Salaam Wana JF
Nilikuwa nasafiri kuelekea mkoa fulani hivi, kwakweli kama nchi tumejitahidi kufanya Maendeleo, kila baada ya umbali kadhaa unaona miradi ya Barabara inaendelea. Kuelekea nchi ya ahadi japo kuna watu wanaponda juhudi za serikali lazima tujue kuwa hata Roma haikujengwa kwa siku moja, development is a process.
Ukija kwenye suala la amani serikali chini ya mwamvuli wa CCM imejitahidi kujenga misingi ya undugu kwakuwa hakuna ukabila wala aina zozote za kubaguana. Kwa hili CCM wanahitaji pongezi kubwa japokuwa kuna changamoto kubwa kutoka kwa watu mbali mbali.
Tukubali tu kuwa vyama vya upinzani bado sana kupata ukomavu wa kuongoza nchi hii sababu wana siasa za vurugu, hakuna democracy with themselves + siasa za kugawa nchi. Yote kwa yote CCM tuwape maua yao.
NB: Kama kusingekuwa na CCM basi nchi ingekuwa kama Somali, Sudan, CAR etc. Je, kama Mtanzania unaonaje hili?
Nakala waione;
Mshana Jr
Erythrocyte