Bilioni 50 za CCM zitatugharimu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bilioni 50 za CCM zitatugharimu!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Martinez, Aug 20, 2010.

 1. M

  Martinez JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Tayari CCM imeshayakamua makampuni mbalimbali yaliyopo tanzania. Mpaka sasa imekusanya tzs bilioni 40, lengo ni bilioni 50(milioni 50,000.00). Kisa... Kampeni!

  ...kwangu hiki ni kielelezo cha ujinga wa viongozi wetu, hawaangalii upande wa pili. Kampuni hizi kesho zikikwepa kodi utazilaumu? Kesho zikichota fedha BOT utazilaumu? Kesho zikipora ardhi za wananchi utakuwa na ujasiri wa kukemea? Kesho zikijenga barabara feki utaweza kuchukua hatua??? ...nani hasa anayeumia?

  ...kwanini chama kisichangiwe na wanachama wake kama ilivyo kwa wenzetu???
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  nitaleta data soon ya ujambazi wa CCM , wamechukua THS. BILIONI 1.8 toka TANAPA aidha pia MAMLAKA YA NGORONGORO wamechukua Bilioni 1.2 nimepokea vielelezo vya SONGAS wamechukua Bilioni 4 naendelea kuunganisha ushaiidi huu ili nimpe Dr. slaa na pia kuuwasilisha Benki ya Dunia na kwa wafadhili ili wachukue maamuzi.
   
 3. a

  akilipana Member

  #3
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  What do you mean "wamechukua"? Kampuni zililazimishwa/shurutishwa au zilichangia zanyewe kwa woga wao? Hebu fafanua zaidi
   
 4. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  anasema wamechukua maana TANAPA ni ya watanzania na hatujatoa ridhaa ya kuzitoa
   
 5. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Kaka unapotaka kuhakikisha unarudi madarakani by all means hii ndiyo maana yake, unakumbuka zile Mahindra 4 x 4 za CCM toka india?
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,548
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Hivi unafikiri nini, rais amewaita hao wafanya biashara kwenye fund raising ya CCM, kama siyo kuwalazimaisha ni nini? Au kwa yale mashirika ya uma, ni meneja gani atakataa kuichangia CCM, il hali huo umeneja kapewa na huyo mgombea wa CCM? Haya ndiyo matumizi mabaya ya Ofisi za serikali. Hivi watanzania mnataka ushahidi gani juu ya ufisadi wa CCM ? Matokeo ya hayo mabilioni tumeshaana kuyaona, magazeti yanayounga mkono upinani hasa Chadema,yananunuliwa na kwa wingi na mafisadi na kuchomwa moto ili yasiwafikie walengwa.Kweli CCM ni mafia.
   
 7. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kichefuchefu.
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hata Dr Slaa akifia majukwaani kwa kuwaeleza wananchi wizi huo wa CCM wqananchi wengin hawatomuelewa kabisa. Wengi kwanza hawajui TANAPA ni nini.

  CCM inajua inachokifanya kwa kutambua kuwa nchi hii is blessed with teeming herds of sheep instead of humans!
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,345
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  he...tukipata hii itakuwa poa eeeee......nchi inaliwa hivihivi tukiwa macho...yaaani kweupeeeee...sisi kweli wadanganyika.................
  sasa ccm wanajisifu wametekeleza ahadi zao walizoahidi...swali, je wana wasiwasi gani kuhusu ushindi ktk uchaguzi wa mwaka huu...kweli kuhangaisha watu wachange mihela yooote hiyo badala kuwaomba wasaidie kujenga huduma za jamii wanafanya upumbafu huu???? kweli?..watu hawana vitanda mahospitalini...wanafunzi wanafukuzwa shule na vyuo....hakuna dawa mahospitaliniu......hey jk wake up!!!! where are u.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Halafu nauliza -- kwa nini MS (na aliases zake nyingine anazotumia humu ndani) huwa hazungumzii kabisa ufisadi -- kwa maana ya kuchangia mjadala, achilia mbali kuanzisha topic kuhusu ufisadi? Yeye kikubwa anakazani topic za muelekeo wa kidini tu.

  Hana habari kabisa kama nchi hii inaliwa na genge la mafisadi ndani ya serikali ya CCM -- huku serikali hiyo ikifanya ubaguzi wa ikiwalinda mafisadi wale inaowapenda na kuwatoa kafara wale isiyowapenda kwa geresha ya kuwapeleka mahakamani!
   
 11. m

  mapambano JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vyama vyote vya siasa vinafanya fundraising...sasa tatizo liko wapi ? Ukitoa malalamiko ni vizuri kuthibitisha au sio inakuwa ni majungu tu!
   
 12. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280

  Siku zote mjue anayetoa majibu kama haya mjue na yeye ni yule yule kwenye kundi. Huyu si mtanzania wa hali ya kawaida, Lazima hapo alipo anafaidi kwa namna moja au nyingine matunda haya ya ufisadi. Ole wenu Ipo siku tu mtaondoka. Endeleeni kula raha za dhuluma. Lakini jua Mungu yupo kaka. Huwezi jua watanzania wengi wanavyoishi kwa taabu. kama kila siku uko kwenye shangingi linawekwa mafuta na hela zetu walipakodi, huwezi kunielewa nikilalamikia bei ya mafuta inayotokana na Mfumko wa bei uliosababishwa na uongozi Mbaya,
  Naomba nikupe taarifa tu. Slaa is our next President kwahiyo jiandae.
   
 13. Mwanamosi

  Mwanamosi Member

  #13
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sioni tatizo la CCM kukusanya bilioni 50 kwa njia ya fund raising..ishu labda tuseme matumizi ya hela zote hizo kwa kampeni..sina hakika na sijaona mchanganuo wa CCM kwa ajili ya kampeni zake mwaka huu ila nadhani hayo ni malengo waliyojiwekea ili kuweza kushindana kikamilifu katika uchaguzi...suala la msingi si kulaumu makampuni yanayochangia ila ni kuyabana yachangie kwa mtindo huu huu kwenye huduma za jamii kwani kama inawezekana kuchangia CCM basi inawezekana kuchangia maendeleo ya jamii kwa kiwango hikihiki walichochangia kwa njia hizo hizo...nadhani CCM wamewazidi mbinu tu wapinzani kwenye hili kwani hata wapinzani wangetumia fursa hii kukusanya fedha za kampeni ila kwa kuwa makampuni yalishawahiwa na kujicommit kuchangia CCM hivyo inawawia ugumu kuchangia na upinzani pia..nijuavyo mimi kampeni zina mambo mengi na humo pia kuna watu hujitengenezea miradi yao na kujipatia chochote so sishangai kuona CCM ikilenga kukusanya BIL 50 kwa kampeni kwani gharama za vifaa vya uchaguzi nk ni kubwa ukichukulia ni kampeni ya kuzunguka nchi nzima kwa takriban miezi miwili...hapa ndipo CCM huwapiga bao wapinzani ambao huchagua maeneo muhimu kwa kuwa gharama ya kuzunguka kila kona ni kubwa mno.
  binafsi sipendi ufisadi ila kwenye hili natofautiana kidogo na baadhi ya watu coz nazitazama bil 50 na matumizi yake ktk uchaguzi kwa maana ya gharama halisi ya kuzunguka mikoa yote kwa kampeni au kanda zote na kundi linalozunguka je uwezeshaji wake ukoje? kinachonichukiza ni pale baadhi ya watu wenye mamlaka wanapotumia fedha hizi kunyanyasa wanyonge na kujinufaisha binafsi hali inayopelekea CCM kuingia lawamani kwamatumizi mabaya ya fedha ambazo malengo yake ni kampeni japo hawabanwi jinsi ya kuitumia( wanaweza kutumia kwa kuimarisha chama kwa fedha hizo nk.)
  Rai yangu ni kwa vyama vingine kuchukua hii kama changamoto ili nao wanapokuwa na fedha ya kutosha basi ushindani utaongezeka na pengine kupunguza margin kati ya ushindi wa tsunami wanaoutambia CCM na mshindi wa pili na mwishowe mageuzi yatawezekana.
   
 14. M

  Martinez JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Ni kweli kwamba ccm ni kikundi cha nzige wanaoitafuna nchi, unachotakiwa kuelewa ni vyanzo haramu wanavyotumia kupata hizo 50BN. Kwanini wasichangishe wanachama wao kama vyama vingine? ...ni sawa na kumkamua ngombe, atahitaji kesho umlishe
   
 15. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ...changanya na za kwako...
   
 16. M

  Martinez JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  kuchangisha makampuni ni sawa na kumkamua ngombe, ni lazima kesho umlishe. ndio baadae tutasikia maufisadi kwenda mbele. Ukienda Arusha ndio utaujua ukweli huu. ardhi karibu yote ya mkoa huo imeuzwa kwa wazungu
   
 17. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,559
  Likes Received: 1,648
  Trophy Points: 280
  What if TUCTA wangechangia shilingi ata moja, i mean only 1/=
   
 18. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,559
  Likes Received: 1,648
  Trophy Points: 280
  Nasikia walitoa wale wahindi wa TRL. na hizi cruserr za sasa sijuhi katoa nani?
   
 19. M

  Mutu JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hii ndilo la maana ,thanks again
   
 20. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  CCM ni majambazi
   
Loading...