Bila Rapid Test Kits tutapoteza wengi wasio na Corona kuliko walio na Corona

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,312
Huu ni ushauri tu, tena ambao unatakiwa upewe priority kubwa kuliko chochote kile.

Kwa sasa ukienda hospitali yoyote first impression wanayokujengea ni kwamba una COVID19. Na kwa bahati mbaya sana wale wenye chronic conditions kama kisukari, ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa ini, hypertension wanapresent na dalili kuu ya COVID19 ambayo ni kupumua kwa shida.

Sasa ukifika hospitali yoyote na ukaonekana una shida ya kupumua obviously watahitaji kujiridhisha kwanza kama una COVID19 ama laah.

Kwa hali hii Rapid test kits zinatakiwa ziwepo kila hospitali/kituo cha afya/dispensari. Hizi zinaondoa chaos zote zinazoendelea kwa sasa za wagonjwa kuzungushwa huku na huko hasa jiji la Dar.

Jijini Dar malalamiko ya wagonjwa kukataliwa hospitali yamekuwa mengi na mpaka wengine wanafia njiani ama nyumbani. Mbaya zaidi wakifa serikali inazuia mwili wajiridhishe kama ni COVID19 ama sio ndipo mruhusiwe kuendelea na mazishi. Wakikuta ni COVID19 serikali inahusika na mazishi.

Kwa rate ya maambukizi ilivyo sasa haiwezekani kuendelea kutegemea PCR ambayo mchakato wake wa kupata majibu ni mrefu. Kwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa haraka wanakufa hata kabla ya hayo majibu kutoka. Na huwezi kuwalaumu wafanyakazi wa afya kwa sababu kwenye milipuko ya magonjwa kama haya wanatakiwa wajiridhishe kwanza ili wajue wanajilinda vipi.

Serikali leteni rapid tests, hizi haziepukiki. Kuweni proactive ili kudhibiti huyu mdudu kuenea. Kwa nini mko nyuma sana kwenye kuchukua hatua stahiki. Sababu mnaweza kujifanya hamnunui hizo kits sasa lakini mwisho wa siku mtakuja kununua tu.

images.jpg
images%20(1).jpg
 
Jiwe anasema ni ka kirusi ka kawaida tu badala ya kuomba misaada, tuna uhusiano mzuri na nchi kama South Korea ambao wametengeneza rapid test kit kibao, juzijuzi wametoka kuzituma nyingi mno marekani zinatoa majibu ndani ya saa moja tu. Badala ya kukaa tukajaribu kuwasiliana na nchi zenye high tech kama hizi zitupe msaada au ziweze kutuuzia kit kwa bei nafuu tunakaa kusema fungeni muombe, alafu mjifukize. Nyoooooko we are doomed kuongozwa na kilaza
 
Tatzo Tanzania hatunaga akiri ya kuzuia tatzo mapema tunasubiriaga had hali iwe mbaya ndo tuanze kuangaika
 
Back
Top Bottom