Bilion 1.3 zatumika kuitangaza Tanzania nje

Bodi ya Utalii isiangalie TV tu, kuna njia zingine nafuu kama internet. Wanaweza wakaweka tangazo la video kwenye YOUTUBE pamoja na mitandao ya magazeti maarufu duniani kama New York Times, Washington Post, New York Post, Washington Times, The Guardians, The Jerusalem Post etc. Najua humo kwenye hayo matangazo ndo kuna milo ya fisadiz wengine, hivyo ni vizuri kila kiti kikawekwa wazi.
 
But was it a worthwhile undertaking? 1.3bn kwa utangazaji-there must be something wrong with our priorities!!

We call this "Economic Diplomacy"..."inabidi kuliwa kidogo kabla nawe hujala"

Tatizo ni tunapokuja katika aina ya watumishi wanaopaswa kuwa frontline ya ku-utilize oppurtunities zinazoibuka kutokana na haya matumizi.....let say our front Desk people, secretaries, trade representatives in our embassies...

Hapo hatujafika kwa Mzee Ole Naiko na vijana wake wakiwa karibu na "wenziwao" wa Mamlaka ya Biashara za Nje....

Then we come to TRA....

Hatujaongelea kina Mr 100,000 thousand dollarmne waliojaa katika nafasi za uheshimiwa....

Ni disaster....

Tanzanianjema
 
Halafu labda watanzania tupunguze longolongo, maana hizi posts za kwenye hii topic (including my post) ni blaze blaze kila mtu anajua hata kama sio field yake, sababu sisi watanzania tunajua kila kitu.

Tuwaachie wataalamu wa Marketings & Ads wazalendo pale mjini wasaidie TTB na wizara ili kuitangaza Tanzania, na sio kila mtu kujifanya tunajua topics zote.

Humu ndani hatuchelewi hata kusema Dr fulani wa Moyo kakosea, ilibidi pulmonary artery ..... blah blah (na mimi na kibiology changu cha Azania) nataka nicomment.
 
Ni kweli kutumia site kama Youtube ni rahisi sana na haihitaji big production cost au gharama za utangazaji kama matangazo mengine kwenye televisheni. Kwenye Youtube wanaweza wakawa na channel ambayo kunakuwa na monthly statements kutoka kwa waziri husika na kueleza vivutio gani vinafaa kutembelewa na ni kwa nini hao watu watembelee, pia wanaweza kujumuishe videos za vivutio hivyo ma kuhoji hata baadhi ya tourists ambao wako hizo sehemu. Kitu kama hiki hakihitaji kuwa fancy sana. Na si Youtube peke yake kwani kuna video sharing site nyingi sana na ambazo zinaweza kusaidia kwenye hiki kitu.

Kutoa packages za bure kwa baadhi ya celebrities ili waje Tanzania na kutembelea vivutio mbalimbali, hii itasaidia kwa sababu hawa watu wanaporudi na kukutana na media mfano Jay Leno, Letterman au Oprah tutapata free advertisements wanapokuwa wanaongelea trips zao.

Summer Festivals mbalimbali ni muhimu sana kwa bodi ya utalii kuhudhuria, kila summer kuna festivals kibao za ethnic groups na hata baadhi ya conferences. Mfano kuna German Fest, Summer Fest, Irish Fest, African Fest, Italian Fest na nyingine nyingi sana.

Kuweka Billboards barabarani along airports kubwa na karibu na Theme Parks kama zile za Great America, Wisconsin Dells, Disney, Mount Rushmore, Great Canyon, Las Vegas na sehemu nyingine kibao. Hapa kuna chances ya kupata baadhi ya tourists ukichukulia baadhi ya hizi parks zinajisikia kuwa hakuna haja ya kwenda Africa kwenye safari wakati wanyama wote wanao hapa.

Nadhani kuna umuhimu wa hawa madingi wengi ambao wako kule bodi ya utalii na wizarani kuajiri vijana ambao wataleta fresh ideas.
 
Ni kweli, utaalamu unatakiwa kuheshimika, na sidhani kama kuna aliyepost kuwa matangazo yaliyofanywa yamekosewa, tunachojadili hapa ni jinsi ya kuharakisha namna ya watu wa nje kuifahamu nchi yetu. Kutangaza nchi duniani ni tofauti na kutangaza bidhaa kwenye soko fulani; kwa hiyo tukisema tutangaze nchi kwa kutumia njia conventional tu za kutangaza biadhaa kwenye masoko, kama vile matangazo ya television, magazetini, redioni, posters n.k., hatutafika popote. Njia unconvetional zinatakiwa sana, na hizo ndizo tunazo-brain storm hapa. Hao wataalamu watachambua ni njia gani ya kuongezea kwenye hizo conventional methods.
 
Ni kweli kutumia site kama Youtube ni rahisi sana na haihitaji big production cost au gharama za utangazaji kama matangazo mengine kwenye televisheni. Kwenye Youtube wanaweza wakawa na channel ambayo kunakuwa na monthly statements kutoka kwa waziri husika na kueleza vivutio gani vinafaa kutembelewa na ni kwa nini hao watu watembelee, pia wanaweza kujumuishe videos za vivutio hivyo ma kuhoji hata baadhi ya tourists ambao wako hizo sehemu. Kitu kama hiki hakihitaji kuwa fancy sana. Na si Youtube peke yake kwani kuna video sharing site nyingi sana na ambazo zinaweza kusaidia kwenye hiki kitu.

Kutoa packages za bure kwa baadhi ya celebrities ili waje Tanzania na kutembelea vivutio mbalimbali, hii itasaidia kwa sababu hawa watu wanaporudi na kukutana na media mfano Jay Leno, Letterman au Oprah tutapata free advertisements wanapokuwa wanaongelea trips zao.

Summer Festivals mbalimbali ni muhimu sana kwa bodi ya utalii kuhudhuria, kila kuna festivals kibao za ethnic groups na hata baadhi ya conferences. Mfano kuna German Fest, Summer Fest, Irish Fest, African Fest, Italian Fest na nyingine nyingi sana.

Kuweka Billboards barabarani along airports kubwa na karibu na Theme Parks kama zile za Great America, Wisconsin Dells, Disney, Mount Rushmore, Great Canyon, Las Vegas na sehemu nyingine kibao. Hapa kuna chances ya kupata baadhi ya tourists ukichukulia baadhi ya hizi parks zinajisikia kuwa hakuna haja ya kwenda Africa kwenye safari wakati wanyama wote wanao hapa.

Nadhani kuna umuhimu wa hawa madingi wengi ambao wako kule bodi ya utalii na wizarani kuajiri vijana ambao wataleta fresh ideas.

Hizo ndiyo njia zinazotakiwa; walete wao ndio watutangaze.
 
mie sipendi hata waje, wakija wakipenda sehemu wananunua, angalia zanzibar east cost yote,sijui paje ,bwejuu,jambiani na makunduchi,yani wanzungu tu wazungu na waarabu tu wamejazana pwani,halafu kila mtu akijenga anaweka na ukuta sasa kuta zinakutana tu,soon kutakuwa hata vijiuchchoro vya kuendea pwani hakuna, halafu labda sijui ama mnielimishe mtu kama mimi nafaidika na nini na utalii? hivi mnajua bei ya kiwanja cha kawaida pwani ya zanzibar,bwejuu kuna mtu kanunua sehemu dola lakio mbili na nusu embu niambieni mie nifanye nini hili nipate hizo pesa, nami nataka pia kaa pwani.
 
Jamani lini mtakuja kubali kwamba Tanzania tumeishiwa vivutio?.. Yaani hao wanyama na mlima Kilimanjaro imekuwa maajabu ya dunia toka miaka mingapi maanake sisi wengine tunazeeka bado wimbo ni ule ule wa Ujamaa na asili.
Kuna kila haja ya kubadilisha vivutio, kusema kweli mimi hata kama kuna Jurassic Park Tanzania bado nina hakika watu watakao visit hawatakuwa wengi kwa sababu kwanza inatisha.. Inatakiwa uwahakikishie usalama wao hasa ukizingatia kuwa nchi yenyewe maskini..
Ukweli utabakia kwamba hata tukiwa na wasomi wa namna gani ktk marketing bado watatangaza tu kile tulichokuwa nacho..Tanzania ya mkoloni bado ni ile ile haina jipya wakati nchi zote maskini leo hii zinatumia kila mbinu za starehe kuwavuta watalii ambao hukimbia makwao wakati wa baridi kali..
Ni vigumu mtu aliyefanya kazi ya nguvu mwaka mzima uje umpandishe mlima na kukaa porini ambako amefundishwa kwamba kuna kila aina ya maradhi kutokana na maji machafu. Ukisikia hesabu ya watu wanaokufa kwa Maleria na kadhalika yote haya yanachangia sana mtu kuamua kwenda kujirusha Thailand ambako hakuna mbuga wala milima kama Kili.
Nina hakika kabisa nchi kama Thailand inaingiza watalii kama wetu wa mwaka mzima, kwa mwezi au miezi tu...
Je, na sisi tujipange kama Thailand?.. sio lazima lakini muhimu tutazame ni vitu gani vinavutia watalii hasa toka nchi za Ulaya na kujenga misingi ambayo inatuwezesha kuwavuta..Haya ATCL ndio kwanza inakufa wakati tangazo la Airline tu linaweza kabisa kuonyesha maraha yanayoweza patikana Tanzania..
Tunayo Zanzibar, Bagamoyo ambazo ni sehemu za historia kubwa ya utumwa lakini leo hii tumefagia kila kitu..Ni sehemu muhimu sana kama zingeendelezwa kwa malengo ya Utalii.
Nina hakika kama sio Zanzibar, jinsi inavyojulikana nje basi bara tungepata shida kubwa sana kupata watalii kwani 2/3 ya Watalii wanaokuja Tanzania ni lazima wadai wanataka kufika Zanzibar, sasa sielewi Zanzibar wameweza vipi kujitangaza wakati sioni kabisa matangazo yao.
Again, kitu kinachouma hapa sio kuitangaza nchi yetu au wapi tunaitangaza isipokuwa ni hizo gharama tunayotumia kuitangaza nchi ambayo kifupi vivutio havijai mkononi.. Na ukija ambiwa pato la Taifa toka Utalii nguvu inakuishia..
 
- Hayo matangazo nimeyaona nikiwa majuu, ni saafi sana iwapo tu waliohusika wakatueleza hizo hela zilizotumika zimetuletea taifa hela ngapi back au in return, kutumika sio tatizo, tatizo ni tumepata ngapi back?

- Maana ndio the only way ya kuona kama the end justifies the means, sasa wapi more facts?
 
Field Marshall Es,
Mkuu hakuna kitu chochote, nina hakika hata Joseph Kusaga anaitangaza Tanzania vizuri kuliko hawa jamaa zetu na usije akaambiwa hata hao musician waliokuja TZ wametokana na matangazo ya CNN....
Nimeliona Tangazo na kusema kweli limenivutia tu kwa sababu mimi ni Mtanzania na nimesikia Tanzania ikitangazwa.. The same nikiona news zozote zinazohusiana na Tanzania lakini hakuna jipya bob la kumvutia Mtalii zaidi ya wanyama ambao anaweza kwenda Zoo akawaona wote.. Kuna zoo hapa inaitwa African Lion Safari basi wanyama aina zote tulizokuwa nazo tumewauzia hawa wazungu sasa waje Bongo kufanya nini wakati hiyo Zoo imetengenezwa utafikiria uko Serengeti!
 
Inavyoonekana hawa wizara ya Utalii hawajui kufanya umachinga.
Tofauti iliyopo kati ya dola 700 000 na 125 000 elfu ni kubwa mno hasa ukizingatia kwamba cnn na ABC zote zinapatikana nchi zote ulimwenguni.

Kama ku-spend kwenye Tv za USA ndo deal za kuwaleta walipa dola, Tanzania ikumbuke kwamba hawa sasa wana credit clunch na matangazo ya utalii yaelekezwe zaidi kwa nchi kama Japan, Singapore, China, Malaysia na Uarabuni ambao ni big spenders kuliko hawa 'so called white trash'.

Waende pia kwenye show nyingine za Arts na tourism exhibition centres ambapo wanaweza kujitangaza vema tu kwa gharama nafuu for maximum impact kuliko hizo CNN.

Ni hayo tu wakuu...
 
Ubuniufu ubunifu wa vivutio Watanzania, dunia ya sasa hata kama si kivutio unakipamba kinavutia... Tuache kulala na ushamba wa kufikiri. Watu wanaajiriwa kufikiri vivutio ni milima na mabonde na wanyama, more than that zerooooooooooooooo
By the way nani anataka kuliwa na mamba, simba nk? Those were old stories The Prey we need more.
Hivi Tanzania huwa hakuna watu zaidi ya wale ndugu zangu wanaotumiwa kwa utalii? Maana matangazo yote ni pori na wazee wa pori au ufukwe na ngalawa zake. Flora and Fauna je? How about film industry to boost tourism industry?
 
By Jenerali Ulimwengu

KATIKA makala za hivi karibuni nimekuwa nikijadili masuala yahusuyo elimu kwa sababu naamini kwamba elimu iliyoratibiwa vilivyo na yenye maudhui ya kimaendeleo ndiyo njia pekee ya kutuondoa katika umasikini ndani ya kizazi kimoja au vizazi viwili.

Elimu ya aina hiyo (pamoja na afya) ndiyo imekuwa tofauti baina ya nchi za Kiafrika na zile za Asia, ambazo wakati tunapata Uhuru zilikuwa sawa sawa na nchi zetu lakini leo zimetuacha mbali. Ukweli ni kwamba nchi kama Malaysia, Korea ya Kusini na Indonesia ziliwekeza katika maarifa na siha ya watu wake wakati sisi tuliwekeza, ama kwa kutokujua ama kutokujali, katika ujinga na maradhi.

Napenda kuamini kwamba hatujachelewa sana, ingawaje hata wakati huu tunaposherehekea miaka 47 ya Uhuru bado sioni mwelekeo wa wazi wa kujikosoa katika jinsi tunavyoenenda. Kwa jinsi tunavyoenenda tutatimiza miaka 50 tukiwa bado tunasuasua, na tusipoangalia nusu karne nyingine ya upuuzi itatukuta bado tupo hapa hapa tulipo au tumerudi nyuma.

Wakati tunaitafakari elimu yetu hatuna budi pia kufanya tafakuri ya dhati juu ya kipengele kingine ambacho kinaambatana na elimu katika kumjenga Mtanzania wa karne hii: Afya.

Miaka 47 iliyopita, wakati Tanganyika inapata Uhuru nilikuwa mtoto wa darasa la saba, na nakumbuka jinsi tulivyoelezwa na Mwalimu Julius Nyerere na viongozi wengine wa wakati ule kwamba tulikuwa na maadui wakuu watatu: Umasikini, Ujinga na Maradhi.

Naamini maadui hawa bado tunao, na katika maeneo kadhaa wamekuwa wakali zaidi na wanazidi kututeketeza. Haielekei kama jitihada zetu zimezaa matunda ya kuridhisha, na mara nyingi watawala wetu wanaonekana kama watu wasiokuwa makini katika kuwashughulikia maadui hawa.

Watawala wetu, ama wanawatomasatomasa maadui juu ya magamba yao bila kuwaingia katika undani wao au wanatumia nguvu nyingi mno na maarifa kidogo mno katika kukabili matatizo ambayo yanahitaji tafakuri ya kina kabla ya harakati na mikurupuko.

Sina haja ya kurejea nilichoandika hivi karibuni kuhusu ‘madarasa' yasiyokuwa na waalimu, isipokuwa inawezekana pia kwamba tutajenga zahanati na vituo vya afya visivyo na waganga wala wauguzi.

Hebu tufikiri tena, na labda katika tafakuri yetu turejee misingi tuliyofundishwa, si tu na Mwalimu Nyerere, bali na ukweli unaojidhihirisha katika historia ya dunia katika karne iliyopita, historia ambayo hadi leo tunashuhudia ikiandikwa.

Nchi nilizozitaja hapo juu zilitambua yale yale aliyotufundisha Mwalimu: Maendeleo ya jamii huletwa si kwa kujenga vitu bali kwa kuwajenga watu, na kuwajenga watu ni kuwapa vitu viwili muhimu, elimu na afya. Ndivyo walivyofanya wenzetu wa zamani niliowataja hapo juu ambao leo tunashangaa jinsi walivyotuacha kimaendeleo.

Katika makala zangu za Aprili 1995 nilikumbushia msemo maarufu wa Kilatini, Mens sana in corpore sano (Akili Safi Ndani ya Mwili Imara). Msemo huu unaweza kutafsiriwa kwa maneno mawili: Elimu, Afya. Jamii inayoshindwa kulielewa hili haiendi ko kote.

Ndiyo maana nilishituka niliposoma mahojiano kati ya Rais Mteule wa Jamhuri Benjamin Mkapa na mwandishi (sasa marehemu) David Martin mara tu baada ya uchaguzi wa mwaka 1995 kabla Mkapa hajaapishwa. Alipoulizwa ni katika sekta zipi angetoa kipaumbele, Mkapa alizitaja sekta za madini na utalii, jambo ambalo kwangu mimi lilidhihirisha kwamba tulikuwa na tatizo la msingi.

Dunia ya kisasa (na ya wakati ule), bila kujali mielekeo ya kisiasa na kiitikadi, inatambua (na ilikwisha kutambua wakati ule) hatari za nchi yo yote kutegemea uchumi wa ‘chimba-ondosha,' nikijaribu kupata tafsiri ya ‘extractive industry' ingawaje mbali na uchimbaji dhana hii inaweza kuhusishwa pia na ukataji wa magogo, uvuvi wa samaki na kadhalika.

Leo hii tunashuhudia malumbano makali miongoni mwetu kuhusu uchimbaji huo ambao wengi wanauona kama uwanja wa utapeli na uuzaji wa rasilimali za nchi unaofanywa na watu waliokabidhiwa madaraka kuitumikia nchi yao. Lawama hii Mkapa hawezi kuikwepa, hasa kwangu binafsi kwa sababu nilipata wasaa wa kumweleza na hakuwa na majibu ya kuridhisha isipokuwa tu kuniuliza hizo fedha za kuwekeza katika elimu na afya zingetoka wapi.

Uwekezaji ni uwekezaji, na una gharama zake. Kuwaruhusu wageni waje wachimbe-waondoshe huku wakituachia mashimo matupu na ardhi iliyochuja si uwekezaji ni wendawazimu. Hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa uchumi atakwambia hivyo.

Uwekezaji katika elimu na afya ya watu wetu ni uwekezaji wa kweli kwa sababu kilichowekezwa kinabaki nchini na kinakuwa kimeongezwa thamani kubwa na isiyoondosheka. Raia wenye elimu bora na siha imara ni vito vya thamani ambavyo haviwezi kulinganishwa na dhahabu, almasi wala mafuta ya peteroli, vitu ambavyo wakati mwingine vinakuwa chanzo cha vita miongoni mwa wananchi wajinga chini ya watawala walafi.

Hebu tuangalie mifano ya nchi mbili katika eneo letu. Zimbawe inakiona cha mtema-kuni kutokana na ufisadi wa ajabu wa mzee mwenye ugonjwa wa akili. Lakini siku moja ataondoka kwa sababu hata wendawazimu hawaishi daima. Zambia imekuwa na uchumi ‘mzuri' kwa miaka kadhaa sasa lakini wakati ninaandika makala hii habari ni kwamba bei ya shaba imeshuka vibaya mno na kwamba Zambia na DRC zinalazimika kuwaachisha kazi maelfu na maelfu ya wafanyakazi.

Utabiri wngu? Mara yule mzee mwendawazimu atakapoondoka (kwa hiari au kifo) na Wazimbabwe wakajipanga upya wataiponya nchi yao na kuirudishia neema haraka zaidi kuliko watakavyoweza kufanya Wazambia. Sababu? Pamoja na mambo mengine yote, Zimbabwe iliwekeza katika rasili-mali watu, ambao wanachohitaji pekee ni fursa ya kurejea nyumbani. Zambia watakuwa na mashimo mengi, makubwa.

Kama tutakubali kwamba uwekezaji katika elimu na afya ni wa msingi, basi tuikubali ankara yake tukijua kwamba matunda yake yatakuja, na hatuhitaji kusubiri zaidi ya vizazi viwili kabla hatujaona matokeo yake.

Hata tungekopa matrilioni ya dola za Marekani na tukaziwekeza zote katika elimu na afya ya watoto wa nchi hii, hao watoto watakaonufaika na programu hiyo watawezaje kutulaumu kwa kuwaachia deni ambalo linatokana na maendeleo yao ambayo watakuwa wanayaona?

Sasa, nini ni bora kati ya deni la aina hiyo na yale mashimo tunayoyaona huko tulikoruhusu ‘uwekezaji' wa kijuha. Ningependa iwepo fursa kwa watoto wa maeneo hayo kuwauliza watawala wao walikuwa wanafikiri nini wakati wakiwaleta ‘wawekezaji' hao.

Lakini bahati ya watawala wetu ni kwamba wakati maswali hayo yanaulizwa watakuwa wamekufa au wameikimbia nchi. Hapa ndipo itabidi lifanyike zoezi alilolieleza Mwalimu Nyerere, la kufukua maiti zao na kuzichunguza bongo zao ili kujua kama kweli walikuwa na akili timamu.

Kilicho dhahiri ni kwamba watawala wetu wanapenda kufanya ‘uwekezaji' katika mambo ya haraka haraka, yatakayoonyesha faida kubwa mara moja, kimsingi kwa sababu, moja, hawana ‘vision' ya muda mrefu, na pili, wanataka matokeo ya papo kwa papo kwa sababu watanufaika binafsi, kisiasa na kimali.

Tumegeuka nchi isiyoweza kufikiri nje ya vipindi vya miaka mitano kwa wakati mmoja, kwa sababu kinachotafutwa ni madaraka ya kisiasa ambayo yanampa aliyenayo nafasi ya kuiba. Kwa hiyo kila aina ya juhudi, halali na haramu, inaelekezwa katika uchaguzi, na baada ya uchaguzi mmoja yanaanza maandalizi ya uchaguzi unaokuja.

Kwa chama-tawala ndiyo kabisaa, na wala si miaka mitano. Angalia hii: 85 uchaguzi; 87 uchaguzi; 90 uchaguzi; 92 uchaguzi; 95 uchaguzi; 97 uchaguzi; 2000 uchaguzi; 2002 uchaguzi; 05 uchaguzi; 07 uchaguzi; 010 uchaguzi; 012 uchaguzi; 015 uchaguzi; 017 uchaguzi; 020 uchaguzi…

Laiti kama nusu ya muda, nishati na fedha zinazowekezwa katika chaguzi hizi zisizo na mwisho zingeelekezwa katika elimu na afya ya watoto wa nchi hii Tanzania ingekuwa nchi tofauti kabisa. Lakini huko siko yaliko maslahi ya wakubwa.

Itaendelea

Priority priority...
 
Matangazo ya Tanzania hayajaifikia Jamaica, kwa costs. Jamaica pamoja na kwamba inajulikana kukiko Tanzania, pamoja ni kuwa ni nci ndogo kuliko Tanzania, lakini inatumia fedha nyingi sana kwenye kutangaza utalii wake ambao sio kingine bali ni beaches ambazo hazijafikia viwango za beaches kama za Brazil.

Swali ni Matangazo yanalipa?, Jibu ni Yes BIG TIME YANALIPA. Watoa hoja hapa ambao wanapinga matangazo hayo wangekua wanamiliki Nike, sijui wangechanganyikiwa kiasi gani, Nike pamoja na kuiningia mikataba na wanamichezo wengi, ni inategemea matangazo sana, "Siwezi ku-prove", lakini kuwalipa wakina Jordan, Tiger Woods, etc Mamilion ya dola unaweza kutoa hoja kuwa katika culture ya sasa karibu watu Bilion 4 wanategemea TV iwaonyese service au product ili waweze kununua.

Kama 100 millions ya wamarekani wanapenda actions za Serengeti, Animals, Ngorongoro, Lions, Safari Zanzibar Beaches, Big Cat Stories etc lakini hawajui hizi actions zinapaticana Tanzania, itakuaje kusita at least kutumia USD 40millions (sawa na hela aliyopewa 50 cents kuuza maji ambaye ana-afect kama 20 milions drinking water consumers), kua-affect /to get at least 1% of that population.

In today economy I believe in three things, 1.Capitalism, 2.Marketing(advertising) 3.Sales over Cost.
 
But was it a worthwhile undertaking? 1.3bn kwa utangazaji-there must be something wrong with our priorities!!

matangazo ni kitu muhimu sana. katika biashara yeyote na nchi kujulikana. ni lazima hili tendo tulisifu na aliyeanzisha tumsimfu. na kwasababu ni mara yetu ya kwanza kunaweza kukawa na shida kidogo. Qualty ya matangazo na kuongeza maeneo ya nafuu ili kutoa matangozo mengi kwa muda mrefu.
kwa kusema 1.3 bill ni nyingi sio nyingi kumbuka hutangazi chang'ombe unatangaza ulaya na marekani. Na hawa ndio watalii. Uchumi umedorora huu ndio wakati muafuka wa kutangaza kwani watu wengi wanaangalia TV kuliko kipindi chochote, na ukumbeke nchi za ulaya na marekani watalii wengi ni wazee waliostaafu na baadhi ya vijana. na hufanya utalii kwa bajeti ya muda mrefu. for me it is good timing but just add some more creativity on our add. matunda huja taratibu kumbuka hii ni biashara ya nchi so is a long term goal.
 
Kutangaza nchi yetu ni jambo zuri sana, na nimuhimu. Hata hivyo, tukumbuke tena maneno ya Nyerere kuwa "We must run while they walk......"

Sisi tumechelewa sana kiasi kuwa majirani zetu ndio wanaojulikana kumiliki hivyo vivutio tunavyotangaza. Kwa hiyo matangazo yetu mengi yanaweza kuwa yanaonekana kama vile ni kanyabwoya tu, yaani tunawaambia njooni muone Kilimanjaro wakati wao walishaambiwa siku nyingi kuwa Kilimanjaro iko Kenya. Tunahitaji juhudi kubwa sana, ndiyo maana mawazo ya kuwaleta watu wao mashuhuri ndio watusaidie kutanganza mimi naona ni mazuri na ndiyo njia ya haraka kurekebisha makosa hayo ambayo sasa ni ya kihistoria. Kama tutategemea kutangaza wakati Kenya nao wanaendelea kutangaza vivyo hivyo, tena very effectively wakisaidiwa na historia iliyokwisha jengeka, tutakuwa tunatwanga maji kwa kinu tu.

Jioni hii nilikuwa naangalia huu wimbo wa Priva na Q-Chilla pale You-Tube, nikaona una label ya Kenya.org, nikasem dah!!!, wenzetu wako haraka sana kuvutia kwao.

[media]http://www.youtube.com/watch?v=Xt9uGRwF1VM[/media]
 
Mazee hiyo Kenyan.org ni site tu ya mtu binafsi(mkenya) ambaye ameamua ku-watermark video zake anazozi-upload pale Youtube kwa dhumuni la kutangaza tovuti yake, faida iliyokuwepo ni kutokana na hiyo site kutumia jina la nchi kwa hiyo kuweza kuitangaza Kenya na wakati huohuo kuitangaza tovuti yao.
 
inavyoonekana hawa wizara ya utalii hawajui kufanya umachinga.
Tofauti iliyopo kati ya dola 700 000 na 125 000 elfu ni kubwa mno hasa ukizingatia kwamba cnn na abc zote zinapatikana nchi zote ulimwenguni.

Kama ku-spend kwenye tv za usa ndo deal za kuwaleta walipa dola, tanzania ikumbuke kwamba hawa sasa wana credit clunch na matangazo ya utalii yaelekezwe zaidi kwa nchi kama japan, singapore, china, malaysia na uarabuni ambao ni big spenders kuliko hawa 'so called white trash'.

Waende pia kwenye show nyingine za arts na tourism exhibition centres ambapo wanaweza kujitangaza vema tu kwa gharama nafuu for maximum impact kuliko hizo cnn.

Ni hayo tu wakuu...

wizi mtupu!!!!
 
Unajua hapa lazima tuangalie faida na hasara;tujiulize kwa gharama hiyo waliyotumia kutangaza kwa miezi sita katika hiyo miezi sita sisi tumeingiza kiasi gani kama tumefaidika tuendelee kutumia hayo matangazo katika vyombo vingine vya habari pia.
Ila kama tumepata hasara ni bora tutumie njia za kuhudhuria maonyesho(festivals&Arts exhibitions) halafu balozi za TZ zitumike,mtandao/internet pia.
Walichosema wao baada ya kutoa taarifa hiyo ni kwamba bodi hiyo sasa itatilia mkazo zaidi utalii wa ndani kuliko utalii wa nje ili kupunguza gharama zinazotokana na matangazo nje ya nchi.
Kwahiyo inaonekana hiyo option waliochukua hailipi.Hivyo tumepata hasara zaidi kuliko faida;basi naomba watumia njia nilizoainisha hapo juu.
 
Kutoa packages za bure kwa baadhi ya celebrities ili waje Tanzania na kutembelea vivutio mbalimbali, hii itasaidia kwa sababu hawa watu wanaporudi na kukutana na media mfano Jay Leno, Letterman au Oprah tutapata free advertisements wanapokuwa wanaongelea trips zao.

Summer Festivals mbalimbali ni muhimu sana kwa bodi ya utalii kuhudhuria, kila summer kuna festivals kibao za ethnic groups na hata baadhi ya conferences. Mfano kuna German Fest, Summer Fest, Irish Fest, African Fest, Italian Fest na nyingine nyingi sana.

Kuweka Billboards barabarani along airports kubwa na karibu na Theme Parks kama zile za Great America, Wisconsin Dells, Disney, Mount Rushmore, Great Canyon, Las Vegas na sehemu nyingine kibao. Hapa kuna chances ya kupata baadhi ya tourists ukichukulia baadhi ya hizi parks zinajisikia kuwa hakuna haja ya kwenda Africa kwenye safari wakati wanyama wote wanao hapa.

Nadhani kuna umuhimu wa hawa madingi wengi ambao wako kule bodi ya utalii na wizarani kuajiri vijana ambao wataleta fresh ideas.

Good ideas. If only the people in charge had more creativity and vision. Or is it just laziness and poor leadership.
 
Back
Top Bottom