Bilioni 222 za Mikopo ya Vijana zimetafunwa na wahuni

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Mbunge wa Makete (CCM), Festo Sanga amemuomba Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Tawala za Mitaa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa kuwatafuta waliochukua Sh222 bilioni za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu.

Sanga amesema hayo leo Alhamisi Aprili 14, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 2022/2023.

“Mikopo ya asilimia 10 imegeuka kuwa ni ya vijana wenye uwezo na si kwa ajili ya vijana wa Taifa hili,”amesema.

Amesema maelezo yaliyotolewa na Bashungwa yanaonyesha tangu mwaka 2017/2018 hadi mwaka 2020/2021 halmashauri nchini zimetoa mikopo Sh300 bilioni.

Hata hivyo amesema zaidi ya Sh222 bilioni zipo mikononi mwa wanyang’anyi na akatoa mfano wa Mkoa wa Tabora ambao umekopesha Sh5.7 bilioni, na fedha zilizorudi ni Sh2 bilioni.

Amesema Mkoa wa Pwani ulikopesha Sh11 bilioni lakini fedha zilizorudishwa ni Sh4 bilioni wakati Mwanza walikopesha Sh8.9 bilioni na kurejeshwa Sh3.9 bilioni.

Kwa upande wa Dar es Salaam mikopo iliyotolewa ni Sh52.3 bilioni lakini zilizorudi ni Sh14 bilioni na Sh12 bilioni zilitolewa mkoani Mbeya lakini zilizorudi Sh7 bilioni.

“Fedha hizi zipo katika mikono ya wanasiasa na watumishi, wanatengeneza wanawarubuni vijana wanaunda vikundi wanapewa fedha lakini wanaonufaika si vijana,”amesema.

Sanga amesema waziri huyo anaweza kuzifuatilia fedha hizo ambazo zipo mikononi mwa wahuni
 
Empty talk
Si angefanya uchunguzi kwanza na kubaini majina ya waliochukua mikopo bila kustahili na defaulters
That way angekuwa amemsaidia waziri..
One thing i know hiyo mikopo ya vijana akina mama wanakopeshwaga uvccm na uwt..
Hautasikia kesi hapo.
 
Tunataka uwazi wa namna hii.

Hizi pesa zimeliwa na maofisa wa serikali na wanasiasa kwa vikundi hewa..

Serikali iunde tume Ili waliokula hizi pesa warudishe na washtakiwe.
 
Pia kuweni wawazi kuwa hela zinaenda kwa watu wenu wa ccm tuu! Wengine wasio ccm hawawezi pata hata iweje! Mngesema ni mikopo yenu ya Wana ccm tuu.
Mikopo inatolewa kwa wote sio CCM pekee timiza masharti na vigezo utapewa mkopo
 
Hapo ndipo serikali inapofeli sema tu nao wanajichotea kwanza kisha wanasingizia zimepigwa na vijana.
Kwann pesa kama hizo serikali iwape ruzuku viwanda vya matrekta wazalishe kwa gharama nafuu kisha waje wauziwe wakulima kwa bei ndogo
 
Mbunge wa Makete (CCM), Festo Sanga amemuomba Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Tawala za Mitaa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa kuwatafuta waliochukua Sh222 bilioni za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu.

Sanga amesema hayo leo Alhamisi Aprili 14, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 2022/2023.

“Mikopo ya asilimia 10 imegeuka kuwa ni ya vijana wenye uwezo na si kwa ajili ya vijana wa Taifa hili,”amesema.

Amesema maelezo yaliyotolewa na Bashungwa yanaonyesha tangu mwaka 2017/2018 hadi mwaka 2020/2021 halmashauri nchini zimetoa mikopo Sh300 bilioni.

Hata hivyo amesema zaidi ya Sh222 bilioni zipo mikononi mwa wanyang’anyi na akatoa mfano wa Mkoa wa Tabora ambao umekopesha Sh5.7 bilioni, na fedha zilizorudi ni Sh2 bilioni.

Amesema Mkoa wa Pwani ulikopesha Sh11 bilioni lakini fedha zilizorudishwa ni Sh4 bilioni wakati Mwanza walikopesha Sh8.9 bilioni na kurejeshwa Sh3.9 bilioni.

Kwa upande wa Dar es Salaam mikopo iliyotolewa ni Sh52.3 bilioni lakini zilizorudi ni Sh14 bilioni na Sh12 bilioni zilitolewa mkoani Mbeya lakini zilizorudi Sh7 bilioni.

“Fedha hizi zipo katika mikono ya wanasiasa na watumishi, wanatengeneza wanawarubuni vijana wanaunda vikundi wanapewa fedha lakini wanaonufaika si vijana,”amesema.

Sanga amesema waziri huyo anaweza kuzifuatilia fedha hizo ambazo zipo mikononi mwa wahuni
Nina wasiwasi kama fedha zinazorejeshwa huwekwa kwenye hesabu za mapato ya halmashauri. Huenda nazo hupotelea mifukoni mwa watu. Imagine hizi ni za kuanzia 2017, tukichukua miaka kumi nyuma itakuwaje?
 
Empty talk
Si angefanya uchunguzi kwanza na kubaini majina ya waliochukua mikopo bila kustahili na defaulters
That way angekuwa amemsaidia waziri..
One thing i know hiyo mikopo ya vijana akina mama wanakopeshwaga uvccm na uwt..
Hautasikia kesi hapo.
Mbona kataja wanasiasa au hujaelewa, aisee we utakuwa darasani ulikuwa mweupe. Hapo kamsaidia waziri ajue pakuanzia, kizipata tu hizo takwimu unafikiri ni kula ugali
 
Huyu mbunge ni makini sana.. sijui mama anachelewa nini kumpa wizara
 
Hizo hela wamekula vijana wa CCM na zingekua zinakopeshwa kweli kwa sisi vijana wajasiriamali zingerudi na wangefurahi.... Sasa kama wanagawana watu wasio na focus yoyote zaidi ya vyeo vya chama na madaraka .... Tutoleeni upuuzi wenu hapa
 
Mbona kataja wanasiasa au hujaelewa, aisee we utakuwa darasani ulikuwa mweupe. Hapo kamsaidia waziri ajue pakuanzia, kizipata tu hizo takwimu unafikiri ni kula ugali
Wewe nawe
Wenzie wanakabidhi hadi majina ya watuhumiwa bungeni
Sasa kujua defaulters kuna kazi gani
Ametuhumu watu hapo ni wajibu wake kukabidhi hayo majina
Otherwise ni makelele tu.
 
Back
Top Bottom