Bilcanas ya Mbowe inaondolewa vyombo sasa

Bilcanas ya Mbowe inaondolewa vyombo sasa

Kumbe wakwepa kodi tulikuwa nao humu humu kwenye safari ya mabadiliko na matumaini? Sipati picha chadema ingeshinda uchaguzi!
 
kwahiyo udj ndo basi?
Jamani mbona munang'ang'ana na u-dj. Kweli huo ni mradi mbaya kiasi hichooo! Mbona kuna viongozi hapa walisikika sana kwa kuuza madawa ktk utawala uliopita na hamuwataji tena. Au madawa ni kazi ya kishujaa? Lukuvi alijibu nini bungeni kuhusu kuwataja wauza madawa?

Let's be ethical and objective. Tukiwa JF tuachane na ushabiki wa karume stadium. yaani iwe ni zomea-zomea tuuuuuuu! Elimu ni vazi la akili
 
Jana Kuna post niliweka nikasema Bilcanas inaondolewa.. Akaja member mmoja akasema ni Ofisi za Gazeti la Tanzania Daima.. Nitakwambia labda hakusikiliza Mpaka mwisho wale Wakaka wa NHC wa kuondoa Mali kwenye majengo ya Watu wanaowadai walidai anadai wa kote Na ni zaidi ya Bilioni 1 Na wakitoka Hapo wanapenda Na huko.

Sasa mnaofatilia issue hii ulizieni Vyombo vinatolewa Na Bilcanas.Nimerudia kuandika Baada ya ule Uzi kuondolewa ikionekana nimeongopa.Na pia Sikuandika kwa Hisia Bali why Mbowe kwa kasi hii Na kwa wakati huu..Ivi Shirika kama NHC Mpaka izo MHL zifikishe 1B walikuwa wapiii..

Na mbona Hata Kuna majengo ya Watu wa Kijana wanadai wa zaidi Na Hata majengo waliokodisha serikali ni wadaiwa sugu tena zaidi ya hayo..Na wamekiri wao wenyewe kwamba wapo wengi Na serikalini ila tunaanza Na Mbowe..

Kama wao ni wazalendo kwa nini wasionyeshe Mfano wa Majengo waliokodisha serikali yanayodaiwa zaidi ili tuone Utendaji wao mzuri???
Mshauri alipe. Wizara ya habari ilifurumshwa. Kwa hiyo km wizara ya serikali ilifukuzwa, kwa nn nhc isite kwa mbowe? Sheria ni msumeno.

Pia mbowe ameishi kijanjajanja kwa kufungua kesi ili asifukuzwe
 
Watu wanasubiria serekali ya viwanda muwekezaji gani ataleta pua yake Kuwekeza Tanzania. Wakati serekali inapambana kuwadidimiza wawekezaji.

Huwezi mdanganya ata mtoto kuhusu swala la kodi kufika bil+ . hiyoo iko wazi ni mchezo mbowe kachezewa leo kwake kesho kwako.
 
Nikusaidie kitu kidogo..mimi natumia smartphone... Sometimes nakuwa nimeandika sawa lakini herufi inajibadili nikishatuma but Kuna njia ya kuzuia kama kuangalia maneno yanayojiandika Hapa kati kati ya Simu kama unatumia Simu ya Tochi huwezi elewa nina maanisha nini..Lakini ninachoshukuru ni Ujumbe kufika kama nilivyotazamia.Aksante.
nimekuelewa kaka. ahsante.
 
Matusi ya nini ndugu kudaiwa ni kudaiwa tu alipe kodi ya serikali,kweli ndio viongozi tuliokuwa wanataka kupewa nchi kweli?????????

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
Hapo sasa. ...mtu unamwambia ukweli baada ya kukaa na kufikiri na kuwa mzalendo, anakuja na mitusi, ovyo kabisa. Bilicanas ni biashara kubwa inamaanisha muda wote since 1993 ana operate bila kulipa kodi? Jamani hebu tuache masihara. ..huyu mtu anaitakia hii nchi mema kweli? Hebu amkeni mlio LALA
 
Una habari kwamba serikali yako hiyo hiyo inadaiwa Matrilion...Kwa nini hawalipi.wajabaki hawana deni..kifupi Hapa juu ya jua Hakuna asiyedaiwa.Hapa Kuna mkono wa MTU. halafu hao Watu wa kijani wanavyodaiwa Mbowe cha Mtoto mchanga ila kwa kuwa hujui kitu unaropoka tu Hapa..Hapa ni Kukomoana..kwanza kesi IPO mahakamani miaka Na miaka ..subirini mtaona atakavyolipwa fidia..Na kama hujui hizo Nyumba za NHC sio nyumba za kodi kubwaa kiasi kwamba Bwana mkubwa ashindwe kulipa kwa wakati..Walimwanzishia zengwee ili ashindwe kulipa...Mfano.mzuri ni wa Maduka ya mwanza stendi toka kodi ya Elfu 20 kwa mwezi wakawapandishia Mpaka laki 2 kwa mwezi..So you can imagine how it is..stop judging him wait and see.
Mkuu sio swala la mkono wa mtu,ni srategies za kazi tu,watu wakitaka kurahisisha kazi zao hupenda kuwatumia watu mashuhuri kama role models,kama watu wanakwepa kulipa kodi ukimbananisha mtu mashuhuri ambae watu wanaamini hawezi kuguswa ni rahisi wengine kujiuliza kama huyu kabonyezwa maana yake hakuna atakayeachwa na watachangamka kulipa tu,na wala usiwapangie waanze na kigogo yupi.Kama wewe una umashuhuri wako uchwara muhimu ni kupita kwenye mistari iliyonyooshwa ili usifanywe role model kwenye mambo ya hovyo hovyo.Watu wa aina yako ndio wale ambao unaona kabisa mtu amekufa kwa kipindu pindu tena kwa taarifa ya daktari lakini badala ya kuweka mkazo kwenye kusafisha mazingira wewe unakomaa kusema kuna mkono wa mtu....watu wataendelea kupukutika kwa kipindupindu.
 
Back
Top Bottom