Bila ya kibali marufuku "Live coverage" Ikulu

Bila ya kibali marufuku "Live coverage" Ikulu

Status
Not open for further replies.
hii ikulu yetu mataifa ya kigeni yanaijua vizur kulko yanavozijua nyeti zao wenyewe!!

mfano CIA alipokuja obama watakua walipekenyua mpk vitanda vya mkwere

Tuache utani tunahitaji kujenga ikulu mpya hii ya mkoloni haifai tena, fikiria imejengwa na mjerumani sijui ni ya miti na fitto ikakandikwa udongo manake wakati ule walitoa wapi saruji! haina hata lift ya kupanda ghorofani, Uganda na Kenya wameshajenga ikulu mpya tumebaki sisi tu.

Haya ndo yaliyosababisha wafaransa wakamkamata gagbo akiwa amelala kitandani kwani walijua chocho zote za ikulu na wao ndo walioijenga. mwinyi aliikuta haina hata uzio akijitahidi akaweka japo uzio, mkapa akakuta paa linavuja akaweka supaglue kikwete kaweka angalau ukumbi wa mikutano, mwishowe itakuja poromoka kwa ukarabati usioisha.
 
Hiyo dunia imepitwa na wakati. Mi nikitaka kujua ikulu pakoje google earth ipo hakuna cha unyeti wowote ule. Ss hapo watakapopewa ruhusa watakuwa wanaonesha mawingu? Kwa hali ya kawaida hata kuingia ikulu lazma upate ruhusa hata kama unataka kwenda kuomba chumvi.

Google earth ipo. Endelea ku google tu
 
Sijaelewa hiyo taarifa.live coverage ya wapi? Au mimi ndio sielewi??? Incomplete and an ambiguous statement to say the least

Live coverage ya mambo yoyoye yanayofanyika Ikulu. Ilizoeleka waandishi kuibukia Ikulu na kamera zao bila utatatibu. Ikulu siyo baa ambapo yeyote anaweza kuingia na kutoka bila utaratibu. Waandishi hawajazuiliwa kufanya live coverage, jambo la msingi ni kuomba kibali na kukubaliwa.
 
Hivi Rweyependeza bado yupo kweli?
 
Hivi Rweyependeza bado yupo kweli?au wamemteua yule mkulungenzi wa gazeti la JAMUHURI
 
Taratiiibu mtaanza kumkumbuka mkwere!!@
 
Wanapiga marufuku live coverage bila kibali ila bado email wanatumia za gmail...... haya bana
 
Tuacheni ujuha na ushabiki. Ikulu ni sehemu nyeti kwa nchi yoyote. Juzi ITV walikuwa wanazunguka maeneo mbalimbali ndani ya Ikulu wakiwa live kila mtu anaona lazima tuwe wakweli haikuwa sahihi ki usalama wa nchi yoyote. Mimi nakubaliana na hoja kukiwa na tukio lolote vyombo vya habari viombe kibali vipewe mwongozo ni maeneo gani wanaruhusiwa kurusha live. Siyo kila eneo linarushwa live kila mtu anaona. Tusijitoe ufahamu juu ya usalama wa nchi kana kwamba hatuelewi kwamba usalama wa nchi yoyote kitovu chake ni Ikulu


Sasa shabiki na juha ni nani, mimi au wale walioacha ITV waingie kila chumba kufanya live coverage live?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom