Bilioni 222 za Mikopo ya Vijana zimetafunwa na wahuni

Mbunge wa Makete (CCM), Festo Sanga amemuomba Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Tawala za Mitaa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa kuwatafuta waliochukua Sh222 bilioni za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu.

Sanga amesema hayo leo Alhamisi Aprili 14, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 2022/2023.

“Mikopo ya asilimia 10 imegeuka kuwa ni ya vijana wenye uwezo na si kwa ajili ya vijana wa Taifa hili,”amesema.

Amesema maelezo yaliyotolewa na Bashungwa yanaonyesha tangu mwaka 2017/2018 hadi mwaka 2020/2021 halmashauri nchini zimetoa mikopo Sh300 bilioni.

Hata hivyo amesema zaidi ya Sh222 bilioni zipo mikononi mwa wanyang’anyi na akatoa mfano wa Mkoa wa Tabora ambao umekopesha Sh5.7 bilioni, na fedha zilizorudi ni Sh2 bilioni.

Amesema Mkoa wa Pwani ulikopesha Sh11 bilioni lakini fedha zilizorudishwa ni Sh4 bilioni wakati Mwanza walikopesha Sh8.9 bilioni na kurejeshwa Sh3.9 bilioni.

Kwa upande wa Dar es Salaam mikopo iliyotolewa ni Sh52.3 bilioni lakini zilizorudi ni Sh14 bilioni na Sh12 bilioni zilitolewa mkoani Mbeya lakini zilizorudi Sh7 bilioni.

“Fedha hizi zipo katika mikono ya wanasiasa na watumishi, wanatengeneza wanawarubuni vijana wanaunda vikundi wanapewa fedha lakini wanaonufaika si vijana,”amesema.

Sanga amesema waziri huyo anaweza kuzifuatilia fedha hizo ambazo zipo mikononi mwa wahuni
Milioni 300 kala mwenyekiti wa ccm Temeke Peke yake !
 
Pesa hizi zenye mikono ya damu haziwezi kufanikisha lolote
 
Uaminifu

Matumizi sahihi

Na usimamizi mzuri wa miradi bado ni kitendawili.
 
Tena ngoja nimsaidie tu aende hapo hapo kwao muleba wilaya ya muleba Kuna milioni 104 zimeliwa na familia ya watu wawili Yan jamaa na wake zao eti ndo vikundi
 
Back
Top Bottom