Bili yamponza aliyejirusha ghorofani....................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bili yamponza aliyejirusha ghorofani.......................

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 1, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 69,661
  Likes Received: 3,134
  Trophy Points: 280
  Bili yamponza aliyejirusha ghorofani

  Imeandikwa na Oscar Job; Tarehe: 31st December 2010 @ 23:5


  KIFO cha mwanamke anayedaiwa kujirusha ghorofani juzi kilitokana na yeye kujaribu kukimbia bili ya vinywaji na vyakula akiwa na wenzake kwenye baa iliyoko ndani ya jengo la Benjamin Mkapa Tower.

  Mwanamke huyo alianguka kutoka ghorofa ya tatu na kupasuka kichwa na kuvunjika mkono akikwepa kulipa Sh 95,000 alizokuwa akidaiwa, Polisi imesema.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alisema jana kuwa marehemu ambaye hadi sasa hajatambuliwa jina, aliingia katika baa ya Savanna ghorofa ya tatu akifuatana na rafiki yake wa kiume na dereva teksi aliyewapeleka hapo.

  Alisema akiwa hapo na rafiki yake huyo ambaye pia hajajulikana na dereva teksi huyo, walikunywa vinywaji mbalimbali na kula kuku hali hata kutakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha.

  “Baada ya hapo wahudumu walisema mwanamume alijifanya kwenda chooni na kutokomea
  huku nyuma wenzake wakimsubiri,” aliongeza.

  Inadaiwa mwanamke huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 30 na mwenzake waliosalia walitaka kuondoka, lakini uongozi wa baa hiyo uliwazuia mpaka walipie vinywaji na chakula.

  Kwa mujibu wa Shilogile, hali hiyo ilisababisha malumbano na ndipo mmoja wa wafanyakazi wa baa hiyo alipomdhamini dereva kwa kumlipia Sh 42,000 huku marehemu huyo akitakiwa kulipa Sh 43,000 zilizosalia.

  Kutokana na kutokuwa na fedha, alianzisha malumbano huku akiondoka kwenda nje ya baa huku akifuatiwa na walinzi, lakini kabla hajafikiwa, alijirusha chini ya ghorofa na kufariki dunia.

  Aidha, alisema kwa sasa Jeshi lake linaendelea na upelelezi kumtafuta mwanamume aliyekuwa naye huku likisaidiwa kwa karibu na dereva teksi huyo kwa madai kuwa huenda akawa anamfahamu.

  Alisema mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili kwa kuwa bado haujatambulika na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 69,661
  Likes Received: 3,134
  Trophy Points: 280
  Mpaka unamdhamini huyo dereva yaonyesha muhudumu huyo wanafahamiana naye...........................vinginevyo ingelikuwa ni vigumu............
   
 3. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Polisi waangalie uwezekano wa walinzi kumsukuma au kumfukuzia eneo lisililokuwa imara. Haiingii akilini mtu ajirushe kirahisi hivi.
  Kwani hiyo Hotel haina CCTV cameras?
   
 4. m

  mzambia JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 875
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwani kama unadaiwa bili ndo ujiue? Haiingii akilini
   
 5. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Stori hii haijakaa vizuri; huyu dereva teksi inaonekana alikuwa na uhusiano wa karibu na yule bwana aliyekacha, kwasababu siyo kawaida kwa dereva teksi kukaa meza moja na wale waliomkodisha. Kama hivyo ndivyo inakuwaje ichukue muda mrefu kubaini huyo aliyekimbia. Kwa upande wa marehemu, mpaka huyo dereva inafika hatua ya kumdhamini, bila shaka mvutano kati ya wahudumu na mlinzi wa baa hile kwa upande mmoja, na hao wateja kwa upande mwingine ulikwisha kuwa mkubwa; katika hali hiyo ni vigumu kuamini, kuwa mama huyo angeliweza kutoka nje yeye mwenyewe bila ya kuwa chini ya udhibiti wa mtu.
   
 6. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 7,346
  Likes Received: 446
  Trophy Points: 180
  hapo umenena,
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,366
  Likes Received: 1,347
  Trophy Points: 280
  Mbaya! Hizi 'ofa' ni noma sana.
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,082
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hao wote wanajuwana, kuanzia marehemu, mhudumu, dereva na jamaa aliyeondoka. Hapo kuna kamchezo kamefanyika na kakaingia dosari.
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,082
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Halafu hizo hesabu mbona hazi tally? Bili ni 95,000 na dereva 42,000 + marehem 43,000 jumla 85,000, vipi?
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,271
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Maelezo ya post #1 ni wazi kwamba huyo shori ameuawa na ukweli unafichwa.
  Walinzi na wahudumu wanapaswa kuhojiwa. Polisi watumie teknolojia kubaini tukio zima...
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 55,686
  Likes Received: 20,326
  Trophy Points: 280
  Uwezekano mkubwa huyu ameuwawa. Haingii akilini mtu kujirusha kwa pesa kidogo kiasi hicho.
   
 12. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #12
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyo atakuwa alilewa mpaka kufikia uamuzi huo.
   
 13. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,949
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  hajanena lolote la maana hapa. Kuna yote mawili. Anaweza kuwa karuka mwenyewe, ulevi mnaujua. Inaweza kuwa kaanguka kwa bahati mbaya. Pia huyo taxi driver ni lazima ni mtu wao wa karibu pale bar na pia kwa wateja wake hao. So, watampata. Na huyo bwana alietoroka yaweza kuwa walimuudhi au alihisi ukaribu wa dada yule marehemu na dereva taksi na ndo maana ya kupata hasira na kuwaacha na bili yao na kumbe hawakuwa na hela. Dada zetu nao wamezidi kuchuna jamani. 95000 kwa mtu mwenye family ni nyingi. Duh!
   
 14. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,949
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Nani kakwambia 95000 ni kidogo? Huo ni mshahara wa mtu wa mwezi ndugu yangu. Yaweza kuwa ni ndogo kwako na baadhi ya watu ila siyo wote. Pili kuna swala la kudhalilika. Hatujui huyo dada alikuwa popular kiasi kipi hasa hapo bar. Ni mawazo na maamuzi rahisi kwa bin adam hasa akiwa na laga kichwani. Mungu ilaze roho ya marehemu pema peponi. Amina
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,809
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  kuna uwezekano kajiua, sometimes pombe zinakufanya usahau kwamba uko ghorofani yeye akadhani yuko bar zetu za uswazi....

  Sina hakika kwamba ni murder
   
 16. e

  ejogo JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapa uwezekano mkubwa ni wa kurushwa na kilevi alichopata.
   
 17. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,889
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Uchunguzi wa madaktari uko vipi?unaweza kuta alipigwa chupa na kubakwa halafu wakamrusha ili ionekane kajirusha,wanahitajika wataalamu wa maswala ya uchunguzi.
   
 18. P

  Pretty P Senior Member

  #18
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 110
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  jamani tatizo wadada wenzangu hawatumii akili. We unakwenda out huna hata single cent yakujitetea loo! Jamani ni mbaya. Uchunaji mbaya sana
   
Loading...