things are different na pia ujio wa Dr Slaa, unafanya kibarua chake kiwe kigumu. JK kipindi chake cha kwanza ameshuhudia wapinzani wakiimarika kutokana na utendaji mbovu wa serekali yake ni ufisadi, kitu kianchofanya awamu yake ya pili kuwa ngumu kuitetea.

So CCM watahitaji fedha nyingi zaidi ya 50bn, hapo ndipo penye kirumbe rumbe, yetu macho, Chadema, tupieni jicho mashirika ya umma, mihela itachotwa huko vibaya sana!!
 
Back
Top Bottom