Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,417
- 133,784
Mkuu Kokola, asante kwa hoja murua kuzungumzia harakati za uhuru bila mrengo wa udini.Bwana Mohamed Said "upuuzi" hapa halikuwa tusi ni kinyume cha hoja yenye mantiki ile isiyo na maana ndio upuuzi sio tusi kamwe!! We ndugu yangu nilichosema mimi sio kuwa hatupendi au hatuwaenzi wapigania uhuru wetu la hasha!! Tena ifike mahali wapewe hadhi ya manabii wetu lakini katika context ya Utaifa na sio udini au ukabila Kaka!! Waikela kama yeye ni shujaa wa kumtoa mkoloni kwangu na naamini kwa Watanzania wengi ni mtu muhimu sana bila kujali dini yake au kabila lake. Hapo pia, haitegemei kutembelewa kwake na "mwanasiasa kijana aliye mashuhuri - Zitto Kabwe". Historia yetu imeandikwa na wageni sisi ndio sasa tunaamka kama anavyotaka kuamka rafiki yangu Paskali. Kama hao mashujaa hawakuthaminiwa au hawakutanjwa kwenye historia basi isiwe kuwa tuone ni kwa ajili ya dini zao bali tu kwa ajili ya kile walichokuwa wanakipigania ambacho mgeni alieandika historia hakukipenda. Wewe kama kijana wa sasa rekebisha ukisisitiza Utaifa na sio udini.
Mkuu hii ya wasabato kuwa na shule nyingi kuliko makanisa mengine wakati wa Uhuru nao ni historia mpya kwangu, unaweza kuileza kwa mifano kwa kuangalia zilizokuwa shule za kisabato, kiislamu ,kiroman catholic ,ki Luther walau tuone picha halisi?Hili suala naona watu mnalipeleka kwenye udini.kwani kama waislamu walishiriki kupigania Uhuru wetu,je kulikuwa na makubaliano waliyowekeana kwamba baada ya Uhuru waislamu wapewe upendeleo na nchi hii iwe na sheria za kiislamu?
Kama hakukuwa na makubaliano lawama za waislamu zinatoka wapi.tukumbuke pia harakati za Uhuru sio kweli kwamba wakristo hawakushiriki kabisa walishiriki mfano ni Mwl Nyerere.
Wakati tunapata Uhuru kanisa la wasabato Tanzania ndilo lililokuwa na mashule mengi kuliko makanisa yote hapa Tanzania wakati huu.
Serkali chini ya mwalimu Nyerere ikazitaifisha shule zote za kanisa LA wasabato na kuzifanya za serkali.mbona wasabato hawalalamiki kwamba wanaonewa na serkali. Ebu tuweke utaifa Mbele tuache udini
Boywise,Shukran Mzee wangu Mohamed Said, na kuhusu kitabu ninacho na nimetoa tongotongo nyingi sana kunako historia ya nchi yangu
Binafsi nilielekeza swali hili kwa peterwapeter ili anishibishe kunako hoja yake aloijenga kwa kudhani juu ya mada yetu
Wewe utamaduni wako ni upi?Tena dini zenyewe bora hata zingekuwa zetu kweli.
Zote za kuletewa na meli.
Zote zina mambo tofauti sana na tamaduni zetu.
Na tumezibugia kama mtu mwenye njaa kwenye dhifa.
Maalim Muhammed Said, hoja ya Kokola iko very valid kwa hoja tuwazungumzie wapigania uhuru kama wapigania uhuru bila kuwanasibisha na udini kwa kutaja dini zao.Kokola,
Wala sitakulaumu kwa kuona neno ''upuuzu,'' si tusi na mara nyingi
lugha mfano na hii yako nakutananayo hapa jamvini.
Kwetu siye hilo ni tusi.
Ingekuwa mimi ningeweza kuandikia sentesi hiyo hiyo bila ya kutumia
neno, ''upuuzi.''
Tofauti kati yangu mimi na wewe ni kuwa mimi kwanza ingawa hii nini
historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kubwa ni kuwa historia hii
imewahusu wazee wangu.
Kwa ajili hii basi mimi nayajua mengi ambayo wewe huyajui.
Ukweli ni kuwa palikuwapo na bado ipo njama ya kuifuta historia hii
na laiti kama nisingeliandika historia hii mengi yasingejulikana.
Hili la Uislam katika historia ya TANU huwezi kuliepuka hata ukifanya
nini kwa kuwa ndiyo historia yenyewe ilivyokuwa na mifano iko wala
si ya kutafuta.
Waasisi wa African Association 1929 ndiyo hao walioasisi Al Jamiatul
Islamiyya Fi Tanganyika 1933.
Al Jamiatul Islamiyya ndiyo iliyotoa viongozi wa mwanzo wa TANU na
wanachama wake.
Mimi sijaona ubaya wowote katika kuandika historia hii.
Idd Faiz Mafungo kadi yake ya TANU ni No. 25 na yeye ndiye alikuwa
mweka hazina wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika na pia mweka
hazina wa TANU.
Idd Faiz ndiye aliyekuwa mkusanyaji wa fedha za kumpeleka Nyerere UNO
mwaka wa 1955.
Umepata popote kumsikia akitajwa?
Mkuu AlwatanKwa watu wanaotaka kujenga umoja wa kitaifa, kuanza kuwagawa Watanganyika kwa mafungu ya kidini ni kuharibu umoja wa kitaifa.
Unawaambia wao si wamoja. Kuna waislamu na wakristo.
Sasa hapo kwenye waislamu napo aje mtu aandike kuhusu mchango wa Shia. Wa Shia nao watuambie Wa Ismaili na Zaydi nao walikuwa na mchangi wao tofauti.
Mimi naamini katika kuandika historia, maadam kilichoandikwa ninkweli, lakini naamini pia kwamba unaweza kuandika historia ikaleta kupinda ukweli.
Hususan kama historua yenyewe imekitwa kwenye hizi "imagined realities" za dini za kutungwa.
Hapo ndipo mnapowapa msemo wale watu wanaosema kwamba nia ya Uislamu ni kutawala dunia na popote pale ambapo uislamu haujatawala, utataka kunung'unika na kuua mpaka utawale.
Kwamba mnanung'unika sio kwa sababu mmeonewa (Wasabato wameonewa, makanisa yamenyang'anywa shule etc lakini hatuwasikii wakilalamika kama nyinyi) ila mnalalamika kwa sababu mmefundishwa kuchukua nchibkwa upanga na kueneza dini dunia nzima kama ilivyoenea kutoka Uarabuni mpaka Spain.
Mimi utamaduni wangu ni kutafuta ukweli, dini yangu ni mapenzi.Wewe utamaduni wako ni upi?
Paskali,Maalim asante, sana sasa nimeelewa, kumbe ilikuwa ni Presidential Preventive Detention Order. Hii kitu iliwahi kumkuta Mzee wangu Andrew Mayalla (RIP) aliyekuwa RSO wa Mwanza. Nyerere kiukweli alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo, alikuwa hataki kabisa ujinga ujinga wa aina yoyote. Sisi Wakatoliki tuko kwenye mchakato wa kumtangaza Mwenye Heri ambayo ni daraja moja kabla hajawa Mtakatifu. Naomba tukimtaja Nyerere popote, tumtaje kwa kutazama only the bright side of him and not the dark side isije kuchelewesha mchakato wetu.
Paskali
Utamaduni wenu unaosema ni tofauti na huo wa hao unaona wameubeba kutoka ng'ambo ni upi?:usikwepe swaliMimi utamaduni wangu ni kutafuta ukweli, dini yangu ni mapenzi.
Maalim Muhammed Said, pole kwa yaliyomkuta Baba yako, hata Baba yangu yako yaliyomkuta. Mimi nimemzungumzia Muasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni mtu very serious, alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo na hakutaka kabisa ujinga ujinga. Aliinyoosha nchi hii barabara kabisa kwa kuvunjilia mbali udini udini na ukabila ukabila ukabila kwa kuvunja uchifu.Paskali,
Mimi babu yangu Salum Abdallah aliwekwa kizuizini na hakuwa mtu mjinga.
Alikuwa mtu barabara sana.
1947 aliongoza ''general strike,'' dhidi ya wakoloni na akafanya hivyo 1949.
1953 alikuwa akihudhuria mikutano ya siri wakipanga kuundwa kwa TANU na
katika kundi lao wakamleta Germano Pacha Dar es Salaam kuhudhuria mkutano
wa TAA 1954 ulioasisi TANU.
1955 babu yangu akaasisi Tanganyika Railway African Union (TRAU) akiwa rais
muasisi.
1960 akiwa rais wa TRAU aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82.
Hii ilikkuwa haijapatapo kutokea.
Mgomo mrefu Afrika Mashariki ulikuwa ule wa Kenya ulioongozwa na Makhan
Singh.
Babu aliingoza TRAU ikishirikiana na TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hakuwa mtu, ''mjinga mjinga,'' au wa ''mchezo mchezo.''
Alikuwa na dereva wake Msukuma tulimpa jina, ''Msloopagas.''
Hadi leo sijajua jina lake halisi lilikuwa lipi.
Babu yangu aliwekwa kizuizini kwa sababu alitofautiana na Nyerere alipotaka
viongozi wa vyama vyama vya wafanyakazi wavunje vyama vyao pawepo na chama
kimoja nchi nzima chini ya TANU.
Katika watu waliompinga katika mkutano wa viongozi wa vyama vya wafanyakazi
uliofanyika Moshi alikuwa babu yangu Salum Abdallah.
Hii ndiyo sababu ya yeye kuwekwa kizuizini mwaka wa 1964 akisingiziwa kuwa alikuwa
mmoja wa watu waliokula njama ya kupindua serikali wakati jeshi lilipoasi Januari 20,
1964.
Babu yangu hakuwa mjinga wala mtu wa mchezo.
Sheikh! Neno linalowauma sana ni kusikia Waislam na Uislam katika harakati za ukombozi wa Tanganyika! Wakiwasoma kina Bwana Heri na Abushiri mitima inataka kuwapasuka!! Achilia mbali Mkwawa na Kinjekitile Mashujaa wa Taifa wanaojulikana lakini utambulisho wao ukizuiwa kujulikana kwa uwazi!Al Watan nimeandika kitabu kizima ambacho kinaitwa, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes the Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika." Umuhimu wake ni kuwa walijitolea kupambana na ukoloni.
Paskali,Maalim Muhammed Said, pole kwa yaliyomkuta Baba yako, hata Baba yangu yako yaliyomkuta. Mimi nimemzungumzia Muasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni mtu very serious, alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo na hakutaka kabisa ujinga ujinga. Aliinyoosha nchi hii barabara kabisa kwa kuvunjilia mbali udini udini na ukabila ukabila ukabila kwa kuvunja uchifu.
Paskali
Mkuu Maalim Mohamed Said, hakuna mpenda haki hata mmoja anayekerwa na ukweli. Hivyo hakuna mtu yoyote anayekerwa au kuumizwa na ulichoandika, ila kuwa sisi baadhi yetu ambao ni waumini wa nothing but the truth, hatukerwi na over amplification ya the role of Islam kwenye harakati za uhuru, bali tunakerwa na "the I'll motive behind" haswa pale historia hiyo inapokuwa na over emphasis zenye urongo ndani yake just to make believe Uhuru wa Tanganyika ni kazi ya watu wa dini fulani pekee na baada ya uhuru, watu wa dini hiyo were marginalised kitu ambacho sii kweli.Hakika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika imejaa Waislam kila kona.
Ukijaribu kuwaondoa utakuwa umetoa sehemu kubwa ya historia ya kweli.
Kuwa mimi nimeandika historia ya Waislam wala sikatai.
Hiyo ndiyo ilikuwa nia yangu khasa.
Ikiwa kuna mtu anakerwa na kuandikwa kwa historia hii hiyo ni bahati mbaya
kwake.
Hili ni katika jambo moja ambalo mimi sikulitegemea wakati naandika historia
hii.
Sikutegemea hata siku moja kuwa historia hii ya wazee wangu itawaumiza
baadhi ya watu.
Mwanamageuko,Sheikh! Neno linalowauma sana ni kusikia Waislam na Uislam katika harakati za ukombozi wa Tanganyika! Wakiwasoma kina Bwana Heri na Abushiri mitima inataka kuwapasuka!! Achilia mbali Mkwawa na Kinjekitile Mashujaa wa Taifa wanaojulikana lakini utambulisho wao ukizuiwa kujulikana kwa uwazi!
Huwa najiuliza kwanini "hawa jamaa zetu" wanaumia kwa chuki na hasama pindi uislam unapotajwa je ni zile chuki wanazopandikizana ama kuna jambo jingine limejificha maana tunahimizana utaifa huku wengine wakitajwa kuwa hawana sifa!!!
Mkuu Pasco, Je aliinyoosha nchi kwa kuwaweka watu waliomuonesha alipokuwa akikosea kizuizini ama?? Tuwatazame Kambona na bibi Titi walikuwa wadini au kuna jambo walilipinga halikumpendeza baba wa taifa na ndipo wakanyooshwa na matokeo ya makosa yale yanatugharimu mpaka leo. Mkuu Pasco Historia ya Tanzania toka awali hata kabla ya mjerumani hakukuwa na ubaguzi wa kikabila wala dini. Yako mema ya Mwalimu ni kuimarisha sio kuasisi ama kuvunja ukabila binafsi Babu yangu alioa mkewe wa kwanza Uvinza mwaka 1903 na hakubaguliwa kuwa si mwenyeji wa pale. Pia alioa mke wa pili Tabora 1918 hakubaguliwa, Najiuliza ingelikuwa kuna ubaguzi wale manamba waliopelekwa na mjerumani Tanga hali yao ingekuwaje ugenini? Yako mambo yanapotoshwa kwa makusudi na "wanaotunga" Historia na matokeo yake historia potofu inawatolesha watu povu!!! Mwalimu alitengwa hata na ndugu yake wakati wa kutafuta uhuru na akakimbilia Ikizu kwenye pango ambako alijificha akiandika katiba. Hili haliandikwi ndio maana hata Chief Makongoro Matutu wa Ikizu hajulikani!!! Ilikuwaje Mu Ikizu ampokee Mzanaki kama kungelikuwa na ubaguzi? Ilikuwaje wapwani wampokee mbara kwenye ubaguzi??Ilikuwaje waislamu wampokee mkristu na kumpa nafasi kwenye udini??? Wako walioujenga udini na wanaupalilia nani anawataja na kuwagusa??? 😀😀😀Maalim Muhammed Said, pole kwa yaliyomkuta Baba yako, hata Baba yangu yako yaliyomkuta. Mimi nimemzungumzia Muasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni mtu very serious, alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo na hakutaka kabisa ujinga ujinga. Aliinyoosha nchi hii barabara kabisa kwa kuvunjilia mbali udini udini na ukabila ukabila ukabila kwa kuvunja uchifu.
Paskali
Paskali,Mkuu Maalim Mohamed Said, hakuna mpenda haki hata mmoja anayekerwa na ukweli. Hivyo hakuna mtu yoyote anayekerwa au kuumizwa na ulichoandika, ila kuwa sisi baadhi yetu ambao ni waumini wa nothing but the truth, hatukerwi na over amplification ya the role of Islam kwenye harakati za uhuru, bali tunakerwa na "the I'll motive behind" haswa pale historia hiyo inapokuwa na over emphasis zenye urongo ndani yake just to make believe Uhuru wa Tanganyika ni kazi ya watu wa dini fulani pekee na baada ya uhuru, watu wa dini hiyo were marginalised kitu ambacho sii kweli.
Mimi ni miongoni mwa waumini wa Nyerere, whatever he did kwa kuzivunjilia mbali taasisi zenye mwelekeo wa kuleta fundamentalism Tanzania, he did it in good faith, and thanks to him tuko hapa tulipo kwa kazi yake nzuri iliyotukuka, otherwise saa hizi tungekuwa tunazungumza mengine.
Paskali.
Allah akulipe na akuwezeshe zaidi na zaidi InshaAllah.Mwanamageuko,
Hatuwezi kufuta historia hii itabidi wastahamili tu.
Kitabu nimekiandika cha historia hii na sasa tunakwenda
toleo la nne.
Asante, tuendelee na mnakasha ila uwezo to read in between the lunea, "the ill motive behind" maandiko fulani, is very important tool kuzuia kuwa carried out na the intended "ill motives" zinazojificha ndani ya maandishi fulani yenye nia ovu ya kupanda mbegu fulani za udini udini in a pretext ya kuhifadhi historia za mababu zetu!.Paskali,
Sina ugomvi na fikra zako wala sikuzuii kuamini na kuandika upendacho.
Mie naandika historia kama niijuavyo na wala simlazimishi mtu kuniamini.
AminAllah akulipe na akuwezeshe zaidi na zaidi InshaAllah.
Mkuu Pasco msome Madaraka Nyerere anavyorudia kuandika historia kisha nayeye umuweke kwenye fungu hilohiloAsante, tuendelee na mnakasha ila uwezo to read the motive behind andiko fulani ni very important tool kuzuia kuwa carried out na the ill motives zinazojificha ndani ya maandishi fulani yenye nia ovu ya kupanda mbegu fulani za udini udini in a pretext ya kuhifadhi historia za mababu zetu!.
Tunamshukuru sana Mwalimu Nyerere, naye alikuwa na uwezo huu na kiukweli aliinyoosha bila kujali walichangia nini kwenye TAA au kwenye kuasisi TANU!.
Paskali